Samia Suluhu, doa la kumfunga Mbowe halitafutika, watangulizi wako wote walilikwepa

Samia Suluhu, doa la kumfunga Mbowe halitafutika, watangulizi wako wote walilikwepa

Sasa rais ndio jaji mbona mnaingilia uhuru wa mahakama nyie kwanini mnamlazimisha mama samia afanye kazi ya jaji
 
Hivi nyie mnachekesha mnaweza kumfananisha mbowe na Mandela kwa kipi mbowe kafanya Tz ?
 
Kwahiyo tayari umeshahukumu kuwa kuna vyama vya kigaidi, kwa ushahidi wa kina Kingai?

Wala Mbowe hajuti ndio maana kila siku anatabasamu wala wana Chadema hawatajuta bali waliotengeneza UONEVU ndio watakaojuta na vizazi vyao.
Hajutii sianajua ametenda kweli subiri ashushiwe mvua za kutosha
 
Still something can be done to get away with this mess, and that is by having it thrown away and dismissed for good.
 
Kama wanatafuta namna ya kuitema hii kesi nyie kelele za nini mbowe sio gaidi mpaka mnaenda kuwalilia mabeberu
 
nyie siasa hamuijui hapo mbowe hafungwi kinachofanyika ni kumchosha tu na kumpotezea muda baaadaee anaachiwa watu washafanya yao wala msifikiri anafungwa siasa ni kazi kama kazi zingine tu
Hilo ni kosa la kimkakati,unaweza dhani una solve kumbe unaharibu kabisa,hapo ni sawa na kula embe lililoiva sana Ile michuzi unajifutia kwenye shati
 
Sawa, kama rais aliposema kuna ushahidi wa wazi hajaingilia mahakama, basi na watu wanaosema Mbowe si Gaidi waachwe waseme sio kuwaambia wanaingilia mahakama.
Mkondo wa sheria ukiishafika mahakamani muhimili wa serikali na ule wa bunge hukaa kimya na kuuachia muhimili wa mahakama kufanya kazi yake kwa uhuru bila kuingiliwa na mihimili mingine. Watu wa vijiweni hawakatazwi hawakatazwi kupiga stori zao zinazohusu mchakato wa mahakama unavyoendelea kwani vjiwe hivyo havina uwezo wa kuingilia mchakato wa mahakama. Na wala mahakama huwa hazisikilizi stori hizo za vijiweni. Na vijiwe hivyo vikiamua kufanya maandamano au fujo yo yote kuhusiana na mchakato huo, muhimili wa serikali utavikung'uta ipasavyo vijiwe hivyo. Kwa hiyo vijiwe hivyo vyenu kusema Mbowe si gaidi haiwezi kuingilia mchakato wa mahakama kwani havina uwezo huo. Vinajifurahisha tu.
 
Kwahiyo tayari umeshahukumu kuwa kuna vyama vya kigaidi, kwa ushahidi wa kina Kingai?

Wala Mbowe hajuti ndio maana kila siku anatabasamu wala wana Chadema hawatajuta bali waliotengeneza UONEVU ndio watakaojuta na vizazi vyao.
Hukumu inatolewa mahakamani na hakimu au jaji baada ya kukamilika mchalato wa kisheria. Huku kijiweni ni stori tu za kujifurahisha Mr/Mrs/Miss Quinine!
 
nyie siasa hamuijui hapo mbowe hafungwi kinachofanyika ni kumchosha tu na kumpotezea muda baaadaee anaachiwa watu washafanya yao wala msifikiri anafungwa siasa ni kazi kama kazi zingine tu
Wakiwa wamefanya yao yapi mkuu
 
Nyerere alisema hakuna chama makini kama Chadema wakati huo Mbowe akiwa Katibu Mkuu wa chama, Mkapa akaona isiwe tabu akatunga sheria Mwenyekiti na Mkurugenzi wa NEC wateuliwe na rais lengo likiwa ni kui-contain Chadema na Mbowe, Kikwete hadi akamuita Mbowe ikulu akanywa nae juice.

Magufuli pamoja na ujeuri wake alikuwa na uwezo wa kumfanya Mbowe chochote lakini hakuthubutu, alikuwa anafanya timing ili jumba bovu lisimwangukie yeye, wewe umethubutu kwa kuingizwa kingi na wajanja.

Uongozi ni KARAMA siyo kila mtu amepewa, jitahidi kuishi na viongozi wenzako vizuri hata kama ni kiongozi wa kijiji, elewa kuna watu wako nyuma yake wanamheshimu walimchagua.

Vyovyote utakavyofanya umfunge Mbowe au umuachie lakini hilo doa kwenye utawala wako huwezi kulifuta kamwe kama vile makaburu walivyomfunga Mandela wakamwachia lakini hadi leo dunia nzima inakumbuka.

Nimeshauri kwa staha.
Kamanda_Don_Linace__atuma_ujumbe_Kwa_Rais_Kwa_kusema_%3A%0A%0AMhe.Samia_Suluhu_Hassan_wewe_ni_...jpg
Tutamtoa_Mkoloni_Mweusi_Soon_on_Instagram%3A_%E2%80%9CMwenyekiti_wa_Chadema_Taifa_akisalimiana...jpg
 

Attachments

  • Tutamtoa_Mkoloni_Mweusi_Soon_on_Instagram%3A_%E2%80%9CMwenyekiti_wa_Chadema_Taifa_akisalimiana...jpg
    Tutamtoa_Mkoloni_Mweusi_Soon_on_Instagram%3A_%E2%80%9CMwenyekiti_wa_Chadema_Taifa_akisalimiana...jpg
    51.9 KB · Views: 2
Back
Top Bottom