Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa, Komredi Debora Joseph Tluway Tarehe 28/12/2024 alikutana na madereva bajaji walioko Wilaya ya Mpanda ili kutekeleza dhima ya Program ya "SAMIA MTAANI KWETU" yenye lengo la kukutana na makundi yote ndani ya jamii yetu kwaajili ya kujenga Umoja, Mshikamano na Uwajibikaji rafiki ili kufikisha fursa kwa makundi haya.
Komredi Debora Joseph Tluway amesema kukutana na madereva Bajaji kumesaidia kuwajengea uwezo ili kuleta ufanisi katika shughuli zao za kila siku ili waweze kutimiza Malengo yao na Malengo ya Taifa kupitia Malengo yao lakini pia kujikwamua Kiuchumi kupitia Mikopo ya Asilimia Kumi (10%)
Aidha, yamefanyika mashindano ya kumjua Dereva Bajaji bora wa Mwezi ambaye alichaguliwa na madereva wenzake na hatimaye kujishindia Tanki zima la Mafuta (Full Tank) na Mshindi wa pili amejishindia Nusu Tenki la Mafuta, Jambo ambalo limejenga hamasa miongoni mwa Madereva wa kuongeza umakini wa kazi zao.
"Samia Mtaani Kwetu imelenga kufikia makundi yote ndani ya Mkoa wa Katavi (Mpanda) hususan Madereva Bajaji na baadaye itagusa Madereva Bodaboda, MamaNtilie, Vijana Machinga, Wafugaji na Wakulima"
"Kwanini SAMIA MTAANI KWETU? Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya miradi mingi ya maendeleo ikiwemo Sekta ya Afya, Elimu, Miundombinu na Maji. Vitu vyote hivi vimefanyika mtaani kwetu na sisi ni mashuhuda wa haya maendeleo" - Komredi Debora Joseph Tluway
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-12-29 at 09.44.13.jpeg154.7 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-12-29 at 09.24.32.jpeg202.8 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-12-29 at 09.24.08.jpeg453.8 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-12-29 at 09.24.04.jpeg332.4 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-12-29 at 09.24.12.jpeg475.7 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2024-12-29 at 09.24.19 (1).jpeg377 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-12-29 at 09.24.22.jpeg240.9 KB · Views: 4