GE2025 Samia Suluhu afanya mazungumzo na viongozi wa Kanisa Katoliki mkoa wa Tabora

GE2025 Samia Suluhu afanya mazungumzo na viongozi wa Kanisa Katoliki mkoa wa Tabora

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora Kardinali Protase Rugambwa pamoja na Baba Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo hilo Mhashamu Baba Askofu Paul Ruzoka, Ikulu Ndogo ya Tabora tarehe 12 Septemba, 2025. Pamoja na mambo mengine pia Maaskofu hao walimuombea Rais Dkt. Samia ambaye anagombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
1757671161375.png


1757671173563.png


1757671191147.png


 
Penye uzia penyeza rupia!

Hapo wengine wataendelea na Novena, wengine watabaki upande huo 🙌
 

Katoliki.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na viongozi wa Kanisa Katoliki katika Ikulu Ndogo ya Tabora leo Septemba 12.

Viongozi hao ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, Kardinali Protase Rugambwa, pamoja na Askofu Mkuu Mstaafu wa jimbo hilo, Mhashamu Paul Ruzoka.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wa dini wamepata nafasi ya kubadilishana mawazo na Rais Samia kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii na kitaifa. Kadhalika, wamemwombea baraka na mafanikio katika majukumu yake ya uongozi.

Aidha, maaskofu hao wamemtakia heri njema Rais Samia ambaye ni mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
 
Tabibu hayupo kwaajili ya walio wazima bali walio wagonjwa.

Yesu Kristo hakuja Duniani kwaajili ya watakatifu, bali wadhambi, ili watubu, wapate kuokoka.

Kama Rais Samia ataenda mbele za Mungu na kuomba toba, ni nani atazuia msamaha wake? Ila akienda kuomba toba, huku moyoni akiendelea kuagiza au kubariki watu kutekwa na kuuawa, kutekwa na kupoteza, kubambikia wapinzani wake kesi za uhaini, na kudhulumu haki mbalimbali za binadamu wenzake, hata angeenda kwa Papa, inakuwa ni kupoteza muda.

Samia akijitenga na uovu, akakubali kuona thamani ya uhai wa binadamu wenzake, akathamini haki za wanadamu wenzake, hakika ni wengi tutamwunga mkono katika dhamira yake iliyo njema na takafifu mbele za Mungu.

Vyeo na madaraka ni vya muda mfupi sana, lakini maisha baada ya kifo ni ya milele. Fikirieni zaidi maisha ya milele kuliko ya muda mfupi.
 
Yesu hakuwafukuza makahaba wala watoza ushuru walioenda kuomba toba kwake. Hakuna mtumishi wa Mungu anayeweza kumfukuza mtu yeyote mwenye nia ya kuombewa eti kwa sababu anamwona mtu huyo ni mwovu, maadam haenda kwa kasisi huyo kuomba aubariki uovu wake. Labda pengine ameenda kuombewa kuacha roho ya dhambi inayomfanya akubaliane na kuteka na kuwaua watu wanaomkosoa, au pengine ameenda kuombewa aondokane na shetani aishiye ndani yake anayemfanya awabambikizie kesi washindani waje, n.k.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora Kardinali Protase Rugambwa pamoja na Baba Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo hilo Mhashamu Baba Askofu Paul Ruzoka, Ikulu Ndogo ya Tabora tarehe 12 Septemba, 2025. Pamoja na mambo mengine pia Maaskofu hao walimuombea Rais Dkt. Samia ambaye anagombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Samia kwa akili yake anajidanganya huyo ndio kiongoz mkuu wa wacatholik tanzania wakati huyo ni askofu kama askofu wengine cheo chake ni vatican kuchagua papa
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora Kardinali Protase Rugambwa pamoja na Baba Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo hilo Mhashamu Baba Askofu Paul Ruzoka, Ikulu Ndogo ya Tabora tarehe 12 Septemba, 2025. Pamoja na mambo mengine pia Maaskofu hao walimuombea Rais Dkt. Samia ambaye anagombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Sijui ni mimi tu nnaemuona Kardinali amekaa kijasusi sana
 
Back
Top Bottom