Tabibu hayupo kwaajili ya walio wazima bali walio wagonjwa.
Yesu Kristo hakuja Duniani kwaajili ya watakatifu, bali wadhambi, ili watubu, wapate kuokoka.
Kama Rais Samia ataenda mbele za Mungu na kuomba toba, ni nani atazuia msamaha wake? Ila akienda kuomba toba, huku moyoni akiendelea kuagiza au kubariki watu kutekwa na kuuawa, kutekwa na kupoteza, kubambikia wapinzani wake kesi za uhaini, na kudhulumu haki mbalimbali za binadamu wenzake, hata angeenda kwa Papa, inakuwa ni kupoteza muda.
Samia akijitenga na uovu, akakubali kuona thamani ya uhai wa binadamu wenzake, akathamini haki za wanadamu wenzake, hakika ni wengi tutamwunga mkono katika dhamira yake iliyo njema na takafifu mbele za Mungu.
Vyeo na madaraka ni vya muda mfupi sana, lakini maisha baada ya kifo ni ya milele. Fikirieni zaidi maisha ya milele kuliko ya muda mfupi.