Samia Aifungulia Russia Mlango wa Uranium Namtumbo: Je, Marekani Itavumilia?

Ryan Holiday

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
3,499
Reaction score
5,956
Katika hatua ya kushangaza na inayozua maswali mengi, serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imewapa Warusi mradi wa majaribio wa uchimbaji wa uranium, Namtumbo - Ruvuma. Uranium ni moja ya rasilimali nyeti duniani, inayotumika katika uzalishaji wa nishati ya nyuklia lakini pia inaweza kuwa kiungo muhimu katika uundaji wa silaha za maangamizi makubwa. Kwa taifa kama Tanzania, ambalo linaendelea kutafuta mwelekeo wa kiuchumi kupitia diplomasia ya uchumi, uamuzi huu unazua maswali mengi kuhusu usalama wa taifa, uwazi wa mikataba, na hatari za kidiplomasia.

Zaidi ya hayo, hakuna taarifa ya kutosha kwa wananchi kuhusu mkataba huu. Ni nani aliyehusika? Ni kwa muda gani? Ni kwa masharti gani? Je, serikali imefanya tathmini ya kina kuhusu athari za kimazingira, kijamii, na kiusalama? Na je, tuna uwezo wa kusimamia kwa karibu shughuli za Warusi kuhakikisha kuwa uranium yetu haitumiki kwa malengo mengine yasiyojulikana?

Uranium si mchanga wa ujenzi ni silaha ya kisiasa na kiusalama
.​
 
Kwa taarifa yako tu ,russia ndio kinara wa trcknolojia ya nuclea duniani ,kama hujui ni vyema ukaacha kushapalia ujinga wa hawa mabeberu .Kwa taarifa yako ,zaidi ya asilimia hamsini ya ujenzi wa viwanda vya nishati ya nuclea vinavyojengwa hapa duniani muda huu Russia ndio anajenga.KIMA MKUBWA
 
Matusi ya nini sasa?
 
Kulikuwa na haja gani ya kumtukan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…