Samia Suluhu baada ya kutembelea ziara Korea Kusini, wamarekani watoa uzushi

Lucas anabubujikwa na machozi uzi wake umevurugwa posho itapungua leo
 
Ila tu tuwe wakweli hii mikopo inayokopwa na serikali naanza kupata doubt huenda ndo hii hii tunayokopeshwa online kwa riba ya asilimia 80 maana kampuni za kukopesha mbona zimekuwa nyingi sana nchini ?
 
Kuteteaga hayo mambo bila details huko mbele yanaweza waletea shida.

Tafuta habari zilizopelekea Ivory Coast na Ghana kuzuia uvuvi nchini kwao kwa sababu ya overfishing (wachina wamefanya fujo huko balaa).

Hujui meli ngapi za Korea zinaruhusiwa kuingia na kiasi gani wanavua. Hawa uvuvi wao sio kama wetu bila ya kuwa regulated, huko mbele wavuvi wadogo wadogo watajikuta awapati kitu.
 
Kumbe kuna watanzania wa ajabu kama huyu aliyeandiaka hii makala ambao wanatetea uhalifu na ubadhirifu na uuzaji wa maliasili zetu kutokana na ushabiki wa kijinga kabisa.

Hivi Korea ya kusini na Marekani kuna Tofauti gani?
Ina maana mleta mada Hajui kuwa Korea ya kusini kuna base kubwa ya Jeshi la Marekani na ndiyo inayoudhoofisha Korea ya Kaskazini ambayo ni nchi yq kijamaa ?
Kama hawa ndio washauri wa watawala wetu basi tumekwisha.

Yaani hajui kabisa kuwa Korea ya Kaskazini ni nchi ya Kijamaa na Korea ya Kusini ni nchi ya Kibepari inayoungwa mkono kwa nguvu zote na Marekani.

Hujui kuwa Watawala wetu wameshakua kama mawakala wa mabeberu na wamewakaribisha mabeberu kuja kuinyonya na kutapanya rasilimali za Tanganyika huku wakiwauzia ardhi yetu mamilioni ya hekari wakati wanajua wazi kuwa Mwalimu Nyerere aliwanyanganya Wazungu ardhi wakati huo idadi ya Watanganyika ikiwa haizidi mil. 17 na leo tumefikia mil. 65 Dr. Samia na serikali yake ya CCM inairudisha ile ardhi kwa Warabu na wazungu ambao pia ni mawakala wa Marekani.
Leo serikali inawapa wageni ardhi iliyozungukwa na miundo mbinu mizuri iliyojengwa kwa kodi za watu maskini huku wakiwaacha kwenye lindi la umaskini na kiwatajirisha watwala na wageni kwa manufaa yao.

Falme za Kiarabu (Dubai ) mfano ni kama Tawi la Marekani . Lakini machawa wengi hawajui hilo zaidi ya kudanganywa kuwa na sisi tutakua kama Dubai kwa kuwapa rasilimali zetu kwa mikataba ya kifisadi .Huko ndipo wanapokimbilia watawala wetu kuiweka reheni nchi yetu.
Na sasa wamehamia kwa maswahiba wengine wa marekani ambao ni Korea ya Kusini.

Korea ya Kaskazini ndio waliokua marafiki zetu kutokana na siasa zao za Kijamaa lakini sio Korea ya Kusini.
Korea ya Kaskazini ni nchi ya kijamaa ambayo hata mila,dini na tabia za nchi za kigeni kama ushoga haviruhusiwi kabisa.
Korea Kaskazini Watwala wengi machawa wa Marekani hawawezi kwenda kamwe.


Korea ya Kaskazini Dr. Samia hawezi na hadhubutu kwenda kwa sababu anahofia kupoteza sifa lukuki anazozipata kutoka nchi za Kimagaharibi ikiwemo Marekani na maswahiba wake.

Kwa hiyo mnapotoa sifa au mnapokosoa muwe na Data sahihi na sio kumpa mtu sifa za kuwapotosha watanzania.

Korea ya kusini ni nchi Tajiri sana ukanda huo wa nchi za Asia na ina viwanda vingi sana na teknolojia ya juu sana .

Korea ya kusini ni adui mkubwa wa China na Korea ya Kaskazini.
Na Pia Korea ya Kusini ni rafiki mkubwa wa nchi za magharibi.

Kwa hiyo Dr.Samia ameenda kukopa kwa rafiki mkubwa sana wa Marekani na adui wa ujamaa duniani.

2025 mtaamua wenyewe nchi ipigwe mnada au mumpige kibuti mtu arudi nyumbani kwake akapumzike ale kiinua mgongo kikubwa cha makamu wa Rais na kama Rais mstaafu.
Tuamue moja Kuzineemesha nchi za magharibi na marafiki zake au kulinda rasilmali za nchi na uhuru wa nchi na usalama wake kwa vizazi vijavyo.
 
Uzi wake umepotosha ukweli.

hajui tofauti kati ya Korea Kusini ya Kibepari na Korea Kaskazini ya Kijamaa.

Korea aliyoutaja ni ya Kusini ambayo ni rafiki mkubwa wa Marekani.
Kwa hiyo uzi wake umewapotosha sana watanzania.

Uzi wako ni mzuri tatizo lako umeegemea upande mmoja, wewe ni Pro-samia
 
Marekani ni Nchi ya kipumbavu,wao Misaada Yao ni ya ujinga ujinga na hawawezi kukupa hela yote Kwa pamoja.

Loh!! Pole sana. Nadhani ni tatizo la uelewa.

USA ndiyo nchi inayoongoza kwa kutoa misaada Dunia. Na sharti lao kubwa, heshimu haki, demokrasia na utawala wa sheria.

Hata hapa kwetu, kabla ya CCM kukoroga mambo, tulikuwa tunapewa msaada wa dola milioni 800 kila mwaka kupitia MCC, masharti makuu ni hayo hayo. Na hakuna nchi yoyote Duniani ambayo imewahi kutoa msaada wa pesa mkubwa kiasi hicho kwa nchi yoyote ya Afrika. Hapa naongelea msaada na siyo mkopo.

Taasisi kubwa kabisa ya fedha Duniani, WB, na ile ya Bank ya Afrika, kote huko, aliyewekeza pesa nyingi kuliko nchi yoyote ni USA. Hata kwente taasisi kubwa za UN kama vile WHO, WFPni USA.

Jielimishe kabla hujafikia kwenye hitimisho.
 
Hivi, katika hali tu ya kawaida Rais Samia ni mwendawazimu, mjinga, asiye na akili wala uzalendo kiasi gani hadi atoe sadaka ya sehemu ya bahari na madini yetu kwa gharama ya mkopo ambao bado tutailipa?
 
Umechapia sana hapo kwe hizo Korea mbili. South Korea ndiyo rafiki mkubwa wa Marekani na ndiyo Samia alipokwenda kuhemea. Jaribu kuhariri uzi wako vinginevyo utawapotosha wengi.
 
Bunafsi nikupongeze kwa kukumbuka kuandika namba za simu. Ila kiuhalisia sijaona mantiki ya Marekani kufanya hicho unachotaka kutuaminisha kwamba anamsagia kunguni Korea Kusini, hii ni kwasababu nchi hiyo ni mshirika muhimu sana kwa Marekani.
Angalau ingekuwa ni ziara ya kwenda Korea Kaskazini hapo ningesadiki hivyo unavyotueleza kwakuwa inafahamika wazi kuwa Korea Kaskazini ni hasimu wa nchi ya Marekani.
Kwahiyo wakati mwingine ndugu jitahidi uje na hoja zenye mashiko
 
Nimekuelewa sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…