Pre GE2025 Same: Polisi yazuia mkutano wa hadhara wa Tundu Lissu, yasema ni kufanya kampeni uchaguzi S/Mitaa kabla ya muda

Pre GE2025 Same: Polisi yazuia mkutano wa hadhara wa Tundu Lissu, yasema ni kufanya kampeni uchaguzi S/Mitaa kabla ya muda

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nchi ngumu sana hii,mbona Nchimbi na Makalla kila siku wapo mikutanoni mikoani huko??hii ni double standard,moja ya kazi za kipumbavu nilizowahi kufanya ni kuajiriwa na Jeshi la Polisi Tanzania,nashukuru Mungu niliacha kazi
Ww tutakibao ww
 
Jeshi la Polisi wilayani Same, mkoani Kilimanjaro limezuia mkutano wa hadhara uliokuwa umepangwa kufanywa na Makamu Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Bara, Tundu Lissu tarehe 6 Novemba 2024, na mkutano mwingine wa chama hicho uliopangwa kufanyika tarehe 8 mwezi huu Novemba.

Kulingana na barua kutoka kwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Same ya tarehe 5 Novemba, 2024 kwenda kwa CHADEMA Same, uamuzi huo umetokana na sababu ya kuwa katika kipindi cha maandalizi ya kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambazo zitaanza rasmi tarehe 20 Novemba 2024.

Katika barua hiyo, Polisi wamesisitiza kuwa mikutano hiyo inaonekana kama kampeni, ambayo hairuhusiwi kufanyika kwa wakati huu hadi kufikia kipindi rasmi cha kampeni.

"Ofisi hii inakujulisha kuwa imesitisha mikutano yako ya hadhara miwili ambayo ulipanga kuifanya tarehe 06/11/2024 Ndungu, na tarehe 08/11/2024 Same mjini."

"Hii ni kutokana kwamba kufanya kwako mikutano hiyo ni sawa na kufanya kampeni ya uchaguzi wa serikali za mitaa kabla ya muda wa kampeni kufika na kampeni inatarajiwa kuanza tarehe 20/11/2024," imeeleza barua hiyo.

CHADEMA, kupitia Katibu wa chama hicho Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema wameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuwanyima haki ya kufanya mikutano ya kuhamasisha wananchi na kujenga uelewa wa uraia kwa Watanzania.

Aidha Lema amesema kuwa: "Polisi wamesema wamezuia mikutano yote ya siasa mpaka pale tutakapozindua kampeni tarehe mwezi huu, kwamba haturuhusiwi kufanya mikutano ya kisiasa kwa wakati huu....."

"Kwakuwa eti tunajiandaa kufanya kampeni za wiki nzima kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Nimewauliza hiyo ni sababu ya aina gani? Maana sisi (CHADEMA) hatuendi kwa ajili ya kupiga kura, tunakwenda kwa ajili ya kuwahamasisha wananchi na kuwajengea uraia mwema", amesema Lema.
Kwanini sasa wanafanya Kampeni kabla ya muda wakati wanajua ni kukiuka sheria za uchaguzi
 
Back
Top Bottom