Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoani Arusha, tarehe 08 Machi, 2025 amesema sherehe hizo zitakuwa zinafanyika Kimikoa lakini zitafanyika kitaifa kila baada ya Miaka mitano.
Hivyo, sherehe nyingine za aina hiyo zitafanyika Mwaka 2030 atakapokuwa anaachia madaraka ya Urais na kukabidhi kijiti kwa mwingine.
Swali la kujiuliza ana hakika gani kama atakuwa Rais!!?? Ina maana ana maamuzi ya wapiga kura?!!! Ina maana uchaguzi utakaofanyika ni Maigizoo??!! Nawaheshimu sana Mpango na Kinana... Wana akili kubwa sanaa....
InshaAllah , lakini mama hiki ndio kipindi cha kwanza ....tunakuhitaji hadi 2035 panapomajaliwa ..hakuna kama wewe unaupiga mwingi .. ujenzi kila mahali ..sekta ya afya na elimu kumetaradadi...
haha angalau hata angeweka neno Munguakipenda lkn waislamu hawana hilo neno hata hivyo, hajui mpaka 2030 is a loong time chochote kinaweza kutokea kati ya leo na 2030 …
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa maadhimisho mengine ya Siku ya Wanawake yatafanyika mwaka 2030 wakati atakapoachia ngazi.