kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Ukiona Rais wa nchi anatetea wakati wote wafanyabiashara ujue ni mfanyabiashara.
Hivi katika nchi kama Tanzania unahitaji rais mfanyabiashara au mfanyakazi?
Hivi nchi ya uchumi kama wa tanzania unahitaji kuwatetea wafanyabiashara au kuweka sheria kuwadhibiti?
Juzi Rais kasema eti wafanyabiashara wameenda wizara ya afya kutaka kupewa kazi wanazungushwa. Sasa anataka wapewe tu dili hata kama hakuna kazi wanayotaka. Yani raha yake ni private sector wapate tu hela toka serikalini hata kama hakuna thamani yoyote wameipa serikali.
Rais mwenye atitude ya upigaji hela ya umma atatuangamiza. Sekta binafsi ya Tanzania imejaa ubabaishi tele na haina weledi wala uadilifu. Wamejitune kuibia serikali tu. Kwa nini sekta binafsi isikomae kufanya kazi kwenye sekta yenyewe?
Tunajua wenyewe wanajuana na wako makini kupeana kazi. Hawa wezi wanaopitia kwa wanasiasa ndio wanasumbua.
Rais lake kubwa iwe kutetea maslahi ya umma. Wakulima wavuvi wafanyakazi. Hawa ndio wanahitaji usaidizi wa serikali yetu. Sekta binafsi inajua kujilinda na kujitetea.
Pia mipango namna ya wao kutumika kufaidisha uchumi ipo sio rais kila siku kupigia chapuo wababaishaji kama ndio sekta binafsi.