Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

Kwani kuna ubaya gani kumshukuru Mungu kwa kumchukua mja wake JPM?
Hakuna ubaya wowote, tena tumefunzwa kushukuru kwa yote
JPM ni Marehemu tu kama Mkapa na Nyerere, tutayaeleza yake mazuri na yale mabaya bila kupepesa
Kiafrika marehemu hasemwi vibaya, ila kama ni kuyasema makosa as lessons yasirudiwe sawa lakini sio kwa masimango
Amen.
P.
 
Naunga mkono hoja, Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania
P
 
Kwa vile leo ni birthday ya Rais Samia, nawaomba wana jf wote ambao ni well wishers, tuungane kumu wish Happy Birthday this lovely lady Rais wetu mpendwa, Rais wetu mpenzi, Rais wetu kipenzi, Rais Dr. Samia Suluhu Hassan, Chifu wa kabila kubwa kuliko makabila yote Tanzania, ambayo Kanda ya kabila hilo ndio Kanda determinant ya kura za urais wa JMT, Chifu Hangaya.
Happy Birthday.

P
 
NI makara ndefu, lakini nikuulize wewe kama mwandishi wa long. Uonavyo unastahili kuchambua mafanikio na mapungufu kwa kutumia Mungu? Yaani sisi wa-TZ tuamini tuko hapo kwa sababu ya Mungu? Tukiendelea na mtindo wa kushindwa kutofautisha kazi za viongozi wa dini, wanasiasa, waandishi habari, n.k tumekwisha!

Wewe ni mwandishi, chambua kiandishi. Hizo salamu za Mungu wapo wahusika. Tukisikia mwanasiasa naye anatanguliza Mungu na kunukuu misahafu, ni dalili za kufilisika kisiasa.
 
Angalia live Sunday service Arise and shine, Rais amepeleka sadaka ya shukrani kwa Mwamposa kupitia Chalamila.

Mama ni lazima abarikiwe.
Samia ni Baraka kwa Tanzania, ila lazima asaidiwe ili aweze zaidi na zaidi!.
P
 
Paskali! Paskali! acha kujidhalilisha rafiki yangu. Pumzika kidogo upate akili mpya!
 
Ndugu Paskali, Paskali....mkuu naheshimu maoni yako lakini aina yako ya uandishi uwa inaniacha na maswali mengi. Je, wewe ni mwandishi huru au kuna kitu unakitafuta? Kabla ya yote nikuulize,..ni Rais yupi kati ya 5 waliopita kuliongoza taifa letu haukuwa mpango wa Mungu?

Tulimsikia mara kadhaa jpm akidai maendeleo hayana chama, lakini matendo yake yalikuwa tofauti. Rais Samia na zile 4Rs zake, tumeona kilichotokea kwa akina Dr. Slaa, Mwambukusi, Mdude .....na kama haitoshi ni majuzi tu vyombo vya habari vimelalamikiwa kuingiliwa na mkono wa serikali ya Samia kwenye kuripoti baadhi ya taarifa hasa zinazohusiana na sakata la bandari. Bado tumesikia huko kanda ya ziwa, upinzani ukilalamika baadhi ya mikutano yake kuhujumiwa na Serikali kwenye mwanvuli wa chama.

Umezungumzia pia ujenzi wa miundo mbinu, ni sawa, lakini ni Rais yupi hakufanya hivyo kwa kiasi chake? Watanzania tumekuwa watu wa ajabu sana, tunasifia kupita kiasi mtu akiwa madarakani lakini akimaliza muda wake ukosoaji unakuwa mkubwa. Kasumba hii haisaidii kumuonyesha mhusika mapungufu ili ayafanyie kazi. Nilimsikia mh. Kinana juzijuzi tu akiwafokea mawaziri wavivu na kulikemea Bunge liache tabia ya kupitisha kila kitu kinacholetwa na serikali hata kama ni hovyo. Pamoja na kwamba inaweza kuwa imepangwa aseme hivyo katika michezo yao ya kisiasa lakini alisema jambo halisi lililopo.

Ndugu yangu, baadhi ya vitu vinavyolalamikiwa ni pamoja na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Je, kasi ya kushughulikia jambo hili anayoifanya SSH wewe inakuridhisha? Rais Samia kama walivyowanasiasa wengine hapa Tanzania hasa wale wa chama changu CCM, akikwambia jambo jipe muda kwanza atimize ndiyo umpe sifa zake. Sifia, sifia na kutukana wapinzani ilikuwa kete ya kupata uteuzi kwa Rais aliyepita siyo sana kwa mama Samia. Rais Magufuli alikuwa akivunja katiba na Sheria za nchi kwa kuzuia shughuli za vyama vya siasa, na hiyo hatoi uhalali wa kumsifia yule anaelekea kufuata katiba inavyotaka. Ni wajibu wake kufanya hivyo.
 
Mpango wa Mungu usaidiwe tena!? au unataka kumuingiza Shetani katikati ya Mpango wa Mungu!!?

au una maana Allah ashirikishwe kumsaidia Mungu...
Kumsaidia Rais wetu ni jukumu lako, langu na mtanzania mwingine kumwambia ukweli mahala pabovu ili aparekebishe. Hii sifiasifia haimsaidii sana. Na inavyoelekea watu wanaomzunguka wanampotosha na hawampi taarifa sahihi, hivo ili kuziba hilo ombwe, tulioko nje ya mfumo wa serikali yake tumwambie ukweli.
 
Nisahihi kabisa ni nadra sana kukutana na kiongozi ambaye atapigiwa kelele kwa kiwango hili na akabakia na msimamo wake wengi wanayumba ili kujipendekeza ili wapate kura.

Amesimama kidete kama itaathiri kupigiwa kura haina shida muhimu kutekeleza Yale anayoamini yanamanufaa kwa wananchi wake hasa wanyonge.

Ipo siku itaeleweka kwamba wapiga filimbi walikuwa na ajenda nyuma ya tukio hili.

Nchi zote za Afrika zimepitia makosa kama hayo na kusababisha waingie kwenye migogoro isiyokwisha mfano waliompinga Mkwame Nkuruma,Keneth Kaunda nk mpaka Leo hawajazikombia nchi zao dhidi ya udhalimu wa kiuchumi.
 
Mheshimiwa mteue tu huyu Pascal Mayalla mpeleke huko mtwara, huku tutakuja kumvunjia heshima.
Mkuu Mamnde, Mamndenyi , hata kabla sijakujua kuwa wewe ni verified member, nilijikuta nimetokea kukuheshimu kwa michango yako, nakuheshimu sana, nakuomba uniheshimu!. Humu JF tuna wajinga wengi humu wanaodhani mimi natafuta shavu la uDC!. Naomba nisikuhesabu miongoni mwa wajinga hawa!.
Para ya 3 ya bandiko hili ni self explanatory, mimi sio chawa!.

Naomba kuanza bandiko hili kwa angalizo hili la tofauti kati ya pongezi za kujikomba kutafuta uteuzi, na pongezi za kweli bonafide genuine.
P
 
Japo utekelezaji wa hili jambo haujafanyika, lakini dalili zote kuwa linakwenda kutimizwa zipo hivyo tayari baraka mbalimbali zimeisha anza kumiminika Tanzania na kwa Watanzania individually mfano hai ni huu Watanzania Fadhili na Ibrahim kuwania Tsh. Bilioni 2.4 katika Fainali za America's Got Talent

Watanzania tutake advantage ya spirit ya ushindi kwenye kila jambo lako lolote utafanikiwa!. Isiwe ni shida yako ni pesa, hivyo una wish ukiamka ukute pesa chini ya mto!, sio hivyo, you must do something to get the money!.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…