Samia Aifungulia Russia Mlango wa Uranium Namtumbo: Je, Marekani Itavumilia?

Samia Aifungulia Russia Mlango wa Uranium Namtumbo: Je, Marekani Itavumilia?

Katika hatua ya kushangaza na inayozua maswali mengi, serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imewapa Warusi mradi wa majaribio wa uchimbaji wa uranium, Namtumbo - Ruvuma. Uranium ni moja ya rasilimali nyeti duniani, inayotumika katika uzalishaji wa nishati ya nyuklia lakini pia inaweza kuwa kiungo muhimu katika uundaji wa silaha za maangamizi makubwa. Kwa taifa kama Tanzania, ambalo linaendelea kutafuta mwelekeo wa kiuchumi kupitia diplomasia ya uchumi, uamuzi huu unazua maswali mengi kuhusu usalama wa taifa, uwazi wa mikataba, na hatari za kidiplomasia.

Zaidi ya hayo, hakuna taarifa ya kutosha kwa wananchi kuhusu mkataba huu. Ni nani aliyehusika? Ni kwa muda gani? Ni kwa masharti gani? Je, serikali imefanya tathmini ya kina kuhusu athari za kimazingira, kijamii, na kiusalama? Na je, tuna uwezo wa kusimamia kwa karibu shughuli za Warusi kuhakikisha kuwa uranium yetu haitumiki kwa malengo mengine yasiyojulikana?

Uranium si mchanga wa ujenzi ni silaha ya kisiasa na kiusalama
View attachment 3424831.​
Kaka tuambie mkataba gani umewekwa wAZI TANGU ENZI ZA MARAIS WALIOPITA
 
We ulidhania hiki kiburi anakitolea wapi?😂😂😂 Picha la kutisha limeanza sasa. Mtaelewa ni kwann tulikosea kumpa mwanamke nafasi nyeti kama urais.
 
Tatizo lako ni nani anayechimba au ni namna gani kinachochimbwa kitainufaisha nchi?Maana hueleweki unataka nini.Kwasababu sisi wenyewe hatuwezi kua na matumizi ya hiyo kitu bila kumuhusisha mtu mweupe kwa namna yoyote kwasababu ata ugunduzi na utafiti wanafanyaga hao hao sisi karunguyeye kazi yetu nikutoa macho tu.Sisi tuangaike na tutanufaikaje sio nani anachimba.
 
Haupaswi kuwa uhalali wa kuendelea kufanya hivyo. Tunahitaji mabadiliko sio mazoea. Now, things are changing too fast.
Mabadiliko sio kwenye kila kitu.Hakuna jambo la kila mtu duniani.Lazima kuwe na wachache wanaolifanyia maamuzi aidha kwa manufaa ya wengi au wachache.Wabongo walivyo wajuaji mkiwekewa kila kitu wazi hakuna kitakachofanyika.
 
Kwahiyo ulitaka apewe Marekani, sio?
Wenda sisi watanzania sio mpango wa Mungu.
Marekani amekuwa mshirika wetu wa muda mrefu. Amefanya mambo mengi ya kimaendeleo kwa jamii ya watu Watanzania hivyo mkukaribisha adui wake namba moja kwenye Taifa letu, kuna uwezekano mkubwa wa kuathiri diplomasia yetu na Marekani.
 
Back
Top Bottom