Samia Suluhu baada ya kutembelea ziara Korea Kusini, wamarekani watoa uzushi

Mbona mamayo kutwa anajipendekeza huko
Hata kukemea ushoga hadharani aligoma
Hamna lolote hapo
Serikali yetu haieleweki ipo upande gani
Wapi na lini alijipendekeza kama sio wao walimualika? VP Kamala si ndio alimualika au?

Nawa wakajileta huku Tanzania na ahadi kemkem 😁😁

Waache wivu,Tanzania ilishahama kuwa Nchi ya kuendeshwa na kubembeleza.Sera yetu ya Kutofungamana na upande wowote inatumipa.

Najua hamjui ila Iran ni bilateral lender mkubwa wa Tanzania labda saizi Korea ndio itampita.
 
Na moja ya mbinu ya mataifa makubwa ni pamoja na kudhoofisha nchi zingine kiuchumi, kiteknolojia na ikibidi hata kisiasa na kijeshi. Marekani kupitia shirika lake la kijasusi ilitumia kila mbinu chafu kuwatenganisha ndugu wa tumbo moja KOREA ikazaliwa Korea Kusini na Korea Kaskazini huku USA ikilalia Korea Kaskazini na kumuona Korea Kusini kama "nunda" na adui. Korea Kusini imewekewa vikwazo chungu nzima na Marekani hasa katika eneo la ubunifu wa teknolojia ya zana za kivita bila mafanikio.
Ulikuwa unakwenda vizuri kidogo katika kunadi mbuzi wa mama akiwa ndani ya gunia, hadi ulipofikia hapa ukakwama!

Pole zako.
Kuna mambo umeyaandika vizuri 'kidogo kipropaganda, lakini kwa msomaji mwenye upeo anasoma takataka nyingi humo humo kwenye andiko lote. Pengine hizi ni hela za waarabu zinazowakesha usiku mzima mkitafuta namna za kupotosha watu wasione janga la huyu mama yenu analolifanyia nchi hii.

Hebu tuwekee huo mkataba wa miaka 40 na sisi tujionee asli zilizomo humo kutufaidisha sote.'

Hebu elewa hili: Kinachotokea sasa ni mama kufanya mambo yake gizani waTanzania wasijue.Baada ya Lile zoezi la DP World kuwa kama lilivyokuwa, Samia kajiapiza kitu cha namna ile hakitatokea tena. Sasa tunauzwa tu kimyakimya.; na inapobidi, chawa kama wewe mpo tayari kupiga propaganda zisizokuwa na kichwa.
 
Nasikitika umekosea sehemu ya kupeleka porojo zako ziszo kichwa wala mguu. Hauelewi kitu wewe hata historia ya korea ulioandika ni feki kama lilivyo bandiko lako lote. Tafuta jukwaa jingine kama ukivyoshindwa huko x haata hapa umechemka

Pia kamwambie anayekulipa kuwa majamaa hayadanganyiki badala yake yana maswali hadi nimekimbbia labda uniongezee watu kama iivyotokea korea ambapo wakorea 4 wamewabana vilivyo watz 30
 
Wamepata wivu baada ya Nchi ndogo kama Korea kutoa Mkopo wa Trilioni 6.5 Kwa Nchi maskini ya Tanzania kuisaidia Ili uweze kujijenga zaidi.

Mbaya zaidi wao walimualika Kibaraka wao Ruto wakaishia kumpa Msaada wa kufundisha Polisi na ujinga mwingine wa vihela vya Demokrasia 😂😂😂😂😂

Tunawashukuru sana Korea.

-Daraja la Tanzanite ni Korea
-Daraja la Malagarasi ni Korea
-Chuo Cha Tehama Manyara na Dodoma ni Korea
-Hospital ya Mlonganzila ni Korea.
-Vichwa Cha Trni ya Sgr ni Korea.

On top of that Sasa watasaidia Stamico kupata ujuzi wa Madini mkakati Ili kutujengea uwezo.
Hata ujenzi wa meli mpya MV Mwanza Hapa Kazi Tu
ni Korea
 
Mbona mamayo kutwa anajipendekeza huko
Hata kukemea ushoga hadharani aligoma
Hamna lolote hapo
Serikali yetu haieleweki ipo upande gani
Mama hajioendekezi kwa mtu na sisi pia sera yetu kimataifa inafahamika vyema kabisa. Hatuna budi mtu wala kufungamana na mtu yeyote yule waka kupewa adui wa kumchukia na kutokushirikiana naye.
 
Yaani hii dunia ya GIVE and TAKE Wakorea wanaweza kutoa pesa zote hizo kwa NTEREST RATE ya 0.01 % kwa miaka 40 bila kufaidika na lolote....!!? Bila hata kuchukulia INFLATION in the equestion, 0.01 % hawezi kuwa na rertun on investment ... sana sana ni hasara. After 40 years thamani ya hiyo pesa itakuwa imeshuka by almost half..... Tusidanganyane hapa. Unless hiyo pesa ni kwa ajili ya CCM kwa uchaguzi ujao au deal la ABDUL na Mama yake.
Sasa kwa mfano angalia hili aliloweka huyo anayedharau akili za watu humu!!
Ahsante mkuu 'The Khoisan', waongo hawa ni kama hata kutunga uongo hawana uwezo nalo.
 
WE Mbwiga hebu tuambia na uzushi kuhusu Do World, Ngorongoro na Hekta Mili 8 ya Misitu yetu!! Then tohoa huo Ukweli Ili tuelewe kuhusu Hilo la Korea
Na Bollen Ngetti
0683 226539
B-pepe bollenngeti@gmail.com

SIKU tatu kabla Rais Samia Suluhu Hassan hajaelekea Korea Kusini kuhenyea kwa ajili ya nchi yake niliandika huko kwa Max (X) kwamba, "Rais Samia unaenda Korea Kusini lakini jiandaye na matusi, kejeli , dhihaka na hata uzushi kutoka Marekani".

KWELI, Rais Samia Suluhu Hassan amefika Korea na kufanikisha dili la mkopo wa Shilingi 6.57 Trilioni wa sharti nafuu ikiwamo riba ya 0.01% kwa muda wa miongo 4 inayoanzia 2026. Fedha ambayo itaelekezwa katika miradi ya kimkakati inayolipa kama sekta ya usafirishaji na uchukuzi!

Mara baada tu ya Rais kufanikisha jambo letu HIMA Marekani kupitia sauti yake, Voice of America, VoA ikaandika uzushi, dhihaka na matusi kwamba, "Tanzania imesaini mkopo wa fedha na Korea Kusini kwa sharti la kugawa sehemu yake ya bahari na madini". Ujinga uliovuka mawingu!

Hivi, katika hali tu ya kawaida Rais Samia ni mwendawazimu, mjinga, asiye na akili wala uzalendo kiasi gani hadi atoe sadaka ya sehemu ya bahari na madini yetu kwa gharama ya mkopo ambao bado tutailipa? Kwa nini isingekuwa mbadilishano wa hayo matrilioni na kipande cha bahari na madini ili lojiki iwepo? Yani unaenda kwa Mangi unamwambia akukopeshe mchele wa kilo 50 kwa ajili ya shughuli ya binti yako utamlipa mwisho wa mwezi na hapo hapo unamwambia njoo nyumbani nikupe fremu bure pamoja na kwamba mchele wako nitakulipa mwisho wa mwezi! VoA na Joseph Biden mmetukosea sana kwa ujinga huu. We can be stupid but not fool to that extent!

Watanzania tuelewe mambo mawili hapa kama si moja kubwa! Na atakayeelewa awaeleweshe wengine 10 wasio na smart phones. Kwanza kuna vita kubwa ya kiuchumi duniani. Kila Taifa linatumia kila aina ya mbinu halali na haramu kujiweka sawa kiuchumi maana uchumi ndio kila kitu.

Na moja ya mbinu ya mataifa makubwa ni pamoja na kudhoofisha nchi zingine kiuchumi, kiteknolojia na ikibidi hata kisiasa na kijeshi. Marekani kupitia shirika lake la kijasusi ilitumia kila mbinu chafu kuwatenganisha ndugu wa tumbo moja KOREA ikazaliwa Korea Kusini na Korea Kaskazini huku USA ikilalia Korea Kaskazini na kumuona Korea Kusini kama "nunda" na adui. Korea Kusini imewekewa vikwazo chungu nzima na Marekani hasa katika eneo la ubunifu wa teknolojia ya zana za kivita bila mafanikio.

Wananchi wa Korea Kusini waliamua kushikamana na kujenga uzalendo kwa nchi yao wa kupigiwa mfano baada ya kuona, "hatuna ndugu wala mjomba, lazima tujikomboe wenyewe" na pakwanza walipoanzia na kupambana na kushinda saratani ya rushwa na ufisadi na kumtambua kila Mkorea Kusini alipo ndani na nje ya nchi yao na anafanya nini kwa maslahi ya Korea Kusini!

Nimkumbushe Mtanzania jambo ambalo limewahi kutokea lakini haikuandikwa popote na kokote rasmi! Miaka michache tu zilizopita Jeshi letu la Ulinzi limewahi kuwa na haja ya Rada kwa ajili ya Ulinzi wa anga ambayo ingefungwa Morogoro. Maombi yalienda kwa nchi nyingi ikiwemo USA ya Joseph Biden aka Joe Biden bila mafanikio.

Ni hawa hawa Korea Kusini walikubali kutufungia mitambo hiyo tena kwa "Siri Kubwa" Marekani isijue maana ingeleta mushkeli wa kidiplomasia kati yetu na wao. Wakijifanya wakulima wa mboga -mboga mchana lakini kumbe ni mainjinia walifuzu, Wakorea walifunga mitambo.

Hata hivyo USA ilipogundua ilileta shida lakini kwa ukomavu wetu wa kidiplomasia Tanzania ya Jakaya Kikwete iliwaambia USA, "sisi tuna shida ya Rada, kama hamtami hawa watufungie basi mtupe yenu". USA ilikubali lile sharti na Korea Kusini ikafungasha virago maana na wao hawakuona sababu ya magomvi yao kutuathiri. Tuna historia ndefu na Korea Kusini kuliko USA kama nitakavyoeleza kupitia gazeti moja ya gazeti la wiki!

Kwa mantiki hiyo sikushangaa hata kidogo kwa Marekani kupitia TBC yao ya umma kutoa uzushi wa kijinga wenye lengo la kumchonganisha Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi wake kupitia mawakala wao ndani ya nchi kusambaza ujinga huo kuelekea Uchaguzi wa S/M kisha Uchaguzi Mkuu 2025 kwamba "Samia anauza nchi yetu" ili tu Samia achukiwe na chama chake! Huu ni uzushi wa kipumbavu usiovumilika na ninaamini USA itaomba radhi.

Tanzania ni nchi huru na sera yetu siku zote ni kutokufungamana na upande wowote katika vita za kiulimwengu. Hatuchaguliwi adui wala rafiki. Tunachoangalia ni maslahi mapana kwa nchi yetu na watu wake. Leo Iran imewekewa kila aina ya vikwazo vya kiuchumi lakini sisi ni marafiki na Iran na tunafanya nao biashara chungu mzima ikiwemo gesi asilia.

RAIS Samia wewe piga kazi! Hizo ni kelele tu za chura! Wewe hata chama Cha Hamas kikikubali kutujengea Zahanati kila kila Kijiji wewe nenda kasaini mikataba. Tungesikia kelele zao leo tungekuwa na Hospitali ya Palestina pale Sinza? Uongo ukiachwa kusikika sana hufikia hatua ya kuaminika kuwa ni kweli. Ukemewe mapema na kila mzalendo wa nchi YETU!
04/6/2024
Time: 11:23
Dar es salaam

Pia soma: VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini

Teuzi zinatafutwa jaman lah hadi kero
 
Nasikitika umekosea sehemu ya kupeleka porojo zako ziszo kichwa wala mguu. Hauelewi kitu wewe hata historia ya korea ulioandika ni feki kama lilivyo bandiko lako lote. Tafuta jukwaa jingine kama ukivyoshindwa huko x haata hapa umechemka

Pia kamwambie anayekulipa kuwa majamaa hayadanganyiki badala yake yana maswali hadi nimekimbbia labda uniongezee watu kama iivyotokea korea ambapo wakorea 4 wamewabana vilivyo watz 30
Kaandika baada ya kupata OFA ya MBs
 
Mtoa mada inawezekana ni chawa au umekurupuka kuandika uzi, kwanza uelewa wako ni mdogo unajichanganya mwenyewe yahani huwezi tofautisha kati ya Korea ya kusini na Kaskazini.

Kwa taarifa yako hao Korea ya kusini alipoenda huyo mama yako kuiuza Tanganyika ni washikaji wakubwa wa Marekani sasa sijui unataka kutueleza nini?
 
Wewe ni mpumbavu angalia land cruiser zote za miradi zenye plate number nyekundu(DFP) uangalie pia ubavuni zimeandikwa USAID. Zipo Tanzania nzima halafu ulinganishe na hao macho madogo( wachina) wameisaidia nn nchi yetu zaidi ya rushwa na kujenga miradi chini ya kiwango. Hizo Arv unazotumia bure wew na mkeo unajua unajua nani amekulipia? Ke.nge wewe
 
Back
Top Bottom