Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na Makala zangu elimishi za "Kwa Maslahi ya Taifa", Makala ya leo ni jinsi Rais Samia alivyo ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Rais Samia, Akifanikiwa kwenye hili, atabarikiwa sana na taifa la Tanzania, litabarikiwa!
Natoa wito kwa wote wenye mapenzi mema na nia njema na taifa letu la Tanzania, sote katika umoja wetu, tupaze sauti zetu juu na kumshukuru Mungu kwa kutuletea Samia, "Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, ili atimize mapenzi yako"!
Mungu Ibariki Tanzania"!
View attachment 2285981View attachment 2285982
Naomba kuanza bandiko hili kwa angalizo hili la tofauti kati ya pongezi za kujikomba kutafuta uteuzi, na pongezi za kweli bonafide genuine.
Sasa twende kwenye mada ya leo.
Kila jambo hutokea kwa sababu, hata likiwa jambo baya, kunaweza kutokea jambo mbaya kumbe lina wema ndani yake, mfano wa Yesu kwa Wakristu, alikuja ili kuukomboa ulimwengu, Yesu aliteswa hadi kufa kifo cha aibu kwa kuwambwa msalabani! hiki ni kifo kibaya kuliko vifo vyote, ila ni kwa kupigwa kwake na kwa kuteswa kwake sisi tuliponywa, ukombozi ulipitia mateso na kifo cha msalabani ile dhambi ilikufa, ila aliyashinda mauti kwa ufufuko na kutuachia uzima wa milele kwa waaminio japo miili hii ya kidunia itakufa, lakini mwili wa kiroho haufi na tukapata uzima wa milele!
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa JPM, alikuwa ni chaguo la Mungu kwa Tanzania, baada ya Tanzania ya JK, Tanzania aliyoipokea JPM, mahali ilipofikia, ilimhitaji mtu wa JPM type kuinyoosha kwanza,
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania ilihitaji Dikiteta, tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba! ndipo aje mtu kama Samia, kuipaisha, aliyoyafanya yale aliyoweza kuyafanya, ikiwemo kuchonga mabarabara mengi katika mambo mengi hadi kuitwa Tingatinga, baada ya kuukamilisha mpango wa Mungu kwa Tanzania kupitia JPM, Mungu akamuita kwake kwa namna ambayo ilituachia majonzi, lakini ndio mpango wa Mungu yeye kuondoka kwa namna hiyo, na hatuwezi kuhoji kwasababu kazi ya Mungu haiina makosa.
Kama JPM alikuwa ni mpango wa Mungu kwa Tanzania, na baada ya Mungu kumuita JPM kwake na kumpangia majukumu mengine kule, ujio wa Samia pia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania, mpaka hapa tulipofika, Rais Samia, ameisha onyesha kwa kauli na matendo, kuwa na yeye ni mpango wa Mungu kwa Tanzania, Watanzania wote wapenda mema na ustawi wa taifa hili, sote tuseme Asante Mungu kwa Samia.
Hatusemi asante Mungu kutuondolea JPM na kutuletea Samia, tunasema asante Mungu kwa JPM na asante Mungu kwa Samia, kila zama na zama zake, kwa vile JPM alikuwa binaadamu na sio malaika, yale mambo ya kibinaadamu yasiyotupendeza enzi za JPM, tuyaache, tusiendee kuyasema sema ni kama kumsimanga marehemu, tumuache JPM apumzike kwa amani, na kwa mazuri ambayo Samia sasa anayafanya, tumpongeze Samia kwa mazuri yake bila kumlinganisha na mtangulizi wake.
Samia alipoingia tulishauri
Mwaka 2021 ulikuwa ni Mwaka wa Majanga kwa Tanzania. Mwaka 2022 uwe Mwaka wa Mabadiliko, Watanzania tubadilike! Happy New Year!
Enzi za JPM, kuna baadhi yetu tulikuwa hatukohoi, na JPM alisema wazi “mimi sipangiwi” na hatukumpangia, Samia mara tuu baada ya kuingia, ameruhusu watu sasa tunakoa, kwa vile JPM hatukumpangia, nashauri hata kwa Samia, kama ni kukohoa tukoe lakini na yeye tusimpangie!
Pamajo na hoja hii kuwa tusimpangie rais wetu Samia, kufanya jambo lolote, lakini kukiwa na jambo lolote ambalo sio jema sio zuri sio la kupendeza, tulisema kwa nia ya kulionyeshea, na tutoe ushauri wa nini cha kufanya, huo ushauri wa kupendekeza nini cha kufanya, sio kumpangia ni kumshauri tu.
Kwa muda mrefu baadhi yetu tumekuwa tukilalamikia baadhi ya sheria ambazo zinawakosesha haki Watanzania na baadhi ya sheria hizo zinahusiana na uendeshaji wa siasa za vyama vingi nchini Tanzania. Ukilalamikia jambo fulani, ukaliangazia, wenye mamlaka wakalisikia, wakatoa kauli kuwa jambo hilo litashughulikiwa. Kitu cha kwanza ni kwa wewe uliolalamika kusema asante, kilio chako kimesikika, na kitu cha pili ni kumshukuru huyo aliyesikia kilio chako na kuahidi kushughulikia hilo jambo lako.
Baadhi ya hoja zangu kulalamikia sheria na kutaka watu tutendewe haki ni hizi
kwa wanaopenda Rejea. Kwa wasiopenda rejea you can just jump
Wiki hii Tanzania imeadhimisha miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi nchini, vyama vingi vilipoanza tena nchini Tanzania ile 1992, umenikuta mimi tayari nina mwaka mmoja kazini, nimeanza kazi Januari 2, mwaka 1990, hivyo mfumo wa vyama vingi umenikuta kazini, mpaka leo tunatimiza miaka 30 ya vyama vingi nchini, mimi niko Newsroom, na kati ya marais 6 wa Tanzania, nimapata bahati ya kufanya mahojiano ya ana kwa ana na marais 4, maombi ya kufanya mahojiano na Samia yako njiani.
Katika hii miaka yangu 30 ya mfumo wa vyama vingi, nimefanya vipindi vingi, nimehoji watu wengi, akiwemo Mama Samia nimefanya nae mahojiano ya saa moja mara mbili, mara ya kwanza akiwa Waziri Ofisi ya Makamo wa Rais na Mara ya pili akiwa Makamo Mwenyekiti Bunge Maalum la Katiba, kuna siku nitarushia vipindi vya mahojiano hayo, hivyo kuna wengi ndio watamjua kumbe Samia na demokrasia, hakuanza leo!.
Miongoni mwa makubwa ambayo nimekuwa nikilalamikia ni sheria yetu ya uchaguzi, na makala zangu mbili zilizotangulia kabla ya leo, nikaeleza jinsi sheria hizo batili na kinyume cha katiba, zilivyokuja kuhalalishwa kwa kuchomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu hivyo kuinajisi katiba!.
Juzi katika waraka wake wa Miaka 30 ya Vyama Vingi nchini Tanzania, huku kwenye mtandao wa jamii unaoongoza nchini Tanzania, Jamii Forums, kuna makala inayosaamba inayodaiwa kuandikwa na mwandishi kwa jina la “
Ameandika Rais Samia Suluhu Hassan: Miaka 30 ya Vyama Vingi - Changamoto na Mustakabali Kusonga Mbele”
Sina uhakika kama ni kweli ameandika Samia, kwasababu nimetembelea Mtandao wa :Mawasiliano Ikulu, sikuiona makala hii, ila ingekuwa ni fake, taarifa ingeishatoka kuwa hii ni fake, ila hata bila ya udhibitosho mwandishi ni Samia, maadam imesema jambo jema naomba kuinukuu.
“Nimedhamiria, kwamba kwenye kuenzi miaka yetu ya demokrasia ya vyama vingi. Serikali yangu itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi.
Lengo, ni kwamba Tanzania yetu iende na wakati na kama ilivyokuwa wakati mwingine, tujue mapema ni wakati gani wa kufanya jambo, hata kama si watu wanaliunga au hawaliungi mkono kwa wakati husika.
Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza” Mwisho wa kunukuu.
Japo hii ni ahadi tuu, lakini hili ni jambo jema kwasababu tumelipigia sana kelele.
Haki huinua taifa, kwa ahadi kama hizi, Rais Samia anazidi kuthibitisha yeye ni Chagua la Mungu kwa Tanzania, na akitekeleza haya, Rais Samia, atabarikiwa na Taifa la Tanzania litabarikiwa sana!. Asante Mungu kwa Rais Samia,
Mungu Mbariki Rais Samia ayaweze kupitia YEYE.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali