Samia: 70% wanalinyooshea kidole jeshi la polisi

Hao wanajeshi wanatokea nchi Gani?

Jamii ni corrupt kuanzia JUU mpaka chini halafu utegemee kuwa na jamii yenye watumishi waadilifu?

Unajua ufisadi unaofanywa na mawizara hayo unayoyasifia . ?

Hiví unajua Miaka ya 1980 Kuelekea 90 mpaka 2000 majambazi waliokuwa wanateka mabasi na malori walikua ni Akina nani?

Unajua kama SIO mission za kimataifa Leo hii wanajeshi wetu wangekua na maisha magumu kuliko mtumishi yeyote duniani na ambacho kingetokea ni Mapinduzi.
Unajua maslahi ya mabosi Wa JUU ya Jeshi ni Kwa nini ni makumbwa ?

Leo ukiona mwanajeshi Amejenga nyumba SIO Mshahara anaolipwa na Taifa lake Bali ni pesa za UN zinazotokana na vita za kisiasa KWENYE nchi nyingine.
Tumshukuru Mungu nchi nyingine Zina vurugu mana tusingeweza kukabiliana na mtiti Wa wanajeshi Wenye njaa.

Ukitaka kujua jamii ilivyokaa Angalia Walimu wetu Wa Shule , maprofesa Wa vyuo, wakuu Wa wilaya na mikoa n.k. wanavyotumia Nguvu na ubabe na vitisho kufifisha Haki za watu.

Rushwa IPO Hata KWENYE taeuzi Kuna rushwa za ngono,vyuoni Kuna rushwa ya ngono n.k. Sasa kama maprofesa wasomi wanafaulisha wataalam Kwa rushwa ya ngono na IPO wazi lakini Kwa sababu inawahusu wasomi Kwa maslahi Yao Inaonekana ni NZURI kuliko ya polisi na Sheria za hovyo zinazoweka mianya ya rushwa.

Kama Mama Samia anataka kuwafanya Watanganyika wachukie rushwa ni vema akakubali mabadiliko ya Katiba yatakayoleta mfumo mpya Wa utumishi na kuipa Nguvu tume ya maadili. Rushwa yote ni watu kutaka kulimbikiza Mali .
Hakua MTU anayemuuliza mtumishi Wa umma kuwa amewezaje kujenga nyumba kumi Kwa muda mfupi Wakati wenzake Wenye Mshahara kama wake hawana Hata nyumba Moja? Lazima pawe na kuulizana mana ni watumishi Wa umma.Wahalali wajulikane
 
Mmatumbi unahasira kweli umetema nyongo hapa kwa hakika watakupata.
 
Yule mwovu aliyeko motoni ndiye aliliharibu kabisa hadi limekuwa majambazi wanaovaa uniform. Kuwashirikisha polisi kwenye wizi wa kura nalo limechangia jeshi hili kuwa washirika wa maovu ya watawala waovu.
 
Polisi ni mahakama siku hizi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…