Rais Samia ameyasema baada ya kupokea Ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Yaliyotokea Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025, tarehe 23 Aprili, 2026, Dar es Salaam.
"Ndugu wananchi, wakati nafuatilia uwasilishaji wa ripoti hii katika... nilisikia sentensi inayosema: 'Tunamtaka Samia wetu tunayemfahamu.' As if kwamba nilipoingia alikuwa Samia mwingine na sasa ni Samia mwingine. Nataka niwahakikishie Watanzania: mimi ni Samia yuleyule wa 4R.
Ni yuleyule wa 4R. Ninachoomba ni ushirikiano wenu katika kutekeleza hizo R nne. Wanasema kidole kimoja hakivunji chawa au 'it takes two to tango'. Kwa hiyo mkimtegemea Samia peke yake afanye, hayaendi. Lakini mkinipa ushirikiano mkubwa ndugu zangu, tutafika."
Katika miaka ya mwanzo ya uongozi wake, Rais Samia Suluhu Hassan alionekana kubadili upepo wa kisiasa kwa kuonesha utashi mpya uliogusa moja kwa moja masuala ya demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari na mwelekeo wa kidiplomasia. Kauli na hatua zake za awali zilijenga taswira ya kufungua milango iliyokuwa imeonekana kufungwa, huku wadau mbalimbali wa siasa, wanahabari na jumuiya ya kimataifa wakianza kuona Tanzania ikiingia katika awamu mpya ya demokrasia na ushirikiano.
Hata hivyo, kadri muda ulivyokwenda, hasa baada ya miaka mitatu ya mwanzo, mjadala unaibuka kuhusu...