Kwa mara nyingine tena Wajanja wamebuni mpango wa kujisaidia wenyewe kwakua hawa waliopata ufadhili kupitia Samia scholarship ni watoto ambao wengi wao walisoma masomo ya sayansi, yaani PCM, PCB na EGM. Watoto na wazazi walijuwa kuwa 98% ya watoto ambao wanasoma masomo ya sayansi (physics, Chemistry, Biology, Hesabu, Agriculture, Zoology kule A' Level moja kwa moja wanalenga kwenda kusoma kozi za sayansi kule vyuo vikuu, hivyo sio kweli kuwa Samia scholarships zingewavutia watoto hawa kwenda kusoma fani za sayansi, kwakuwa kwa kusoma tahasusi za sayansi kule sekondari tayari walishaamua (narrow) kusoma kozi za sayansi huko mbele ya safari vyuo vikuu, hivyo Samia Scholarship sio kwaajili ya mtoto bali ni kwaajili ya mzazi kupunguziwa gharama za kumsomesha mwanawe ambae tayari walishaamua na mwanawe kusoma masomo ya sayansi ili hatimae wasome kozi za sayansi chuo kikuu.
Dhambi iko wapi hapo? Dhambi inakuja pale Samia scholarship inapogharamia hata wale watoto waliosoma shule za ada kubwa, automatically watoto hawa wana nafasi ya kusoma vyuo vikuu kozi za sayansi hata bila Samia scholarship wala mkopo. Hii maana yake imekwenda kupunguza uwezo wa watoto masikini kupata msaada wa kusoma vyuo vikuu kozi za sayansi.
Ikumbukwe kuwa 90 ya wanafunzi wanaosoma A' Level shule nzuri kama tabora boys, tabora boys, Kilakala, dakawa, Msalato, Iliboru, nk ni watoto ambao wamesoma shule za private za msingi na sekondari (O' Level) na kuchaguliwa kwenda hizo shule za vipaji maalum,
Hii maana yake ni nini?: Ina maana kuwa elimu itakuwa kwa watoto wa tabaka fulani tu, kwakuwa watoto wanaosoma hizi shule binafsi zenye walimu na mazingira mazuri ya kusoma ndizo zinazotoa watoto wenye ufaulu mkubwa wa kuweza kupata Samia scholarships, kuchaguliwa vyuo vya serikali vyenye ada nafuu na kupata mikopo pia. Hili ni kundi la watoto ambalo wazazi wao wana uwezo mkubwa wa ku lobby kwenye bodi ya mikopo na taasisi za fedha ili watoto wao wapate mikopo au ufadhili.
Samia scholarship ungebaki kuwa mfuko wa wanyonge tu waliofanya vizuri darasani kwenye masomo ya sayanzi, na hii ndio njia madhubuti ya kupunguza pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho nchini.