Forbes wametoa tena
orodha ya wanawake wenye nguvu zaidi duniani ambayo ya mwaka wa jana (2024) Rais
Samia Suluhu Hassan alikuwa nafasi ya 91. Lakini cha kushangaza mwaka huu amekosekana kwenye orodha hiyo huku wakionekana Wanawake wengine Wakiafrica zaidi ya nane, kama vile
Rais mpya wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah na
Waziri Mkuu wa DRC Judith Suminwa.
View attachment 3517364
Hii inakuja wakati wa kuna kelele za kimataifa kuhusu
uchaguzi uliofanyika Oktoba 2025, uliogubikwa na madai ya udanganyifu, ukandamizaji wa haki za binadamu na kikatili unadhaniwa kusababisha maelfu kufa. Bado kumekuwa na lawama nyingi kutoka Umoja wa Afrika, kulingana na ripoti kutoka Journal of Democracy na Index on Censorship.
Licha ya kuwepo kwa maoni yanatofautiana kwenye majukwaa ya kimataifa huku, Wengine wakimtaja kama "
mtawala dhalimu" kwa ukandamizaji upinzani na uhuru wa kujieleza, kuna ambao wanamtetea kama mzalendo, huku orodha hii ikilenga wanawake 8 wa Afrika wanaosukuma ushawishi wa kiuchumi badala ya misukosuko ya kisiasa.
Wakuu, mnadhani
matukio ya kabla, wakati na baada ya uchaguzi ndiyo yaliyosababisha asionekane kwenye orodha hii?