Ukweli usemwe TATIZO sio Jeshi la polisi.
TATIZO ni wale wanaolitumia kuficha maovu Yao .
Polisi ni Kama kuku wa Kienyeji wameachwa wafanye wanavyotaka Kwa sababu mabosi Wao wananufaika na mapungufu ya kisheria na wananchi kutojua Haki ZAO.
SERIKALI iliyojaa rushwa kule JUU Siku zote inawapumbaza wananchi Kwa kupambana na virushwa uchwara vya polisi.
Ukitaka Ujue ni Vipi polisi wanafanya KAZI ZAO Angalia aina ya viongozi wanaopandishwa vyeo na kuwa makamishna . Wengi ni wale Wenye sifa ya kupenda anasa ,rushwa ,ngono na Ulevi. Sasa wanalewaje Kila Siku na anasa kama SIO michongo na madili ya rushwa na magendo au kushirikiana na Wahalifu. ?
Wengi ni ZAO la CCM na SERIKALI yake katika kubebena wakati Wa Uchaguzi.
Ni Vipi mabosi wanaohamasisha kuandika Faini tuu Badala ya KUTOA elimu Barabarani waweze kuwafanya askari wasilalamikiwe. Mbona Taasisi nyingine Kuna rushwa kubwa sana Lakini hakuna kelele. Jibu ni kuwa polisi wanakula rushwa lakini pia wanaosimamia Sheria zote za Nchi Hali inayosababisha Kila MTU akutane na polisi KWENYE matukio yote.
Hata hivyo tuache unafiki . Kama Kweli SERIKALI Iko sirias kulibadili Jeshi la polisi Jambo la kwanza ni kuliondoa KWENYE Médani za kijeshi na kuwa ni watoa huduma Kama walivyo watumishi WENGINE mana wanakutana na watu Wenye mahitaji mbalimblia SIO Wahalifu tuu.
Huwezi kubadili Hulka za polisi wakati mafunzo Yao ni ya kibabe ,kikatili,kujuana ,rushwa , Bila kujali kuwa wanakwenda kuwahudumia watu Wa aina zote ikiwemo Watoto na wazee. Unakuta polisi anampiga vibao na mateke mtoto Wa Miaka Mitano kisa ameletwa na mama yake kuwa hataki Shule . Chanzo ni mafunzo yaliyojaa ukorofi Badala ya KUTOA huduma Kwa weledi na kumsimamia Haki na utu .
Lakini pia Namna ya kupata Wakuu Wa Jeshi hilo ni changamoto sana mana wanapatikana kisiasa na kuteuliwa kama dili Badala ya MALENGO ya kuihudumia jamii. MTU akipewa mkoa kama Arusha ,Mbeya Mwanza ,Dar es salaam basi Ujue Kuna MTU amemuweka Ili kujinufaisha kupitia wafanyabiashara haramu na kulinda Mali za watu Fulani.
Wahali wakubwa hawawezi kuguswa kwenye mifumo Kama hiyo .
Badilisha polisi kuanzia Namna wanavyoteuliwa na kupeana Maeneo yenye ulaji Wa kushirikiana na Wahalifu wakubwa Kama wauza madawa,magendo,wakwepa Kodi na wengineo.hakuna Bosi anayependa Kwenda KUFANYA KAZI Sehemu isiyo na uhalifu mkubwa unaofanywa na matajiri . Nini Maana yake ni kwamba kuna uhusiano Mkubwa sana kimaslahi.
Ingewezekena wangepiguwa kura zansiri Ili kuwataja wale wakubwa wanaoendekeza uhalifu na rushwa Bila kujali Haki za wananchi wanyonge.
Lakini wale Wa usalama Barabarani wanapewa mamlaka na kuwa na Sheria nyingi sana za usalama Barabarani zisizotekelezeka na nyingine ni usumbufu tu.
Askari Wa Barabarani Tanzania ni Wazuri ukilinganisha na Wa nchi Jirani. Wana ustarabu ZAIDI.Barabarani Kuna kanuni nyingi ambazo zinatoa Mwanya Wa Rushwa.
Ingewezekena kungefungwa kamera na kuandika Faini zinazoweza kulipwa Bila kukamata gari kupitia akaunti za benki na miamala mingineyo.
Hii ingepunguza usumbufu na dhana ya kuonewa Barabarani japo sio kuonewa Bali ni Sheria KUTOAwanya Wa uonevu.
Umaskini ni TATIZO kubwa mana Askari Kwa Mishahara Yao midogo wakijifanya kuwa waadilifu wangi watachekwa sana wakistaafu mana Hata vinwamgongo vyao ni vidogo sana. Wale walarushwa wanasifiwa na jamii mana jamii imejaa rushwa hivyo anayekula rushwa na kujijenga anapata Heshima kubwa na pongezi nyingi hasa anapostafu.
CCM imeshindwa kusimamia Kila kitu ikiwemo Jeshi la polisi Wala wasijaribu kurusha lawama Kwa polisi.
Kila Idara imefeli mana siasa imeshika Hatamu.