Wanabodi, hii ni nukuu ya Rais Samia katika andiko lake la miaka 30 ya Vyama Vingi. Asabuhi hii, naomba nifanye revisiting ya bandiko hili la Julai 2, 2022.
Maneno hayo ni maneno makubwa sana kwasababu yanahusu "kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao".
Kiongozi yoyote anapoandika ama anapohutubia, kuna mambo mawili, kwenye andiko lake ama hotuba yake.
1. Kati ya andiko la Kiongozi kuna vitu ni maono, mawazo, maneno na maandishi ya Kiongozi yeye mwenyewe kutoka moyoni mwake, kichwani mwake, mawazoni mwake, yaani ni yeye mwenyewe halisi.
2. Viongozi wana wasaidizi ambao huwa wanawaandikia talking notes, na kwa rais wa nchi, ana wasaidizi hotuba ambao wanamuandalia nini cha kusema kwa kumuandikia, kisha Rais kwanza anapitia kile alichoandikiwa lakini sio chake, anaweza kuongeza chake au kupunguza, na ndipo anakuja kuhutubia au kutoa andiko.
Wakati akihutubia, sisi tunaosikiliza, tukisikia kila Rais anachosema kwenye hotuba yake, tunahesabu kila kilichosemwa ni rais kusema.
Wakati Rais akihutubia, kila anachosema ni Rais kusema, huwezi kujua kipi ni cha kwake na kipi ni ameandikiwa tuu lakini sii cha kwake.
Hii pia hutokea kwa wasomaji wa habari kwenye TV zote na redio zote, watazamaji na wasikilizaji, wanamuona mtangazaji, wanamsikiliza mtangazaji, wao wanajua hizo habari wametangaziwa na mtangazaji fulani, wao wanajua ni mtangazaji huyo ndie anajua habari hizo, kumbe hawajui kazi ya mtangazaji wa habari ni kutangaza tuu habari alizoandikiwa na wengine, yeye kazi yake ni kusoma tuu!.
Vivyo hivyo kwenye hotuba za Viongozi, kuna Viongozi wanasoma tuu hotuba walizoandikiwa na wengine lakini sio mawazo yao, sio maneno yao, ila ni matamshi yao!.
Kama nolivyosema kwenye habari, mtangazaji unaandikiwa ,kisha unapewa kuipitia habari hiyo , kwa RTD, taarifa ya habari ni dakika 10, mtangazaji unatakiwa kuipitia nusu saa kabla, ili uielewe na unaposoma, una soma kitu unachokijua.
kitendo cha kuichukua habari ambayo hujaiandika wewe, ukaipitia na kuisoma as if ni umeiandika wewe, kinaitwa "presence", ndio maana watangazaji huitwa presenters, kazi yao ni ku present tuu.
Kuna wakati msomaji wa habari unapitia habari usiyoielewa, unapaswa uulize, ili usisome kitu usichokielewa, ili ukisoma ile presence iwepo. Lakini katika mitikasi hii na ile, kuna siku unakuwa umechelewa kupitia news kabla, hivyo unasoma tuu kwa uzoefu, hata ukikutana na kitu usichokielewa, unakisoma tuu hivyo hivyo, na wasikilizaji na watazamaji watasikia tuu nabkuelewa, lakini kwa watu sensitive na kitu kinachoitwa graphology, utamnote mtangazaji ana fanya stammering, then unajua huyu hajapitia, hivyo anasoma kitu asichokijua, anasema kitu alichoandikiwa lakini hakijui.
Vivyo hivyo hutokea kwenye hotuba za Viongozi anaandikiwa kitu asichokijua, anapitia hotuba, kisha anahutubia kitu asichokijua, hii inaitwa "paying lip services".
Maneno hayo ya Rais Samia kwenye andiko lake ni maneno makubwa, mazito Bonafide Genuine, kwenye bandiko hili, nikasema "Rais Samia atabarikiwa sana kama atatekeleza hili"
Sasa sheria mpya ya uchaguzi imeishatungwa, its very unfortunately sheria hiyo mpya bado ina ubatili ule ule tunaoupigia kelele, hali inayonifanya kuanza kujiuliza, hivi maneno haya "Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza”
Jee ni maneno ya Rais Samia mwenyewe au aliandikiwa?!. Jee hii sheria mpya ya uchaguzi, yenye ubatili ule ule, italeta vipi ushindani wa haki wakati Rais Samia ameahidi, "kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza”
wakati sheria mpya ya uchaguzi, watu bado hawana haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka, bali Watanzania tunalazimishwa kuwachagua viongozi waliopitishwa na vyama vya siasa na sio viongozi wanaowataka!.
Tafsiri ya alichokisema Rais Samia, na kilicholetwa kwenye sheria mpya ya uchaguzi ni sawa na kusema, jee kuna uwezekano Rais Samia na yeye is just paying 💋 services kwenye baadhi ya kauli zake ama ahadi zake?.
Paskali