Nini kimebadili mwelekeo wa uongozi wa Rais Samia ulioanza kwa 4R?

BungeLetu

Member
Joined
Feb 4, 2026
Posts
11
Reaction score
21
photo_2026-04-07_12-16-31.jpg
Katika miaka ya mwanzo ya uongozi wake, Rais Samia Suluhu Hassan alionekana kubadili upepo wa kisiasa kwa kuonesha utashi mpya uliogusa moja kwa moja masuala ya demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari na mwelekeo wa kidiplomasia. Kauli na hatua zake za awali zilijenga taswira ya kufungua milango iliyokuwa imeonekana kufungwa, huku wadau mbalimbali wa siasa, wanahabari na jumuiya ya kimataifa wakianza kuona Tanzania ikiingia katika awamu mpya ya demokrasia na ushirikiano.

Hata hivyo, kadri muda ulivyokwenda, hasa baada ya miaka mitatu ya mwanzo, mjadala unaibuka kuhusu iwapo mwelekeo huo umeendelea au umebadilika. Zipo dalili za kusuasua kwa utashi wa kisiasa, mabadiliko katika uhuru wa vyombo vya habari, pamoja na mitazamo mipya ya kidiplomasia ambayo inaonekana kutofautiana na matarajio ya awali.

Hali hii inaibua swali kubwa: ni nini hasa kimebadili mwelekeo wa Rais Samia kwenye maeneo haya matatu yanayogusa mustakabali wa demokrasia nchini?

Uhuru wa kisiasa
photo_2026-04-07_12-16-32.jpg

photo_2026-04-07_12-31-08 (2).jpg

photo_2026-04-07_12-31-08.jpg
Baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani, vyama vya siasa vilikuwa vimewekewa vikwazo katika kufanya shughuli za kisiasa. Shughuli za kisiasa, hasa kwa vyama visivyounda dola, zilikuwa zimeingia katika giza zito kutokana na zuio la mikutano ya hadhara.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kukabidhiwa kijiti cha uongozi kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Rais Samia alikuja na falsafa ya 4R (Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Ujenzi upya) ambayo ilitafsiriwa na wengi kama ufunguo wa siasa mpya nchini.

Hatua hiyo ilishuhudia shughuli za kisiasa zikianza kufanyika. Vyama vya upinzani vilianza kufanya mikutano na hata maandamano bila vikwazo vilivyozoeleka awali. Baadhi ya wakimbizi wa kisiasa pia walianza kurejea nchini.

Katika mazingira hayo, matarajio ya wadau wengi yalikuwa makubwa kuhusu mwelekeo mpya wa siasa. Rais Samia alipokea pongezi na hata tuzo kwa juhudi za kupunguza joto la kisiasa, huku fursa ya kukosoa na kukosoana ikionekana kurejea bila hofu.

Sasa mambo ni tofauti
Hata hivyo, katika kipindi cha takribani miaka miwili iliyopita, mwelekeo huo unaonekana kuyumba. Mfumo wa 4R unaonekana kupungua nguvu, huku baadhi ya vyama vya siasa na wanasiasa wakipitia misukosuko inayohusishwa na dola.

Kwa mfano, imeshuhudiwa Chama kikuu cha upinzani, CHADEMA, kikishindwa kushiriki uchaguzi kwa kusisitiza mabadiliko ya sheria za uchaguzi. Baadhi ya wadau wanaamini kuwa katika mazingira hayo, falsafa ya 4R ingeweza kutumika kuleta suluhu.
photo_2026-04-07_12-16-32 (2).jpg

photo_2026-04-07_12-31-08 (2).jpg
Aidha, matukio ya kukamatwa kwa wanasiasa wakosoaji wa Serikali yameanza kurejea. Mfano ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ambaye yuko gerezani akikabiliwa na kesi ya uhaini. Baadhi ya wadau wamependekeza maridhiano, huku Serikali ikisisitiza kuwa suala hilo liko mikononi mwa vyombo vya kisheria.

Matukio haya, pamoja na zuio la baadhi ya mikutano ya upinzani, sarakasi katika cahaguzi, yanajenga picha mpya na kuibua maswali kuhusu mwelekeo wa siasa za Tanzania baada ya Rais Samia kuingia madarakani.

Uhuru wa vyombo vya habari
Mnamo Aprili 6, 2021, siku chache baada ya kuwa Rais, Samia Suluhu Hassan aliagiza Wizara ya Habari kuvifungulia vyombo vya habari vilivyokuwa vimefungiwa. Hatua hiyo ilitafsiriwa kama mwanzo wa kuimarisha uhuru wa habari nchini.

Alisisitiza kuwa vyombo vya habari vifunguliwe lakini vifanye kazi kwa kuzingatia sheria na miongozo, akionya dhidi ya kufungia vyombo vya habari kwa ubabe. Pia alisisitiza kuwepo kwa kanuni wazi zinazoeleza makosa na adhabu zake.

Hata hivyo, katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na matukio ya kufungiwa kwa vyombo vya habari. Mfano, siku chache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, jukwaa la mijadala la JamiiForums lilifungiwa kwa siku 90, hali iliyotafsiriwa na baadhi ya wadau kama kubana uhuru wa kujieleza. Pia kumeshuhudiwa kufungiwa kwa baadhi ya vyombo vya habari kama Mwananchi na Jambo TV.

Vilevile, kumekuwepo na madai ya uthibiti wa maudhui, hasa kwa vyombo vinavyoripoti taarifa zinazokwenda tofauti na msimamo wa mamlaka. Baadhi ya vyombo vimedai kupokea simu kutoka kwa watu wasiojulikana wakivitaka kuondoa maudhui fulani.

Hali hii inaacha maswali mengi kuhusu dhamira ya awali ya kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari. Je, dhamira hiyo imeyeyuka, au kuna sababu nyingine zimeleta mabadiliko hayo?

Mwelekeo wa kidiplomasia
Katika miaka miwili ya mwanzo ya uongozi wake, uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na mataifa ya Magharibi, hususan Ulaya, ulitajwa kuimarika. Kauli mbiu ya “Mama amefungua nchi” ilisikika mara kwa mara, huku ziara za kimataifa zikiongezeka.

Rais Samia alisisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuzingatia misingi ya demokrasia, uhuru wa kujieleza na haki za binadamu. Mazingira haya yalichochea kurejea kwa baadhi ya misaada na mikopo, pamoja na wadau wa maendeleo kufungua upya ushirikiano.

Hata hivyo, katika miaka miwili ya hivi karibuni, baadhi ya wadau wa kimataifa wameeleza wasiwasi kuhusu hali ya haki za binadamu na utawala bora nchini. Umoja wa Ulaya, pamoja na mashirika mengine ya kimataifa, umeonesha kutoridhishwa na baadhi ya matukio, huku ukisisitiza uchunguzi huru na maridhiano.

Hali hii inaonekana kubadili mwelekeo wa kidiplomasia, huku baadhi ya wachambuzi wakihusisha hali hiyo na kupungua kwa misaada ya nje. Kauli ya Rais Samia kwamba “kwa sasa mabakuli hayawekewi pesa” imechukuliwa na baadhi ya wadadisi kama ishara ya mabadiliko katika uhusiano huo.

Wadadisi wa mambo wanaona kuwa kuna dalili za mwelekeo tofauti ukilinganishwa na dhamira ya awali iliyooneshwa kwa jumuiya ya kimataifa kuhusu uhusiano wa kidiplomasia.

Hitimisho
Kwa ujumla, mwenendo wa kisiasa, uhuru wa vyombo vya habari na diplomasia chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan unaonekana kupitia hatua mbili tofauti: matumaini ya mwanzo yaliyojengwa juu ya falsafa ya 4R, na maswali mapya yanayoibuka kutokana na matukio ya hivi karibuni. Ingawa hatua za awali zilionesha kufunguka kwa mazingira ya kisiasa na kidiplomasia, mabadiliko yanayodaiwa kujitokeza yanaibua mjadala mpana kuhusu iwapo dira hiyo bado inaendelea au imechukua mkondo mwingine.

Hivyo basi, Swali linalobaki ni kama Tanzania itaendelea na njia ya maridhiano na ufunguzi iliyotazamwa awali, au kama hali ya sasa itaashiria sura mpya ya uongozi.
 
Katika miaka ya mwanzo ya uongozi wake, Rais Samia Suluhu Hassan alionekana kubadili upepo wa kisiasa kwa kuonesha utashi mpya uliogusa moja kwa moja masuala ya demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari na mwelekeo wa

Hivyo basi, Swali linalobaki ni kama Tanzania itaendelea na njia ya maridhiano na ufunguzi iliyotazamwa awali, au kama hali ya sasa itaashiria sura mpya ya uongozi.
Sababu ni hii: Aggressive supreme of power! and hence the formation of a Cartel to OWN TANGANYIKA with cronies including Uncles from Arabs!
 
Ukweli ni kuwa Samia ni mtu laghai na analinda zaidi maslahi ya kimadaraka yake binafsi na chama chale. Alichokuwa anasema mwanzo alitegemea chama chake kitakuwa salama madarakani, lakini alipoangali uhalisia akajua akitekeleza hizo 4R ni kutaka kukianganiza chama chake kilichopoteza ushawishi kwa umma.

Hata akiitisha maridhiano sasa itakuwa ni danganya toto. Kinachotakiwa ni mapambano ya kumwaga damu ili kukiondoa chama chake.
paskali mayalla hayaland
 
Katika miaka ya mwanzo ya uongozi wake, Rais Samia Suluhu Hassan alionekana kubadili upepo wa kisiasa kwa kuonesha utashi mpya uliogusa moja kwa moja masuala ya demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari na mwelekeo wa kidiplomasia. Kauli na hatua zake za awali zilijenga taswira ya kufungua milango iliyokuwa imeonekana kufungwa, huku wadau mbalimbali wa siasa, wanahabari na jumuiya ya kimataifa wakianza kuona Tanzania ikiingia katika awamu mpya ya demokrasia na ushirikiano.

Hata hivyo, kadri muda ulivyokwenda, hasa baada ya miaka mitatu ya mwanzo, mjadala unaibuka kuhusu iwapo mwelekeo huo umeendelea au umebadilika. Zipo dalili za kusuasua kwa utashi wa kisiasa, mabadiliko katika uhuru wa vyombo vya habari, pamoja na mitazamo mipya ya kidiplomasia ambayo inaonekana kutofautiana na matarajio ya awali.

Hali hii inaibua swali kubwa: ni nini hasa kimebadili mwelekeo wa Rais Samia kwenye maeneo haya matatu yanayogusa mustakabali wa demokrasia nchini?

Uhuru wa kisiasa
Baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani, vyama vya siasa vilikuwa vimewekewa vikwazo katika kufanya shughuli za kisiasa. Shughuli za kisiasa, hasa kwa vyama visivyounda dola, zilikuwa zimeingia katika giza zito kutokana na zuio la mikutano ya hadhara.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kukabidhiwa kijiti cha uongozi kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Rais Samia alikuja na falsafa ya 4R (Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Ujenzi upya) ambayo ilitafsiriwa na wengi kama ufunguo wa siasa mpya nchini.

Hatua hiyo ilishuhudia shughuli za kisiasa zikianza kufanyika. Vyama vya upinzani vilianza kufanya mikutano na hata maandamano bila vikwazo vilivyozoeleka awali. Baadhi ya wakimbizi wa kisiasa pia walianza kurejea nchini.

Katika mazingira hayo, matarajio ya wadau wengi yalikuwa makubwa kuhusu mwelekeo mpya wa siasa. Rais Samia alipokea pongezi na hata tuzo kwa juhudi za kupunguza joto la kisiasa, huku fursa ya kukosoa na kukosoana ikionekana kurejea bila hofu.

Sasa mambo ni tofauti
Hata hivyo, katika kipindi cha takribani miaka miwili iliyopita, mwelekeo huo unaonekana kuyumba. Mfumo wa 4R unaonekana kupungua nguvu, huku baadhi ya vyama vya siasa na wanasiasa wakipitia misukosuko inayohusishwa na dola.

Kwa mfano, imeshuhudiwa Chama kikuu cha upinzani, CHADEMA, kikishindwa kushiriki uchaguzi kwa kusisitiza mabadiliko ya sheria za uchaguzi. Baadhi ya wadau wanaamini kuwa katika mazingira hayo, falsafa ya 4R ingeweza kutumika kuleta suluhu.
Aidha, matukio ya kukamatwa kwa wanasiasa wakosoaji wa Serikali yameanza kurejea. Mfano ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ambaye yuko gerezani akikabiliwa na kesi ya uhaini. Baadhi ya wadau wamependekeza maridhiano, huku Serikali ikisisitiza kuwa suala hilo liko mikononi mwa vyombo vya kisheria.

Matukio haya, pamoja na zuio la baadhi ya mikutano ya upinzani, sarakasi katika cahaguzi, yanajenga picha mpya na kuibua maswali kuhusu mwelekeo wa siasa za Tanzania baada ya Rais Samia kuingia madarakani.

Uhuru wa vyombo vya habari
Mnamo Aprili 6, 2021, siku chache baada ya kuwa Rais, Samia Suluhu Hassan aliagiza Wizara ya Habari kuvifungulia vyombo vya habari vilivyokuwa vimefungiwa. Hatua hiyo ilitafsiriwa kama mwanzo wa kuimarisha uhuru wa habari nchini.

Alisisitiza kuwa vyombo vya habari vifunguliwe lakini vifanye kazi kwa kuzingatia sheria na miongozo, akionya dhidi ya kufungia vyombo vya habari kwa ubabe. Pia alisisitiza kuwepo kwa kanuni wazi zinazoeleza makosa na adhabu zake.

Hata hivyo, katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na matukio ya kufungiwa kwa vyombo vya habari. Mfano, siku chache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, jukwaa la mijadala la JamiiForums lilifungiwa kwa siku 90, hali iliyotafsiriwa na baadhi ya wadau kama kubana uhuru wa kujieleza. Pia kumeshuhudiwa kufungiwa kwa baadhi ya vyombo vya habari kama Mwananchi na Jambo TV.

Vilevile, kumekuwepo na madai ya uthibiti wa maudhui, hasa kwa vyombo vinavyoripoti taarifa zinazokwenda tofauti na msimamo wa mamlaka. Baadhi ya vyombo vimedai kupokea simu kutoka kwa watu wasiojulikana wakivitaka kuondoa maudhui fulani.

Hali hii inaacha maswali mengi kuhusu dhamira ya awali ya kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari. Je, dhamira hiyo imeyeyuka, au kuna sababu nyingine zimeleta mabadiliko hayo?

Mwelekeo wa kidiplomasia
Katika miaka miwili ya mwanzo ya uongozi wake, uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na mataifa ya Magharibi, hususan Ulaya, ulitajwa kuimarika. Kauli mbiu ya “Mama amefungua nchi” ilisikika mara kwa mara, huku ziara za kimataifa zikiongezeka.

Rais Samia alisisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuzingatia misingi ya demokrasia, uhuru wa kujieleza na haki za binadamu. Mazingira haya yalichochea kurejea kwa baadhi ya misaada na mikopo, pamoja na wadau wa maendeleo kufungua upya ushirikiano.

Hata hivyo, katika miaka miwili ya hivi karibuni, baadhi ya wadau wa kimataifa wameeleza wasiwasi kuhusu hali ya haki za binadamu na utawala bora nchini. Umoja wa Ulaya, pamoja na mashirika mengine ya kimataifa, umeonesha kutoridhishwa na baadhi ya matukio, huku ukisisitiza uchunguzi huru na maridhiano.

Hali hii inaonekana kubadili mwelekeo wa kidiplomasia, huku baadhi ya wachambuzi wakihusisha hali hiyo na kupungua kwa misaada ya nje. Kauli ya Rais Samia kwamba “kwa sasa mabakuli hayawekewi pesa” imechukuliwa na baadhi ya wadadisi kama ishara ya mabadiliko katika uhusiano huo.

Wadadisi wa mambo wanaona kuwa kuna dalili za mwelekeo tofauti ukilinganishwa na dhamira ya awali iliyooneshwa kwa jumuiya ya kimataifa kuhusu uhusiano wa kidiplomasia.

Hitimisho
Kwa ujumla, mwenendo wa kisiasa, uhuru wa vyombo vya habari na diplomasia chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan unaonekana kupitia hatua mbili tofauti: matumaini ya mwanzo yaliyojengwa juu ya falsafa ya 4R, na maswali mapya yanayoibuka kutokana na matukio ya hivi karibuni. Ingawa hatua za awali zilionesha kufunguka kwa mazingira ya kisiasa na kidiplomasia, mabadiliko yanayodaiwa kujitokeza yanaibua mjadala mpana kuhusu iwapo dira hiyo bado inaendelea au imechukua mkondo mwingine.

Hivyo basi, Swali linalobaki ni kama Tanzania itaendelea na njia ya maridhiano na ufunguzi iliyotazamwa awali, au kama hali ya sasa itaashiria sura mpya ya uongozi.

Kumbe alisikia huku.
 
Back
Top Bottom