Samia Aifungulia Russia Mlango wa Uranium Namtumbo: Je, Marekani Itavumilia?

Samia Aifungulia Russia Mlango wa Uranium Namtumbo: Je, Marekani Itavumilia?

Katika hatua ya kushangaza na inayozua maswali mengi, serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imewapa Warusi mradi wa majaribio wa uchimbaji wa uranium, Namtumbo - Ruvuma. Uranium ni moja ya rasilimali nyeti duniani, inayotumika katika uzalishaji wa nishati ya nyuklia lakini pia inaweza kuwa kiungo muhimu katika uundaji wa silaha za maangamizi makubwa. Kwa taifa kama Tanzania, ambalo linaendelea kutafuta mwelekeo wa kiuchumi kupitia diplomasia ya uchumi, uamuzi huu unazua maswali mengi kuhusu usalama wa taifa, uwazi wa mikataba, na hatari za kidiplomasia.

Zaidi ya hayo, hakuna taarifa ya kutosha kwa wananchi kuhusu mkataba huu. Ni nani aliyehusika? Ni kwa muda gani? Ni kwa masharti gani? Je, serikali imefanya tathmini ya kina kuhusu athari za kimazingira, kijamii, na kiusalama? Na je, tuna uwezo wa kusimamia kwa karibu shughuli za Warusi kuhakikisha kuwa uranium yetu haitumiki kwa malengo mengine yasiyojulikana?

Uranium si mchanga wa ujenzi ni silaha ya kisiasa na kiusalama
View attachment 3424831.​
Hii project ilikuwepo tangu 2013 na tathmini ya mazingira ilifanyika, na pia eneo la Selous linalohusishwa na mradi liliondolewa rasmi na UNESCO as an area within the Heritage Site.
 
Marekani wanahusikaje kwenye uranium iliyoko Tanzania? Acha fikira za kitumwa.

Russia imeinvest kwenye mataifs ya deposits kubwa ya uranium kuliko Tanzania kama Namibia, Kazakhastan na Niger

Na Marekani haijaishobokea itakuwa sembuse uranium ya Tanzania!
​
Kubali au ukatae lakini baki nalo kichwani mwako kwamba Afrika bado tunatawaliwa na huo ndiyo "Ukweli mchungu".
 
Hii project ilikuwepo tangu 2013 na tathmini ya mazingira ilifanyika, na pia eneo la Selous linalohusishwa na mradi liliondolewa rasmi na UNESCO as an area within the Heritage Site.
Kwenye ishu za Mazingira uwa sikupingi hata kidogo. Najua upo nondo kweli kweli.
 
Kubali au ukatae lakini baki nalo kichwani mwako kwamba Afrika bado tunatawaliwa na huo ndiyo "Ukweli mchungu".
Suala la Marekani kuingilia Tanzania kisa Russia wamewekeza kwenye uranium sahau hakuna kitu kama hicho​
 
Suala la Marekani kuingilia Tanzania kisa Russia wamewekeza kwenye uranium sahau hakuna kitu kama hicho​
Ndiyo maana nikaandika "Je, Marekani atavumilia?'' swali nimeliacha kwako na ahsante kwa jibu lako.
 
Niliwahi andika uchaguzi wa 2025 October ni vita vya kijasusi kati ya mashirika ya kijasusi ya kichina,kirusi KGB,kiarabu na co dhidi ya marekani CIA,mossad,M16 na co dhidi ya umiliki wa rasilimali zetu na mgombea wa urais yeyote atawakilisha mashirika hayo na kushinda au kushindwa kwa mgombea ni ushindi au kushindwa Kwa mashirika hayo!!

Ngoja tuone huo mnyukano!
 
Marekani amekuwa mshirika wetu wa muda mrefu. Amefanya mambo mengi ya kimaendeleo kwa jamii ya watu Watanzania hivyo mkukaribisha adui wake namba moja kwenye Taifa letu, kuna uwezekano mkubwa wa kuathiri diplomasia yetu na Marekani.
Hizi Barabara kubwa kubwa kabla ya mwaka 2000 hazikuwepo, unajua sababu?
 
Ndiyo maana nikaandika "Je, Marekani atavumilia?'' swali nimeliacha kwako na ahsante kwa jibu lako.
Kama huko pengine Marekani ilivumilia uwekezaji wa Russia kwenye migodi ya maana ya uranium ndiyo ashindwe kuvumilia ya Tanzania?​
 
Je, una uhakika gani wanaweza ku-offer misaada na maendeleo aliyokuwa anaitoa Mmerakani kwa Tanzania karibia katika sekta zote.
Misaada ya kusenge hatutaki kwa kweli kama inaunganishwa na kuwa lazima tukubali ushoga na usagaji na ndoa za jinsia moja
.wabaki na pesa zao hatutaki tutaenda tu na wachina na waarabu kwenye biashara na uwekezaji hata kama hawatupi misaada
 
Acha tutumie huu umeme wa maji, technology ya kuzalisha umeme wa nuclear bado sana kwa sasa tupambane kuacha matumizi ya kuni na mkaa.
Uho ukija ni uhakika no kukatika katika na treni kukwama kwama njian ili iundwe tren ya umeme toka dar uo kigoma
 
Kwa taarifa yako tu ,russia ndio kinara wa trcknolojia ya nuclea duniani ,kama hujui ni vyema ukaacha kushapalia ujinga wa hawa mabeberu .Kwa taarifa yako ,zaidi ya asilimia hamsini ya ujenzi wa viwanda vya nishati ya nuclea vinavyojengwa hapa duniani muda huu Russia ndio anajenga.KIMA MKUBWA
Kwamba Russia kwenye ubeberu haimo?!
 
Warusi ni wataalam wa nuclear duniani pia hawana restriction nyingi.
Urusi ndio nchi iliyowahi kusababisha ajali kubwa zaidi ya nuclear duniani kutokana na uzembe na siasa, Chernobyl mwaka 1986.
 
Faida kwa WaTz na Mkataba unasemaje??

Ni jambo jema.
 
Kwa taarifa yako tu ,russia ndio kinara wa trcknolojia ya nuclea duniani ,kama hujui ni vyema ukaacha kushapalia ujinga wa hawa mabeberu .Kwa taarifa yako ,zaidi ya asilimia hamsini ya ujenzi wa viwanda vya nishati ya nuclea vinavyojengwa hapa duniani muda huu Russia ndio anajenga.KIMA MKUBWA
Kwani amekosea wapi mpaka una mtukana !?
 
Back
Top Bottom