Samia kila anachokifanya kinayeyuka kama barafu, jamii imemkataa

Nyinyi vijana wadogo badilikeni, anzeni kutazama nchi kwa kuzitazama fursa, mnakuwa na akili za uchochezi kwa sababu mnashinda mkisoma habari za kichochezi habari za maasi.

SSH hana sababu yoyote ya msingi ya vijana wa mijini kumkataa, haipo. Mengi sana anayafanya ambayo yanagusa uhai wa hao hao vijana wa instagram.

Hakuna anayetegemea mitutu, nidhamu ilihitaji kurudishwa baada ya vijana kudanganywa kwamba yale ya Madagascar na Sri Lanka yanaweza kutokea TZ. Wakasahau tulishawahi kumtoa madarakani Obote na yule dikteta wa Comoro isingeshindikana kushughulikia uasi wa humu humu nchini.
 
Samuya anakubalika na kagenge kadogo ka wanufaika na machawa machoko kama wewe...% kubwa ground HAKUBALIKI!.
 
Yaan hadi Samia amalize miaka 5 vijana wengi watakua matahira
 
Hotuba ya sekunde chache ya Gamondi ilileta ushawishi chanya nchini kuliko kauli za dharau za SSH.
 
Hao unaodhani ni wengi ndio wachache. Wale wazee wa no reform sio wengi kulinganisha na wote wanaofahamu kipi haswa SSH anakifanya akiwa ikulu.
Uovu wa SSH umeleta hisia za visasi kwenye familia nyingi za WaTanganyika hasa hasa za hao wafia-ccm wanaofahamu kipi anakifanya Ikulu.
Time 💣 Tick-tock!
 
Alipata kura ngapia kwenye kituo chako na jimbo lako ulipopigia kura?
 
Sasa kwa nini hawakutoka kumpigia kura?
 
Mkuu, umenikumbusha Swala la Kigoma.

Imekuwaje barabara mbovu kiasi kile inajengwa katikati ya mji na viongozi mko kimya, huoni kama ile ni aibu.

Tembelea TZ huwezi kuta Barabara ya aina ile popote.
 
Uovu wa SSH umeleta hisia za visasi kwenye familia nyingi za WaTanganyika hasa hasa za hao wafia-ccm wanaofahamu kipi anakifanya Ikulu.
Time 💣 Tick-tock!
Laumu uchochezi, chuki na udini. Laumu fitina inayosambazwa na kina Mange na Maria ambayo imetufikisha hapa.

Tanzania ina utajiri wa kila aina cha ajabu huwezi kumkuta mtu akipoteza hata dakika tano katika kufikiria anavyoweza kufaidika na utajiri atakachofanya ni kuendelea kuandika negativity peke yake.

Labda tunalo tatizo la elimu, labda hatuna ubunifu vichwani mwetu. Hatuna jema kabisa mtu kuanzia Jumatatu asubuhi mpaka Jumapili usiku anatengeneza nishati hasi kila sekunde!.

Uwanja wa ndege wa Mwanza kujengwa kwake ni kulifanya eneo lile la kanda ya ziwa liwe kituo cha kibiashara (hub) mikoa yote ya kanda ile ifaidike na uwepo wake wafanyabiashara wafaidike na uwepo wake lakini cha ajabu wenyeji akili zao zinamezwa na mambo hasi peke yake!.

Hii fukwe kutoka Tanga mpaka Mtwara ina urefu wa kilomita 1420 hiyo fursa tupu ya kimaendeleo. Badala ya watu kukesha tunaongea hasi tu akili zetu ziwazie namna zipi tunaweza kufaidika na uwepo wa bandari ya Dar ya Tanga na inayokuja ya Bagamoyo.

Ukiikuza sana fitina kuna siku utailipia hiyo dhambi. Madhara ya dhambi hiyo humgusa kila mtu japokuwa inaingia kwenye jamii kupitia mtu mmoja tu.

Mungu atusaidie mwaka 2026 uwe wa mabadiliko ya kimitazamo miongoni mwetu
 
wewe sema umemkataa wewe
 
Sasa kwa nini hawakutoka kumpigia kura?
Wamempigia kura kwa wingi. Sisi huku bara wengi wetu tunafahamu kitu gani anakifanya. Mange na Maria wameshindwa kuitisha maandamano, kila wakijaribu watu wanaishia kuwakejeli tu kwa maoni ya dhihaka.

Maana yake wanaunga mkono kinachofanywa na SSH hawapendi tena kuona vifo vya watu wasio na hatia kwa kivuli cha maandamano feki. Raia wameweza kuonyesha kwa dhati kwamba kuna nguvu kubwa inatumika katika kujaribu kujenga chuki dhidi ya SSH haswa humu mitandaoni.

Tunaposema kuna uasi kutokea nje ya Tanzania tunamaanisha ile nguvu iliyopo nyuma ya chuki dhidi ya SSH na serikali yake.

Bila ya msaada haramu kutoka kwa majirani maandamano ya tarehe 9 Desemba yalifeli halafu wakenya wakaandamana kule kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Kenya, kuliwahusu nini kushindwa kufanyika kwa maandamano ya siku ile huku Tanzania wakati wao wapo nchi nyingine?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…