Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

paschal tangu nimfahamu, sijawahi kuona ameandika kitu kinachoeleweka. nadhani anahitaji msaada.
Mkuu chapwa24 , kwavile kichaa huanzaga hivi hivi, kichaa mwenyewe hajitambui kuwa ni kichaa ila wanaomuona ndio wanamjua ni kichaa!. Makala hizi pia zinachapishwa gazetini na soon kipindi cha TV kitaruka hewani, haiwezekani wote hao pia wawe ni vichaa!.

Kwenye uandishi wangu kuna uandishi unaitwa abstract, mpaka uwe na kiwango fulani cha uelewa ndipo utaelewa!, hivyo usikute ni wewe ndio hujafikia kiwango cha kunielewa, pole!.
P
 
I acknowledge you are my brother, kitu pekee nilichowahi kuappreciate kwako ni kipindi cha "kitimoto" miaka ileee, ila vingine vyote seriously huwa sikuelewi, I am glad unaleta kipindi hicho, pengine kitakuwa kama kile. hivi hujiangalii na kujikumbuka mwenyewe ulivyokuwa? rudi kule paschal. achana na mambo ya uchawa hayo hayajakusaidia hadi leo.
 
 
Hiki ndicho nilichokisema na wewe unakirudia tena, kwa kiwango chako cha uelewa, rukhsa kuniona mimi ni chawa wa Mama na nayaheshimu mawazo yako.

Elimu haina mwisho, please take time kunisoma huku umetulia, Chawa wa Mama anaweza kupandisha bandiko kama hili
-https://www.jamiiforums.com/threads/watanzania-tuunge-mkono-2025-ni-zamu-ya-mwanamke-ila-sio-lazima-awe-yeye-bali-yule-aliyepangiwa-na-yeye-kama-ni-yeye-aliyepangiwa-then-ni-yeye.1913484/

P
 
Paskali una mapepo wachafu wengi sana. Katubu kwenye kaburi la Magufuli.
 
Mkuu.
Siku ulipoandika hii maneno ilikuwa Sawa.
Je na huu wakati tulio nao bado unaendelea kuyaenzi uliyoandika??
Uke utuambie kama unayoyaona, kuyasikia na yanayotendeka ni haki bin haki kwa Taifa la Tanzania yetu????
 
Tunapoelekea mwisho wa mwaka, huku tukielekea mwaka wa uchaguzi, nafanya tathmini ndogo ya expectations zangu na awamu hii ya Rais Samia, nili expect nini, nini kimefanyika, nini bado hakijafanyika, na nini kinaweza kufanyika kabla ya 2025 ili Watanzania tufanye Uchaguzi Mkuu huru na wa haki unaosimamiwa na Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi.

Katika bandiko hili, nikemquote Rais Samia with the following expectations

“Nimedhamiria, kwamba kwenye kuenzi miaka yetu ya demokrasia ya vyama vingi. Serikali yangu itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi.

Lengo, ni kwamba Tanzania yetu iende na wakati na kama ilivyokuwa wakati mwingine, tujue mapema ni wakati gani wa kufanya jambo, hata kama si watu wanaliunga au hawaliungi mkono kwa wakati husika.


Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza” Mwisho wa kunukuu.
Expectation number 1 mabadiliko ya mifumo ya siasa, lazima yaanze na katiba, ndipo kwenye sheria, kisha Tume huru ya uchaguzi. Hivyo hili bado!.
Expectation number 2 na number 3, imo on a pipeline mwezi February 2014.
Expectations ya katiba mpya kwa muda uliobakia kabla ya uchaguzi, the time is too little too late, hatuwezi kupata katiba mpya!, ila sasa tumuombe Rais Samia, hata kama muda uliobakia hauwezi kutupatia katiba mpya, muda huu unatosha kufanya mabadiliko madogo ya katiba, tukafanya uchaguzi Mkuu huru na wa haki.
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
 
To be honest huyu mama anafaa sana kwa nyakati hizi.
Ila kuna baadhi ya watendaji wake wanamuangusha WANAFIKI.
 
JK Mpango wa Mungu, Mwendakuzimu Jiwe Mpango wa Mungu, Bi Kizimkazi Mpango wa Mungu
Mungu gani huyu mnayemzungumzia Mwenye Mipango inayo fail Kila wakati
 
Hii ni MTR ya Bandiko hili
Rais Samia aendelee kuombewa
View attachment 2285981View attachment 2285982
Naomba kuanza bandiko hili kwa angalizo hili la tofauti kati ya pongezi za kujikomba kutafuta uteuzi, na pongezi za kweli bonafide genuine.
Pongezi hizi ni bona-fide genuine
JPM alikuwa mpango wa Mungu kwa Tanzania,
Tuendelee kumshukuru Mungu kwa Samia.
Samia ni Samia
Sasa mwaka wa mabandiko ni mwaka huu wa 2024!.
hili liendelee, tuendelee kumshauri lakini tusimpangie!.
Tuendelee kumshauri
Tunaendelee kushukuru na kusema asante, kilio chetu cha sheria mbovu na kandamizi kimesikika, sheria zinakwenda kubadilishwa, tuendelee kumshukuru huyu mwenye hili sikio sikivu.
Chance ya kufanya interview na Rais Samia, bado haijapatikana, tuendelee kuvuta subra.
Vipindi vipo, ukipatikana muda muafaka, nitavirusha.
Licha ya miswada ya mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, ubatili huo bado upo!. Kiukweli hili linanitatiza sana, kwasababu mimi licha ya kuwa ni mwandishi tuu wa habari, na mtangazaji wa kujitegemea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, kitu kikiisha kuwa batili kisheria, kinaitwa "null and void above initio" yaani ni sawa na hakipo!. Sheria iliyokuwepo ni sheria batili!, unairekebisha hiyo sheria, lakini ule ubatili bado unaendelea kuwepo kwasababu ubatili huo uko kwenye katiba!. Swali ni kwanini tusirekebishe kwanza katiba, tukauondoa huo ubatili, kisha ndio tukarekebisha sheria?.
Zifuatazo ni nukuu za Rais Samia
“Nimedhamiria, kwamba kwenye kuenzi miaka yetu ya demokrasia ya vyama vingi. Serikali yangu itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi.
Kwa vile mifumo ya kisiasa inaongozwa na katiba, ndipo zije sheria, mabadiliko yoyote ya kweli, yataanza na katiba, ndipo tuje kwenye sheria!.

Naendelea kusisitiza "Mabadiliko yoyote ya sheria zilizotokana na katiba, bila mabadiliko ya katiba, mabadiliko hayo ni superficial!"-Paskali.
Lengo, ni kwamba Tanzania yetu iende na wakati na kama ilivyokuwa wakati mwingine, tujue mapema ni wakati gani wa kufanya jambo, hata kama si watu wanaliunga au hawaliungi mkono kwa wakati husika.
Naunga mkono hoja
Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza” Mwisho wa kunukuu.
Hapa sasa ndipo kwenye mzizi wa fitna, Rais Samia amezungumzia "Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yatakayo leta ushindani wa haki"
hapa anamaanisha sheria hiyo, ita rekebisha ule uwanja tenge wa ushindani wa kisiasa and creates a level playIng field,
"na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza” Mwisho wa kunukuu.
Hapa anazungumzia haki ya kila Mtanzania kuchagua kama ilivyotolewa na Ibara ya 6 ya katiba ya JMT, lakini hazungumzii haki ya kila Mtanzania kuchaguliwa kwa mujibu wa Ibara ya 21, haki hii imeporwa kwa kuwekewa kifungu batili cha kudhaminiwa na chama cha siasa!.

Hapa ni sawa na kama wale watu wanaotembea na kuwafuata kuja kama wanao hubiri amani usoni huku wameyaficha mapanga mgongoni, wakiisha wakaribia huku na nyinyi mnawakimbilia kuwakumbatia kuwa amani imefika, wanapowafikia, ndipo wanachomoa mapanga na kuwa fyekelea mbali!.

Kwa vile bado tuna fursa za kuijadili miswada hii, let's hope for the best kuwa ubatili huu ndani ya Katiba yetu na ndani ya sheria yetu ya uchaguzi utaondolewa!.
Japo hii ni ahadi tuu, lakini hili ni jambo jema kwasababu tumelipigia sana kelele.
Hii sasa sio ahadi tena, utekelezaji umeanza, na hapa lazima tumpe a very big up sana Rais Samia.
Asante Mungu kwa Rais Samia,
Mungu Mbariki Rais Samia aweze kuyakamilisha kupitia YEYE.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
 

Hii ni zawadi yangu kwa Birthday ya Mama leo, nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
 
Nyie wanasheria ndio mlituambia na kutuwekea vizimba vya kupiga kura kwa siri, sasa inakuwaje mwanasheria wewe unatoa siri ya kura yako ya 2025? You will never ever be another Lakha.
 
"Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza” - Samia Suluhu Hassan Mwisho wa kunukuu.
Wanabodi, hii ni nukuu ya Rais Samia katika andiko lake la miaka 30 ya Vyama Vingi. Asabuhi hii, naomba nifanye revisiting ya bandiko hili la Julai 2, 2022.

Maneno hayo ni maneno makubwa sana kwasababu yanahusu "kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao".

Kiongozi yoyote anapoandika ama anapohutubia, kuna mambo mawili, kwenye andiko lake ama hotuba yake.
1. Kati ya andiko la Kiongozi kuna vitu ni maono, mawazo, maneno na maandishi ya Kiongozi yeye mwenyewe kutoka moyoni mwake, kichwani mwake, mawazoni mwake, yaani ni yeye mwenyewe halisi.
2. Viongozi wana wasaidizi ambao huwa wanawaandikia talking notes, na kwa rais wa nchi, ana wasaidizi hotuba ambao wanamuandalia nini cha kusema kwa kumuandikia, kisha Rais kwanza anapitia kile alichoandikiwa lakini sio chake, anaweza kuongeza chake au kupunguza, na ndipo anakuja kuhutubia au kutoa andiko.

Wakati akihutubia, sisi tunaosikiliza, tukisikia kila Rais anachosema kwenye hotuba yake, tunahesabu kila kilichosemwa ni rais kusema.

Wakati Rais akihutubia, kila anachosema ni Rais kusema, huwezi kujua kipi ni cha kwake na kipi ni ameandikiwa tuu lakini sii cha kwake.

Hii pia hutokea kwa wasomaji wa habari kwenye TV zote na redio zote, watazamaji na wasikilizaji, wanamuona mtangazaji, wanamsikiliza mtangazaji, wao wanajua hizo habari wametangaziwa na mtangazaji fulani, wao wanajua ni mtangazaji huyo ndie anajua habari hizo, kumbe hawajui kazi ya mtangazaji wa habari ni kutangaza tuu habari alizoandikiwa na wengine, yeye kazi yake ni kusoma tuu!.

Vivyo hivyo kwenye hotuba za Viongozi, kuna Viongozi wanasoma tuu hotuba walizoandikiwa na wengine lakini sio mawazo yao, sio maneno yao, ila ni matamshi yao!.

Kama nolivyosema kwenye habari, mtangazaji unaandikiwa ,kisha unapewa kuipitia habari hiyo , kwa RTD, taarifa ya habari ni dakika 10, mtangazaji unatakiwa kuipitia nusu saa kabla, ili uielewe na unaposoma, una soma kitu unachokijua.

kitendo cha kuichukua habari ambayo hujaiandika wewe, ukaipitia na kuisoma as if ni umeiandika wewe, kinaitwa "presence", ndio maana watangazaji huitwa presenters, kazi yao ni ku present tuu.

Kuna wakati msomaji wa habari unapitia habari usiyoielewa, unapaswa uulize, ili usisome kitu usichokielewa, ili ukisoma ile presence iwepo. Lakini katika mitikasi hii na ile, kuna siku unakuwa umechelewa kupitia news kabla, hivyo unasoma tuu kwa uzoefu, hata ukikutana na kitu usichokielewa, unakisoma tuu hivyo hivyo, na wasikilizaji na watazamaji watasikia tuu nabkuelewa, lakini kwa watu sensitive na kitu kinachoitwa graphology, utamnote mtangazaji ana fanya stammering, then unajua huyu hajapitia, hivyo anasoma kitu asichokijua, anasema kitu alichoandikiwa lakini hakijui.

Vivyo hivyo hutokea kwenye hotuba za Viongozi anaandikiwa kitu asichokijua, anapitia hotuba, kisha anahutubia kitu asichokijua, hii inaitwa "paying lip services".

Maneno hayo ya Rais Samia kwenye andiko lake ni maneno makubwa, mazito Bonafide Genuine, kwenye bandiko hili, nikasema "Rais Samia atabarikiwa sana kama atatekeleza hili"

Sasa sheria mpya ya uchaguzi imeishatungwa, its very unfortunately sheria hiyo mpya bado ina ubatili ule ule tunaoupigia kelele, hali inayonifanya kuanza kujiuliza, hivi maneno haya "Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza”
Jee ni maneno ya Rais Samia mwenyewe au aliandikiwa?!. Jee hii sheria mpya ya uchaguzi, yenye ubatili ule ule, italeta vipi ushindani wa haki wakati Rais Samia ameahidi, "kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza”
wakati sheria mpya ya uchaguzi, watu bado hawana haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka, bali Watanzania tunalazimishwa kuwachagua viongozi waliopitishwa na vyama vya siasa na sio viongozi wanaowataka!.

Tafsiri ya alichokisema Rais Samia, na kilicholetwa kwenye sheria mpya ya uchaguzi ni sawa na kusema, jee kuna uwezekano Rais Samia na yeye is just paying 💋 services kwenye baadhi ya kauli zake ama ahadi zake?.

Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…