Samia aizika CCM rasmi: Ugonjwa wa mbeleko za kisiasa zaanza kuitafuna CCM yenyewe

Leo huko DODOMA wametangaza rasmi wagombea wa CCM wa nafasi ya rais wa JMT na rais wa Zanzibar.

Kama mnavyojua kwenye siasa hakuna kitu cha bahati mbaya, ni dhahiri huo mpango wa kumpitisha Samia na Hussein Mwinyi kuwa wagombea kwa Kuwashtukiza wanachama ulisukwa mapema. Kwa hiyo hata kikao hiki cha kwenda kumtafuta makamu mwenyekiti kilikuwa zuga tu, lengo lilikuwa ni kumteua rasmi Samia kuwa mgombea wa Urais.

Hii maana yake nini, maana yake Samia kapita bila kufuata mchakato wa kawaida wa chama wa kuchukua fomu kutafuta wadhamini kutoka mikoa mbalimbali nchini. Na Hussein Mwinyi naye kakwepa mchakato wa kumtafuta Mgombea Urais huko Zanzibar. Ule Msemo wa Rais wa Zanzibar anatokea DODOMA Tanganyika umedhihirika leo.

Hiki alichokifanya Samia na kaka yake Hussein Mwinyi ni Kutafuta mteremko wa kisiasa na Unajenga Precedence moja mbaya sana. Sasa hivi wana CCM wajue tu kuwa in the future, hakuna Rais atakayetokana na chama hicho atakayejali hatua za vikao kadha wa kadha, yeye atakuwa anacheza na mkutano mkuu tu , mkutano ukishasema ndiyoooooo, hakuna cha mkutano wa halmashauri kuu wala kamati kuu utakaokuwa na sauti juu ya maamuzi mbalimbali mazito.

Staili hii hii Samia anaweza kuitumia kuilazimisha CCM iridhie ubadilishaji wa katiba kuondoa muhula wa vipindi vya uongozi au kuongeza muda.

Kwa kweli hii staili ya Mbereko, ya kupitisha watu bila kupingwa, ya kutafuta mbereko kwa kukwepa ushindani wa kisiasa ndani ya chama, CCM imeulea yenyewe na sasa madhara yanawarudia wao. Hakuna tena kufuata due process ya kupata wagombea, ni kuwashtukiza wajumbe tu walioshiba ubwabwa, na kulipiwa guest house za kufikia ili watoe sauti za ndiyooooo.

Hii ni disaster.
Leo Samia amekoleza safari ya CCM kujifia, kimegeuka chama cha maigizo, hakuna brainy aspects ya kila move chama hiki kinafanya kwa sasa. Kimegeuka kama chama cha sherehe ya wachoma nyama kula mapande ya minofu ya nchi bila kujali mustakbali wa vizazi vijavyo.

Yetu macho, lakini kwa sasa hakuna chama hapo ni genge la watafuna nchi huku likiwarushia wajumbe makombo ya posho kipindi cha vikao kama hivi vilivyotawaliwa na upambe, uchawa, mob psychology na group thinking.

Nakubaliaba na wewe. 2030, Atamuachia Hussein kwa mtindo huo huo.
 
Missile of the Nation hoja yako sidhani kama wengi wali iangalia kwa uzito wake. Ni kweli kuna tatizo

1. Mkutano mkuu ulikuwa na agenda ya kuteua Makamu wa Rais Bara.

2. Kulikuwa na hoja ya kuchapisha Fomu 1 ya Urais unaombwa na kuteuliwa na ndivyo ilivyokuwa kawaida

3. Hoja imeletwa kwa kushtukiza katika Mkutano mkuu. Kwa kawaida hoja huanzia vikao vya Kamati kuu, Halmashauri kuu na kuidhinishwa na Mkutano mkuu.

M/kiti Samia anatoa maagizo sekretariati iandae azimio baada ya hoja ya Mkutano mkuu! hapa ni kinyume na taratibu kwasababu Mkutano mkuu huwa ni kauli ya mwisho.

4. Mkutano mkuu umenyima Wanachama walionuia haki yao ya kugombea nafasi ya Urais

5. Consulatation imefanyika ndani ya kikao, kwa maana Kamati kuu na H/Kuu hawana taarifa

Kuna fukuto na tatizo kubwa sana, hii short cut inaashiria walichokifanya ni kukwepa tatizo

Nadhani wanataka kukwepa yale ya Lowassa! wakijua wakati huu kuna udhaifu mkubwa sana.

Pascal Mayalla tusaidie kwasababu wewe ni mwandishi, mwanasheria , mwana CCM na ''Privy''

Mag3 JokaKuu
 
Mkuu Nguruvi3 , japo niko Dodoma kuhudhuria mkutano, but naomba ku reserve my comments at the moment to grasp what real happened!.
Ila msimamo wangu kuhusu mgombea wa CCM 2025 bado ni ule ule wa kwenye HII kitu
mpaka siku ya uteuzi rasmi wa wagombea wa CCM.
P
 
Missile of the Nation hoja yako sidhani kama wengi wali iangalia kwa uzito wake. Ni kweli kuna tatizo

1. Mkutano mkuu ulikuwa na agenda ya kuteua Makamu wa Rais Bara.

2. Kulikuwa na hoja ya kuchapisha Fomu 1 ya Urais unaombwa na kuteuliwa na ndivyo ilivyokuwa kawaida

3. Hoja imeletwa kwa kushtukiza katika Mkutano mkuu. Kwa kawaida hoja huanzia vikao vya Kamati kuu, Halmashauri kuu na kuidhinishwa na Mkutano mkuu.

M/kiti Samia anatoa maagizo sekretariati iandae azimio baada ya hoja ya Mkutano mkuu! hapa ni kinyume na taratibu kwasababu Mkutano mkuu huwa ni kauli ya mwisho.

4. Mkutano mkuu umenyima Wanachama walionuia haki yao ya kugombea nafasi ya Urais

5. Consulatation imefanyika ndani ya kikao, kwa maana Kamati kuu na H/Kuu hawana taarifa

Kuna fukuto na tatizo kubwa sana, hii short cut inaashiria walichokifanya ni kukwepa tatizo

Nadhani wanataka kukwepa yale ya Lowassa! wakijua wakati huu kuna udhaifu mkubwa sana.

Pascal Mayalla tusaidie kwasababu wewe ni mwandishi, mwanasheria , mwana CCM na ''Privy''

Mag3 JokaKuu

..nadhani imetoka hiyo.

..kwa Ccm, Mwenyekiti ambaye muda wake haujaisha, ni alfa na omega.
 
Hili linaeleza zaidi, kwamba, kama wanaweza ''kufanya uhuni' wa namna hii, wanashindwaje chaguzi dhidi ya Wapinzani? Just imagine, waliofikiria kuchukua Fomu wamechinjiliwa mbali.

Wajumbe wa Mkutano mkuu ni kama kondoo, hawajui kwanini wapo Dodoma.
Kuna Wasomi, Maprofesa, Dr n.k. hakuna hata mmoja mwenye kuhoji, hii short cut imeandikwa wapi

Eti wanategemea busara za wazee, wakati inaonekana ilipangwa na Wazee wawe rubber stamp

Kama wanategemea busara, katiba ya CCM ina mapungufu! hakuna anayehoji.

Imesikitisha, Watu 1900 hakuna mwenye akili ya kuhoji halafu ndio walinzi wa rasilimali zetu.
Hivi hawa wanawezaje kuunda serikali itakayohoji 'tycoons'' wanaokuja kupora rasilimali zetu.

Kuna kitu kinaendelea kichini chini 'just a matter of time'
 
Leo huko DODOMA wametangaza rasmi wagombea wa CCM wa nafasi ya rais wa JMT na rais wa Zanzibar.

Kama mnavyojua kwenye siasa hakuna kitu cha bahati mbaya, ni dhahiri huo mpango wa kumpitisha Samia na Hussein Mwinyi kuwa wagombea kwa Kuwashtukiza wanachama ulisukwa mapema. Kwa hiyo hata kikao hiki cha kwenda kumtafuta makamu mwenyekiti kilikuwa zuga tu, lengo lilikuwa ni kumteua rasmi Samia kuwa mgombea wa Urais.

Hii maana yake nini, maana yake Samia kapita bila kufuata mchakato wa kawaida wa chama wa kuchukua fomu kutafuta wadhamini kutoka mikoa mbalimbali nchini. Na Hussein Mwinyi naye kakwepa mchakato wa kumtafuta Mgombea Urais huko Zanzibar. Ule Msemo wa Rais wa Zanzibar anatokea DODOMA Tanganyika umedhihirika leo.

Hiki alichokifanya Samia na kaka yake Hussein Mwinyi ni Kutafuta mteremko wa kisiasa na Unajenga Precedence moja mbaya sana. Sasa hivi wana CCM wajue tu kuwa in the future, hakuna Rais atakayetokana na chama hicho atakayejali hatua za vikao kadha wa kadha, yeye atakuwa anacheza na mkutano mkuu tu , mkutano ukishasema ndiyoooooo, hakuna cha mkutano wa halmashauri kuu wala kamati kuu utakaokuwa na sauti juu ya maamuzi mbalimbali mazito.

Staili hii hii Samia anaweza kuitumia kuilazimisha CCM iridhie ubadilishaji wa katiba kuondoa muhula wa vipindi vya uongozi au kuongeza muda.

Kwa kweli hii staili ya Mbereko, ya kupitisha watu bila kupingwa, ya kutafuta mbereko kwa kukwepa ushindani wa kisiasa ndani ya chama, CCM imeulea yenyewe na sasa madhara yanawarudia wao. Hakuna tena kufuata due process ya kupata wagombea, ni kuwashtukiza wajumbe tu walioshiba ubwabwa, na kulipiwa guest house za kufikia ili watoe sauti za ndiyooooo.

Hii ni disaster.
Leo Samia amekoleza safari ya CCM kujifia, kimegeuka chama cha maigizo, hakuna brainy aspects ya kila move chama hiki kinafanya kwa sasa. Kimegeuka kama chama cha sherehe ya wachoma nyama kula mapande ya minofu ya nchi bila kujali mustakbali wa vizazi vijavyo.

Yetu macho, lakini kwa sasa hakuna chama hapo ni genge la watafuna nchi huku likiwarushia wajumbe makombo ya posho kipindi cha vikao kama hivi vilivyotawaliwa na upambe, uchawa, mob psychology na group thinking.
Kumbe wakati mwingine huwa unaona mambo vizuri? Asante sana kwa maono hayo ambayo wengine tusingeweza kuyaandika bila kupokea matusi.
 
Chama kimepoteza mwelekeo. Chombo kinayumbayumba. Naodha wa chombo na wasaidizi wake wa.epotea njia. Abiria tafuteni maboya ya kujiokoa na dhoruba.
 
Hili linaeleza zaidi, kwamba, kama wanaweza ''kufanya uhuni' wa namna hii, wanashindwaje chaguzi dhidi ya Wapinzani? Just imagine, waliofikiria kuchukua Fomu wamechinjiliwa mbali.

Wajumbe wa Mkutano mkuu ni kama kondoo, hawajui kwanini wapo Dodoma.
Kuna Wasomi, Maprofesa, Dr n.k. hakuna hata mmoja mwenye kuhoji, hii short cut imeandikwa wapi

Eti wanategemea busara za wazee, wakati inaonekana ilipangwa na Wazee wawe rubber stamp

Kama wanategemea busara, katiba ya CCM ina mapungufu! hakuna anayehoji.

Imesikitisha, Watu 1900 hakuna mwenye akili ya kuhoji halafu ndio walinzi wa rasilimali zetu.
Hivi hawa wanawezaje kuunda serikali itakayohoji 'tycoons'' wanaokuja kupora rasilimali zetu.

Kuna kitu kinaendelea kichini chini 'just a matter of time'

..hata wangefuata utaratibu Samia angeshinda.

..nadhani mambo yamekuwa complicated na suala Dr.Mpango kuamua kung'atuka.
 
Hoja si kushinda, hilo likuwa wazi. Hoja ni njia iliyotumika ''short cut'' ya kushtukiza Wajumbe
Hata utaratibu walioandika wao wenyewe kwenye katiba yao hawakuufuata! hapa ndipo inaonyesha kuna kitu kilikuwa kinakwepwa au kuogopwa. Nadhani kuna ''internal strife''

Kuhusu Dr Mpango nadhani kuna mambo hakubaliani nayo ! it's obvious
 
Sababu ya uongo hiyo, hakuna wa kushindana na raisi aliye madarakani. Hizo zingine ni hofu tu
Kwa Katiba iliyopo Rais ndio kila kitu Chamani na Nchini hakuna wa kumtingisha hata waliokuwa na nia ya URais wanajua hilo !
Kinachowasukuma huwa ni tamaa tu na kutaka kubahatisha !
 
Back
Top Bottom