Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na Makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", Makala ya leo ni jinsi Rais Samia alivyo ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Rais Samia, Akifanikiwa kwenye hili, atabarikiwa sana na !, Taifa la Tanzania, litabarikiwa!. Natoa wito kwa wote wenye nia njema kwa taifa letu, sote tupaze sauti zetu katika umoja wetu kwa kumshukuru Mungu kutuletea Rais Samia, "Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania"!.

Naomba kuanza bandiko hili kwa angalizo hili

Sasa twende kwenye mada ya leo.

Kila jambo hutokea kwa sababu, hata likiwa jambo baya, kunaweza kutokea jambo mbaya kumbe lina wema ndani yake, mfano wa Yesu kwa Wakristu, alikuja ili kuukomboa ulimwengu, Yesu aliteswa hadi kufa msalabani, hili jambo jema, ila ni kwa kupigwa kwake na kwa kuteswa kwake sisi tuliponywa, ukombozi ulipitia mateso na kifo cha msalabani ile dhambi ilikufa, ila aliyashinda mauti kwa ufufuko na kutuachia uzima wa milele kwa waaminio japo miili hii ya kidunia itakufa, lakini mwili wa kiroho haufi na tukapata uzima wa milele.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa JPM, alikuwa ni chaguo la Mungu kwa Tanzania, baada ya Tanzania ya JK, Tanzania aliyoipokea JPM, mahali ilipofikia, ilimhitaji mtu wa JPM type kuinyoosha kwanza, Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania ilihitaji Dikiteta, tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba! ndipo aje mtu kama Samia, kuipaisha, aliyoyafanya yale aliyoweza kuyafanya, ikiwemo kuchonga mabarabara mengi katika mambo mengi hadi kuitwa Tingatinga, baada ya kuukamilisha mpango wa Mungu kwa Tanzania kupitia JPM, Mungu akamuita kwake kwa namna ambayo ilituachia majonzi, lakini ndio mpango wa Mungu yeye kuondoka kwa namna hiyo, na hatuwezi kuhoji kwasababu kazi ya Mungu haiina makosa.

Kama JPM alikuwa ni mpango wa Mungu kwa Tanzania, na baada ya Mungu kumuita JPM kwake na kumpangia majukumu mengine kule, ujio wa Samia pia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania, mpaka hapa tulipofika, Rais Samia, ameisha onyesha kwa kauli na matendo, kuwa nay eye ni mpango wa Mungu kwa Tanzania, Watanzania wote wapenda mema na ustawi wa taifa hili, sote tuseme Asante Mungu kwa Samia.

Hatusemi asante Mungu kutuondolea JPM na kutuletea Samia, tunasema asante Mungu kwa JPM na asante Mungu kwa Samia, kila zama na zama zake, kwa vile JPM alikuwa binaadamu na sio malaika, yale mambo ya kibinaadamu yasiyotupendeza enzi za JPM, tuyaache, tusiendee kuyasema sema ni kama kumsimanga marehemu, tumuache JPM apumzike kwa amani, na kwa mazuri ambayo Samia sasa anayafanya, tumpongeze Samia kwa mazuri yake bila kumlinganisha na mtangulizi wake.
Samia alipoingia tulishauri Mwaka 2021 ulikuwa ni Mwaka wa Majanga kwa Tanzania. Mwaka 2022 uwe Mwaka wa Mabadiliko, Watanzania tubadilike! Happy New Year!

Enzi za JPM, kuna baadhi yetu tulikuwa hatukohoi, na JPM alisema wazi “mimi sipangiwi” na hatukumpangia, Samia mara tuu baada ya kuingia, ameruhusu watu sasa tunakoa, kwa vile JPM hatukumpangia, nashauri hata kwa Samia, kama ni kukohoa tukoe lakini nay eye tusimpangie.

Pamajo na hoja hii kuwa tusimpangie rais wetu Samia, kufanya jambo lolote, lakini kukiwa na jambo lolote ambalo sio jema sio zuri sio la kupendeza, tulisema kwa nia ya kulionyeshea, na tutoe ushauri wa nini cha kufanya, huo ushauri wa kupendekeza nini cha kufanya, sio kumpangia ni kumshauri tuu.

Kwa muda mrefu baadhi yetu tumekuwa tukilalamikia baadhi ya sheria ambazo zinawakosesha haki Watanzania na baadhi ya sheria hizo zinahusiana na uendeshaji wa siasa za vyama vingi nchini Tanzania. Ukilalamikia jambo fulani, ukaliangazia, wenye mamlaka wakalisikia, wakatua kauli kuwa jambo hilo litashughulikiwa. Kitu cha kwanza ni kwa wewe uliolalamika kusema asante, kilio chako kimesikika, na kitu cha pili ni kumshukuru huyo aliyesikia kilio chako na kuahidi kushughulikia hilo jambo lako.
Baadhi ya hoja zangu kulalamikia sheria na kutaka watu tutendewe haki ni hizi
kwa wanaopenda Rejea. Kwa wasiopenda rejea you can just jump

Wiki hii Tanzania imeadhimisha miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi nchini, vyama vingi vilipoanza tena nchini Tanzania ile 1992, umenikuta mimi tayari nina mwaka mmoja kazini, nimeanza kazi Januari 2, mwaka 1990, hivyo mfumo wa vyama vingi umenikuta kazini, mpaka leo tunatimiza miaka 30 ya vyama vingi nchini, mimi niko Newsroom, na kati ya marais 6 wa Tanzania, nimapata bahati ya kufanya mahojiano ya ana kwa ana na marais 4, maombi ya kufanya mahojiano na Samia yako njiani.

Katika hii miaka yangu 30 ya mfumo wa vyama vingi, nimefanya vipindi vingi, nimehoji watu wengi, akiwemo Mama Samia nimefanya nae mahojiano ya saa moja mara mbili, mara ya kwanza akiwa Waziri Ofisi ya Makamo wa Rais na Mara ya pili akiwa Makamo Mwenyekiti Bunge Maalum la Katiba, kuna siku nitarushia vipindi vya mahojiano hayo, hivyo kuna wengi ndio watamjua kumbe Samia na demokrasia, hakuanza leo.

Miongoni mwa makubwa ambayo nimekuwa nikilalamia ni sheria yetu ya uchaguzi, na makala zangu mbili zilizotangulia kabla ya leo, nikaeleza jinsi sheria hizo batili na kinyume cha katiba, zilivyokuja kuhalalishwa kwa kuchomekewa ndani ya katiba yetu.

Juzi katika waraka wake wa Miaka 30 ya Vyama Vingi nchini Tanzania, huku kwenye mtandao wa jamii unaoongoza nchini Tanzania, Jamii Forums, kuna makala inayosaamba inayodaiwa kuandikwa na mwandishi kwa jina la “Ameandika Rais Samia Suluhu Hassan: Miaka 30 ya Vyama Vingi - Changamoto na Mustakabali Kusonga Mbele”

Sina uhakika kama ni kweli ameandika Samia, kwasababu nimetembelea Mtandao wa :Mawasiliano Ikulu, sikuiona makala hii, ila ingekuwa ni fake, taarifa ingeishatoka kuwa hii ni fake, ila hata bila ya udhibitosho mwandishi ni Samia, maadam imesema jambo jema naomba kuinukuu.

“Nimedhamiria, kwamba kwenye kuenzi miaka yetu ya demokrasia ya vyama vingi. Serikali yangu itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi.

Lengo, ni kwamba Tanzania yetu iende na wakati na kama ilivyokuwa wakati mwingine, tujue mapema ni wakati gani wa kufanya jambo, hata kama si watu wanaliunga au hawaliungi mkono kwa wakati husika.

Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza” Mwisho wa kunukuu.

Japo hii ni ahadi tuu, lakini hili ni jambo jema kwasababu tumelipigia sana kelele.

Haki huinua taifa, kwa ahadi kama hizi, Rais Samia anazidi kuthibitisha yeye ni Chagua la Mungu kwa Tanzania, na akitekeleza haya, Rais Samia, atabarikiwa na Taifa Litabarikiwa. Asante Mungu kwa Rais Samia,

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Kaka Paskali, Hata JPM mpo/wapo waliosema ni mpango wa Mungu..!!
 
Unatumia mda mwingi kuandika uharo tu
Mkuu mpwayungu village, mtu kutoa huo ulioutaja sio kwa kupenda ni kuugua, ukila kitu sicho tumbo likachafuka lazima utahar.sha hivyo ni ugonjwa. Kama ilivyo kwa tumbo, akili pia ikichafuka, utawaza hivyo, utasema hivyo na kuandika hivyo. Asante kwa hili na nimekutwangia like yako.
P
 
Uteuzi hupati
 
Hata JPM mlisema nimpango wa Mungu mnasimana kwenye nini sasa?
 
Paskal unajichanganya sana uandishi wako.Hauko specific ku focus kwenye kile ulichokusudia una hama hama sana mpaka unampoteza msomaji kunasa kile umekusudia akipate..

Inawezekana ni mtind wa uandishi lakin this is real not productive.Uandishi huu unamchosha msomaji..Hit the points direct.
 
Kaka Paskali, Hata JPM mpo/wapo waliosema ni mpango wa Mungu..!!
Mkuu Ngali, Ngalikihinja, sio tupo au wapo waliosema JPM ulikuwa ni mpango wa Mungu, it's as if tulisema tuu, no it was indeed JPM alikuwa ni mpango wa Mungu kwa Tanzania for a specific project, project ilipokamilika, mwendo akaumaliza na kuitwa kwake.
Angalia akina sisi tulisema nini na lini kuhusu JPM, Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
Hivi ndivyo mipango ya Mungu inavyokuwa.
Sasa Samia ndio mpango mzima.

Kaka Paskali, if your references ni projects alizozianzisha na kuzifanikisha, kumbuka kuna zilizofail pia..!! Hiyo haiwezi kuwa reffered kwamba hakuwa mpango wa Mungu?
 
Mungu yupo ila shetani pia yupo, kuna watu kibao wa Mungu wamefanya mambo ya kishetani, Nabii Nuhu, baada ya mkewe kugeuka jiwe la chumvi wakati akitoroka Sodoma na Gomora, aliwalala mabinti wake mapacha akawabikiri na kuwatundika mimba wote wawili!. Hivyo kama kupotea Kwa Ben Saanane, Azory Gwanda na zile pyu pyu za Lissu he has a hand, then hiyo sio mipango ya Mungu ni mipango ya shetani.
P
 
Vitu vinavyosumbua watu wengi sio sijui tume sijui.katiba mpya viko vitu direct mfano vikwazo kwa kupata Passport kwa watafuta fursa nje misharti waliyoweka ni ya kuomba visa ya ubalozini ambayo haiwahusu

Pili Tanzania kuruhusu watanzania kupokea pesa kupitia PayPal kwa mauzo ya online

Ukweli vyama vya siasa hasa upinzani havibebi agenda za wananchi zinakomalia agenda za viongozi
Jitahidi kuonyesha busara hata kama una mahaba makubwa na watawala. Ni ujinga wa wazi kuvibebesha vyama vya upinzani uozo unaosababishwa na CCM na serikali yake.

Serikali ndiyo inayominya haki za wananchi. 2019 na 2020 ilivuka mpaka hadi kuwanyang’anya haki ya kuchagua wawakilishi wao katika serikali za mitaa na bungeni. Waliviengua vyama vya upinzani kwenye mihimili ya maamuzi na kuhakikisha ukiritimba wa CCM.

Halafu unadiriki kulia vyama vya upinzani havibebi ajenda za wananchi? Kupigania katiba na tume huru ya uchaguzi ni ajenda za viongozi? wa nchi gani? Wapinzani wakiongelea utendaji mbovu wa serikali na kutoa mapendekezo - nje ya bunge na Halmashauri wanashambuliwa na kuitwa wanaharakati. CCM yenyewe inajikanyagakanyaga tu. Leo, kinyume na msimamo wa 2015 inakubali kuwa katiba mpya ni hitaji la wananchi!
 
Hahahah
Mkuu Mwizukulu mgikuru, sio kila hoja ina upande. Hapa nimezungumza mambo 4 na hayana upande!.
1. Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania.
2. Kuna jambo amelisema, akilitekeleza Atabarikiwa na Tanzania Itabarikiwa
3. Kumshukuru Mungu kwa Samia
4. Kumuombea na kuliombea taifa.

Hapo kuna issue gani ya upande?.
Maandishi ni kama binadamu, wengine wakubwa, wengine wadogo, wengine wanene, wengine wembamba, wengine warefu wengine wafupi, hivyo maandishi ni kama binadamu mengine makubwa, mengine madogo, mengine marefu, mengine mafupi, mengine magumu, mengine marahisi, ukiona, umesoma kitu halafu huelewi, ujue maandiko hayo sio saizi yako, yatakuwa yamekuzidi Kimo. Pole!.
P
 
🐒🐒🐒
16565816466093.jpg
 
Mungu yupo ila shetani pia yupo, kuna watu kibao wa Mungu wamefanya mambo ya kishetani, Nabii Nuhu, baada ya mkewe kugeuka jiwe la chumvi wakati akitoroka Sodoma na Gomora, aliwalala mabinti wake mapacha akawabikiri na kuwatundika mimba wote wawili!. Hivyo kama kupotea Kwa Ben Saanane, Azory Gwanda na zile pyu pyu za Lissu, hiyo sio mipango ya Mungu ni ya shetani.
P
Then partly alikuwa mpango wa Mungu (due to projects alizopatia) and partly alikuwa mpango wa shetani maana kuna waliopotezwa na wengine kukutwa kwenye viroba as if mtu anajiuwa then akishakufa anaingia mwenyewe kwenye kiroba
 
Sina uhakika kama ni kweli ameandika Samia, kwasababu nimetembelea Mtandao wa :Mawasiliano Ikulu, sikuiona makala hii, ila ingekuwa ni fake, taarifa ingeishatoka kuwa hii ni fake, ila hata bila ya udhibitosho mwandishi ni Samia, maadam imesema jambo jema naomba kuinukuu.
Labda ameandika yeye ila wahuni wamei hack kabla haijafika mlango rasmi wa kutokea kwenda mtandao wa mawasiliano ikulu
 
Well said mkuu,kama hayotuzungumzwa ya huyu anaefanywa special marehemu hatuwez kujifunza
You can't have it both ways
Kwani kuna ubaya gani kumshukuru Mungu kwa kumchukua mja wake JPM?

JPM alimsema Nyerere kwa kusaidia ukombozi. Alimsema Nyerere kwa uhusiano na Israel na mengi tu

JF Mwalimu amejadiliwa miaka 23 tangu afariki , hatukusikia haya ya 'marehemu hasemwi'
Tunamkosoa Nyerere kwa sera zake , Ubinadamu na Utu wake unamlinda bila kuhitaji utetezi akiwa kaburini

JPM ni Marehemu tu kama Mkapa na Nyerere, tutayaeleza yake mazuri na yale mabaya bila kupepesa

Hizi habari za marehemu hasemwi ni kwa kutambua kuwa katika hazina zake kuna tatizo , tunataka afichiwe

No! watu waeleze kila kitu ili tujifunze tusijefanya makosa mengine yatakayotugharimu miongo mingi ijayo

Nashukuru ujio wa JPM. Urais wake umetuonyesha kile wenzetu wa mataifa hasa Afrika walichokilalamikia
Miaka ya 70,80 nchi za Afrika zilitumbukia katika machafuko na Mapinduzi kila uchao, Tanzania hatukujua ni kwanini

JPM alituonyesha kwa uwazi hisani za watangulizi wake na kutufunulia matundu ya katiba ya nchi
Alituonyesha jinsi mtu mmoja na kundi la vijana akina Sabaya na Bashite wanavyoweza kutesa nchi
JPM alitufunulia mengi sana tuliyokuwa hatuyajui hasa ubovu wa mifumo ya nchi ikiangukia mikono mibaya
JPM ametuachia nyufa za mbegu za udini na ukabili vitu tulivvyodhani Tanzania haikuumbwa navyo
JPM akatuonyesha kiongozi anavyoweza ku 'hypnotize ' Taifa

Bila yeye tungeyajuaje hayo? Bila yeye tungejifunzaje ?
 
Back
Top Bottom