Samia aizika CCM rasmi: Ugonjwa wa mbeleko za kisiasa zaanza kuitafuna CCM yenyewe

walichofanya ni sahihi. hata wakimteua mtu mwingine na yeye atatekeleza ilani ya ccm hiyo hiyo

pia ni gharama sana kumtunza rais mstaafu, sioni kama ni sahihi kujiingiza gharama hiyo kwa mtu aliyetawala miaka minne tu, stress za kazi ya urais anapaswa azipate miaka mingi kama wenzake

sio atawale mda mchache halafu apewe pensheni na benefits zote za kikatiba sawa sawa za watu waliotawala miaka 10
 
19 January 2025
Dodoma, Tanzania

Wanakutaka

Kikwete Aitwa Kuingilia Suala la Kumtangaza Rasmi Samia Mgombea CCM 2025, Atoa Msimamo: 'Wanakutaka'


View: https://m.youtube.com/watch?v=8C0iBzeTyH0
Mkutano mkuu maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaofanyika jijini Dodoma, Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete. Leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huu maalum uliowakutanisha wabunge zaidi ya 1900, na kuhudhuiwa na watu zaidi ya 5,000
 
Hujui kitu wewe vyama vyote vya siasa ikiwemo Chadema mgombea uraisi mgombea anatakiwa wanachama wamuombe agombee sio tu kwenda kununua fomu kugombea kama alivyofanya Lisu

Hana mwanachama hata mmoja akiyemuomba agombee huo uenyekiti na huyo Odero pia

Mbowe kaombwa na wanachama agombee ndio akaenda kuchukua fomu

Lisu na huyo odero walienda tu kununua fomu hakuna mwanachama hata mmoja aliyewaomba wagombee

Kuwa tunakutaka kagombee na fomu tutakulipia
 
CCM ilikufa kitambo

Mbadala ndio hayupo

c.c Pascal Mayalla

Huyu mama hatataka hata ushindani, changamoto, kushindana na yoyote hata kufuata mchakato, utaratibu wowote yeye ni kufanya anavyojisikia.

Pamoja na kwamba hakuna mbadala thabiti, tunamuhitaji Lissu na Chadema kuliko wakati wowote walipiganie hili taifa kupata katiba mpya, tume huru, kuondoa ufisadi, rushwa, kuuzwa kwa rasilimali za umma ovyo. Na sisi wengine wote tumuunge mkono Lissu na timu yake kuikomboa Tanganyika na Tanzania.

Muhimu sana twende na No reform no election.
 
Baadhi ya Maoni mitandaoni :

1. Rais Samia anamalizia muhula wa mtangulizi wake baada ya kutangulia mbele za haki. Katiba haikupindishwa, akaingia madarakani. Sasa huu utaratibu wa kumtangaza kuwa mgombea pekee bila kufuata mchakato wa kumpata mgombea upo kwenye Katiba au ni mabavu yanatumika?


2. ULE UTARATIBU WA KUCHUKUA FORM VIPI? HAUPO MWAKA HUU 2025?

3. Mbona Bado mnaogopa kwenda kwenye sanduku la kura? Ni kweli ujanja ujanja unawadhalilisha sana bila sababu za msingi.

4. Yaani tayari wameisha mpitisha kugombea Urais naye anakubali huo utaratibu ili kilichobakia iwe ni kuhakikisha wanahalalisha kisheria ,...na wajumbe wanashangilia mmmmmh hivi hawa wajumbe kweli hawana uwezo wowote wa kujenga hoja kupisha demokrasia ya kweli ndani ya chama chao kuhakikisha kuna kuwako na ushindani wa kweli ....kweli tuna safari ndefu kujenga demokrasia ya kweli katika nchi hii


5. Nimebaini CCM yangu watu HAWANA AKILI. Kwanini mnakwepa kumpitisha Samia kwenye Vikao Rasmi za Chama sawa na Katiba ya CCM? Mnaogopa nini? JK mwenyewe nchi ilimshinda, ndo amekuwa Wakili wa Chama??
 
Hakuna shida

Sababu hatutegemei kura za walala hoi. Kwa msaada wa Polic and tume atashinda tena kwa 100%.

Inabakia kazi ya kuteua wabunge kwa sababu hata wao hawategemia kura za mlala hoi
 

naona kama kuna nusu mlingoti soon
 
kama wenye Chama chao wanakubaliana na hali hiyo sioni kama kuna tatizo lolote !
🙏
 
Mungu ingilia kati kabla ya uchaguzi. Chukua watu
Aamue Ugomvi, CCM Imepasuka Vipande Vipande
Sura /Mioyo Ya Watu Imeinama, Watajua Sasa Umuhimu Wa Kufuata Utaratibu
Nchi Hii Wasomi Hawajulikani Wasiosoma Angalau Wanajielewa

Ubwabwa, Posho, Guest Za Bure, Mabasi Waliyopanda Yatawatokea Puani Watakapofika Mikoani Kwao, Na Kutafakari Kwa Kina Sana. Watagundua Wajumbe Wote Wamekosea Sehemu Kubwa Kuitikia Ndiyoo


Kuusigina Mpango, Kanuni, Taratibu Za Chama Chao Walizojiwekea
Wamekwenda Kuwabana Wote Ndani Ya CCM Bara Na Visiwani
Kuwa Nafasi Ya Rais Imeshajazwa Tayari Bila Utaratibu
 
Ni aibu kubwa kwa Taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…