Samia Suluhu Hassan ni Rais halali kabisa wa Tanzania, tusimdharau ila tumuombee afya, amani na azidishiwe hekima ya kutuongoza watanzania

Mama D kulikoni?
 
AAAMIN
 
Kula dona yako, nawa vizuri jipake mafuta ya kula ulale... Nchi waachie wenye meno
 
Kubwa linalowala viongozi wa CCM waliomo serikalini ni kule ushindi wao kutiliwa mashaka na sikutiliwa mashaka bali ni ushindi usiofuata taratibu,ushindi uliopatikana bila ya uwazi wa kura,ushindi bila ya kura halali si ushinsi ni wizi.
sasa yeyote yule ama aliepo au atakaerithi kutokana na kifo cha alie juu yake bado mshiko ni uleule Serikali iliyopo madarakani haikuchaguliwa kwa kura halali,fulustop.

Hapo hamuwezi kujipapatua ila kwa uchaguzi utakaokubalika,sasa kama mnajiamini CCM mpo na wananchama wengi ,kwa nini mnategemea ushindi wa magumashi,mbadilishe matokeo,mkamatwe na kura,mkimbie na masanduku ya kura ,Yote ya nini hayo ? Muwatumie polisi mhonge mawakala ,tabia zote hizo ndizo zilizoharamisha uchaguzi kwa maana hio waliomo ndani ya serikali na haswa wale waliopitia njia ya uchaguzi ,mishahara yao na posho na kila kitu ni haramu,haramu hio wanakula wao na watoto wao na jamaa zao,hilo sio jambo dogo kwa wenye imani ya kweli.yataka moyo wa jihadi ya nafsi kukataa mishahara na posho hizo.

Makelele ya kuwazuia msile na kupokea hela hizo zimegonga mwamba ,lakini makelele ya kusema hamkushinda kihalali hayo hamuwezi kuyanyamazisha hata majibwa usiku yakibweka yanasema serikali iliyopo madarakani haikushinda kihalali hata ndege na wanyama wote wanapiga makelele.
Msitegeee uongozi kuweza kuleta matumaini kwa wananchi ni shida juu ya shida ikipanda chati moja nyengine inatafuta kiki.

Mizimu inasema bila ya tume huru Tanzania itakuwa na mhaho mtupu. Kila kiongozi anakuja na kauli yake ,zinapingana .
 

Siasa za wanaojiita wapinzani ni za kulaumiana bila kuwa na suluhu la lawama. Huwezi kudeal na tatizo moja miaka30 na ukashindwa kulipatia dawa halafu unataka kuaminisha wananchi kuwa una dawa ya matatizo yao.

Sasa nyie na siasa zenu za mitandaoni endeleeni kulialia bila kujenga chama imara na bila kuwa na misingi imara kwa wananchi halafu mfikiri mtapewa dola kwa huruma...... mtasubiri sanaaaπŸ˜…πŸ˜… maana idadi hao wapiga kura hawana imani na nyie kabisaaa

Ushindi wa Biden mwenye kujinasibu kuwa baba wa demokrasia ulitiliwa shaka na bado ni ushindi halali na yupo madarakani
 
Ndio maana hata kwenye imani zetu tunapaswa kuwaombea viongozi wetu wa nchi kwani wao sio malaika...
 
Ni nani vile aliyesema wananchi wamekubali tozo? Hangaya anajitengenezea kudharaulika
 
Sikilizeni simulizi za wanayopitia akina Mdude na wengine wengi kutoka Kwa vyombo vya usalama kulinda maslahi ya mnaowaheshimu ndio muamue kama wanastahili hiyo heshima mnayowapa.
 
😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏😏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…