Samia Scholarship ni uwekezaji wenye tija

Hii kitu ni ujinga tu na imekaa kisiasa sana
 
Shule za binafsi zinaongoza kwenye udanganyifu wa matokeo, Samia scholarships ni mchongo kwa watoto wa wazazi wanaojiweza kujirudishia fedha walizotoa kupeleka watoto wao shule za private. Kwakutumia samia scholarships tujiandae kuona watoto wengi shule za private wakipata ufaulu mkubwa sana (mchongo) ili wawahi siti za mbele za samia scholarships na kupata nafasi vyuo vikuu vya serikali vyenye ada nafuu. Yaani jasho jingi wakati wa amani ili damu kidogo wakati wa vita.
 
Ndugu zangu waliostahili Samia scholarships na mikopo hawakupata kwakuwa projects zote hizo ni mbinu za kuwawezesha watoto kumudu kusoma vyuo vikuu. Mimi nina ushahidi kuwa hakuna uhaba wa watoto wa kike kwenye kozi za sayansi na elimu ya tiba kwenye vyuo vyetu kiasi cha kuhalalisha samia scholarships na mikopo kupewa hata watoto waliomaliza kwenye shule zenye ada kubwa sanakama FEZA na nyinginezo za aina hiyo. Huu ni upigaji fedha za umma sawa na upigaji mwingine. Ona sasa watoto wa masikini wamebaki nyumbani kwa kukosa ada wakati watoto wa matajiri wamepewa samia scholarships, mikopo ya students' loans board, mikopo ya NMB, scholarships za vodacom na kupewa udahiri kwenye vyuo vya serikali vyenye ada nafuu. mtoto wa mkulima, mmachinga, mvuvi, mfugaji, mama ntilie na muoka vitumbua hana access ya fursa hizi zote. Hii ni dhambi kubwa sana kutokea nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…