Samia atajwa na Forbes kama moja ya wanawake wenye nguvu zaidi duniani kwenye mwaka 2024

Samia atajwa na Forbes kama moja ya wanawake wenye nguvu zaidi duniani kwenye mwaka 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametajwa kwenye orodha ya wanawake wenye nguvu zaidi duniani.

Samia ambaye alitajwa pia mwaka 2023 amewekwa kwenye nafasi ya 91 katika list hiyo ambayo pia ilihusisha viongozi na wanawake mbalimbali maarufu duniani

Forbes.png

======================================

Baada ya kuona listi hii nimepata maswali yafuatayo:

  • Forbes wanajua kinachoendelea Tanzania lakini?
  • Hizi list unaingia by merit au unalipia?
  • Kuna Mtanzania yeyote amehusika kuandaa list hizi?
  • Mwaka jana Samia alikuwa namba 93 mwaka huu kapanda mpaka 91, nini kimempandisha?
  • Samia anajua kama amewekwa kwenye hizi list?
 
Wakuu,

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametajwa kwenye orodha ya wanawake wenye nguvu zaidi duniani.

Samia ambaye alitajwa pia mwaka 2023 amewekwa kwenye nafasi ya 91 katika list hiyo ambayo pia ilihusisha viongozi na wanawake mbalimbali maarufu duniani

======================================

Baada ya kuona listi hii nimepata maswali yafuatayo:

  • Forbes wanajua kinachoendelea Tanzania lakini?
  • Hizi list unaingia by merit au unalipia?
  • Kuna Mtanzania yeyote amehusika kuandaa list hizi?
  • Mwaka jana Samia alikuwa namba 93 mwaka huu kapanda mpaka 91, nini kimempandisha?
  • Samia anajua kama amewekwa kwenye hizi list?
Mbona mnabishana kwani amjui kuwa HATA UPUMBAVU PIA NI NGUVU
..NGUVU ZA UPUMBAVI ...NAUZA NCHI KWA KUPEWA MAJI YA ZAMZAM
 
It's time to really change - to overhaul - when the enemy seems to be praising you.
 
Nguvu ipo utekaji, kuwawa, na kupigwa Lisas kwel nguvu ipo 😀😀😀
 
TAHARIFA HII SIO KWELI,!!!!!!
TAHARKIFA YA KWELI NI KUWA

Kwa sasa Rais Samia Suluhu Hassan ndie Rais mwenye nguvu kuliko Rais yeyote Duniani.
Nafafanua jinsi ilivyo ni kuwa tarehe furani, mwezi furani, saa furani alfajiri ya mwaka furani Rais Samia alipokea wokovu katika eneo la pale Magogoni karibu na Getini.( nimeandika kwa password)
Ishara ya kudhibitisha kuwa kweli alipokea wokovu ni kwa maneno ya kinywa chake ( imeandikwa kwa maneno ya kinywa chako utaukumiwa na kwa maneno ya kinywa chako utahesabiwa haki)
1. Dhamila itoke ndani ya Moyo. Biblia imeandika wanaoongozwa na Roho hawapo chini ya sheria.
2. Kila mtu ale urefu wa kamba yake Biblia imendika asiyefanya kazi na hasile.
3. Don't judge a book by its cover Biblia imendika Kesho ya Mtu hakuna ajuaye.
4. Alisema katiba si kitabu tu mbona vile vitabu vitakatifu hamuvieshimu? Maana yake kwa sasa Taifa la Tanzania lipo chini ya katiba ya dunia hii ( vitabu vitakatifu) kuliko wakati wowote uliowai kutokea.
5. Body language yake akiwa anaongea unaona kabisa moyo wake ni mweupe ( She is Ethical)
6. Kuna cheo furani katika utawa wa Taifa letu kimefutwa tayari tumeingia kwenye utawala wa kifalme.
7. Kwa sasa kinachoendele kwenye taifa la Tanzania nikimaanisha Siasa, watu kutekana, watu Kuuwawa, watu kuchinjana, na vyote unavyovijua wewe unayesoma hapa avitokani na SERIKALI, CCM, CHADEMA, POLISI, au na mtu yeyote hapana ni kwa sababu ya kilichotokea baada ya Mheshimiwa Rais kupokea wokovu. Tunachatakiwa kuelewa ni kuwa sisi wote watanzania tunatembelea kwenye Nafsi ya mtu mmoja ambaye ni Rais wetu nikimaanisha yeye anapokuwa hana furaha na sisi wote kama Taifa tunakuwa hamna furaha and the opposite is true
Sasa nini limetokea baada Rais Samia kupokea wokovu ni kwamba kwa Sasa Taifa la Tanzania system yote ya utawala/uendeshaji imebadilika yaani password za uendeshaji wa Taifa zimebadilika na kumbuka Rais wa nchi ndiye Mtumishi wa KWANZA wa Mungu ndio maana imeandikwa mtawala akisikiliza uongo hata watumishi wake huwa waovu.
Haya mabandiliko ya utawala sio yanafanyika kwa wakati mmoja hapana ni process inaendelea siku kwa siku.....
Maana ya haya yote ni nani?
1. Taifa la Tanzania limekuwa ndio Taifa la kwanza Duniani kuingia kwenye wokovu. ( Tupo kwenye utawala wa haki nikimaanisha kwa sasa kila kinachofanyika kimawekwa wazi uwezi ficha)
2. Tunaelekea kuupata utajili halisi wa nchi hii na kila taifa litapiga salute. ('Nwanzo 1:1-4')
3. Tanzania itaanza kuexport Labour yaani mataifa watakuwa wanakuja kuchukua walau Mtanzania mmoja akafanyike baraka kwenye sekita za makampuni nk

Mambo yanayoenda kutokea ni mengi including mabaya pia maana kuna watu watakao taka kusaidi kusudi la Mungu wataondoka kama ilivyotokea wakati wa wana wa Israel kutoka Misri kuelekea nchi ya Kanan

Biblia Kitabu Cha
Amosi 3:7 inasema:
Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.

Maana yake Mungu uwajulisha watu wake kwenye taifa kwa yajayo hii watu wafuate maelekezo kupunguza taaruki
Haya niliyondika ni kweli na hakuna wa kubatilisha maana yamekwisha kamilika ROHONI na sasa tunaendelea mkutimia mwilini kila tunaposonga mbele
Imeandikwa mambo haya hayawezekani kwa mwili bali kwa Roho
Ndugu zangu watanzania Mungu wa Mbinguni anawapenda sana mlipewa upendeleo wa juu sana na uwezi amini watanzania ndio binadamu wenye akili sana kuliko mwanadamu yeyote duniani.

Kunatakiwa kufuata maelekezo ni mengi hili kuepusha sintofaamu.

MBARIKIWE SAANA
 
Uzuri ni kwamba mwaka 2090 mimi na huyo sijui Samia tutakua tumekufa wote.
 
Vigezo walivyotumia FORBES 👇

"Fedha, vyombo vya habari, athari, na nyanja za ushawishi" ni dhana zinazohusiana zinazoelezea jinsi nguvu na ushawishi vinavyofanya kazi katika jamii. Wacha tuangalie kila kipengele na uhusiano wake:

• Fedha: Hii inawakilisha rasilimali za kifedha, mtaji, na utajiri. Ni kichocheo kikuu cha ushawishi kwa sababu inaruhusu watu binafsi na mashirika kupata rasilimali, kufadhili kampeni, kushawishi sera, na kudhibiti maelezo. Kadiri mtu anavyokuwa na pesa nyingi, ndivyo uwezekano wa ushawishi wake unavyoongezeka.

• Vyombo vya Habari: Hii inajumuisha aina zote za mawasiliano, ikiwa ni pamoja na magazeti, matangazo ya redio na televisheni, vyombo vya habari vya kidijitali, na mitandao ya kijamii. Vyombo vya habari vinaumba maoni ya umma, kuweka ajenda, na kuunda maelezo. Kudhibiti vyombo vya habari, au uwezo wa kuvitumia kwa ufanisi, hutoa nguvu kubwa ya kuathiri mtazamo wa umma na tabia. Mara nyingi fedha hucheza jukumu muhimu katika kudhibiti au kuathiri vyombo vya habari.

• Athari: Hii inarejelea matokeo au athari za matendo na maamuzi. Athari inaweza kuwa kijamii, kisiasa, kiuchumi, au mazingira. Fedha na vyombo vya habari vinaathiri sana athari za vitendo mbalimbali, iwe chanya au hasi. Kwa mfano, mtu tajiri anaweza kutumia vyombo vya habari kukuza jambo fulani, na kusababisha athari kubwa ya kijamii.

• Nyanja za Ushawishi: Hizi ni maeneo au sehemu ambapo mtu binafsi au shirika hutoa nguvu na ushawishi. Nyanja hizi zinaweza kuwa za mitaa, kitaifa, au kimataifa, na zinaweza kujumuisha sekta mbalimbali kama siasa, biashara, elimu, au utamaduni. Fedha na vyombo vya habari ni zana muhimu za kupanua na kudumisha nyanja za ushawishi.


Uhusiano:

Uhusiano kati ya vipengele hivi vinne ni wa mzunguko na unaojirudia. Fedha inaweza kununua upatikanaji wa vyombo vya habari na udhibiti, ambao kisha huongeza athari na kupanua nyanja za ushawishi. Ushawishi huu ulioongezeka unaweza kuzalisha pesa zaidi, na kuendeleza mzunguko huo. Kwa mfano:

• Shirika tajiri linaweza kutumia pesa zake kufadhili kampeni za matangazo (vyombo vya habari) ili kukuza bidhaa zake, kuathiri tabia ya watumiaji na kupanua sehemu yake ya soko (nyanja ya ushawishi).

• Chama cha siasa kinaweza kutumia michango (fedha) kununua muda wa matangazo ya kampeni (vyombo vya habari), kuathiri wapiga kura na kushinda uchaguzi (athari), hivyo kuongeza nguvu na nyanja yake ya ushawishi.

Kuelewa mwingiliano kati ya fedha, vyombo vya habari, athari, na nyanja za ushawishi ni muhimu kwa uchambuzi wa nguvu katika jamii na kuelewa jinsi maamuzi yanavyofanywa na jinsi mabadiliko ya kijamii yanavyotokea. Inaangazia umuhimu wa ufahamu wa vyombo vya habari, uwazi wa kifedha, na mawazo muhimu katika urambazaji wa ulimwengu unaoundwa na nguvu hizi zinazohusiana.
 
Back
Top Bottom