Samia kukosekana kwenye list ya Forbes 2025 ni madhara ya matukio ya Oktoba 29?

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Forbes wametoa tena orodha ya wanawake wenye nguvu zaidi duniani ambayo ya mwaka wa jana (2024) Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa nafasi ya 91. Lakini cha kushangaza mwaka huu amekosekana kwenye orodha hiyo huku wakionekana Wanawake wengine Wakiafrica zaidi ya nane, kama vile Rais mpya wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah na Waziri Mkuu wa DRC Judith Suminwa.

Screenshot_19-12-2025_03811_www.forbes.com.jpeg

Hii inakuja wakati wa kuna kelele za kimataifa kuhusu uchaguzi uliofanyika Oktoba 2025, uliogubikwa na madai ya udanganyifu, ukandamizaji wa haki za binadamu na kikatili unadhaniwa kusababisha maelfu kufa. Bado kumekuwa na lawama nyingi kutoka Umoja wa Afrika, kulingana na ripoti kutoka Journal of Democracy na Index on Censorship.

Licha ya kuwepo kwa maoni yanatofautiana kwenye majukwaa ya kimataifa huku, Wengine wakimtaja kama "mtawala dhalimu" kwa ukandamizaji upinzani na uhuru wa kujieleza, kuna ambao wanamtetea kama mzalendo, huku orodha hii ikilenga wanawake 8 wa Afrika wanaosukuma ushawishi wa kiuchumi badala ya misukosuko ya kisiasa.

Wakuu, mnadhani matukio ya kabla, wakati na baada ya uchaguzi ndiyo yaliyosababisha asionekane kwenye orodha hii?
 
Tumeshakubaliana BAN kwa wote waliotufikisha hapa! Nawaombeni tulizingatie sana hili..
 
Akikosekana mwaka huu atapata mwaka kesho.

Naona kama Mo ibrahim kwa Africa ndio ya maana zaidi kisiasa.

Mtoto wa Dos Santos yule bilionea alikuwa ananunua hizo tuzo kuna Pr company zinakufanyia mafekeche unaingia hizo tuzo. Wana document na kuhighlight your outstanding achievements na kuzituma forbes.

Sasa hapa atafanya nani Kabudi au msigwa
 
Forbes wametoa tena orodha ya wanawake wenye nguvu zaidi duniani ambayo ya mwaka wa jana (2024) Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa nafasi ya 91. Lakini cha kushangaza mwaka huu amekosekana kwenye orodha hiyo huku wakionekana Wanawake wengine Wakiafrica zaidi ya nane, kama vile Rais mpya wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah na Waziri Mkuu wa DRC Judith Suminwa.

View attachment 3517364

Hii inakuja wakati wa kuna kelele za kimataifa kuhusu uchaguzi uliofanyika Oktoba 2025, uliogubikwa na madai ya udanganyifu, ukandamizaji wa haki za binadamu na kikatili unadhaniwa kusababisha maelfu kufa. Bado kumekuwa na lawama nyingi kutoka Umoja wa Afrika, kulingana na ripoti kutoka Journal of Democracy na Index on Censorship.

Licha ya kuwepo kwa maoni yanatofautiana kwenye majukwaa ya kimataifa huku, Wengine wakimtaja kama "mtawala dhalimu" kwa ukandamizaji upinzani na uhuru wa kujieleza, kuna ambao wanamtetea kama mzalendo, huku orodha hii ikilenga wanawake 8 wa Afrika wanaosukuma ushawishi wa kiuchumi badala ya misukosuko ya kisiasa.

Wakuu, mnadhani matukio ya kabla, wakati na baada ya uchaguzi ndiyo yaliyosababisha asionekane kwenye orodha hii?
Unachorea jibu mstari?
Halafu hao Forbes ni nani?- Who are They?
 
Subiri siku wakitoa orodha ya wanawake wauaji na madikteta wakubwa Ulimwengu, huyu wa kwenu atashika nafasi ya juu kabisa, huku wengine wakifuatia kwa points za mbali sana.
 
Back
Top Bottom