Uchaguzi 2020 Samia Suluhu: Hata mkipigia kura kule kwingine CCM ndio inaenda kuunda Serikali, tutashinda vikubwa sana Tanzania

Uchaguzi 2020 Samia Suluhu: Hata mkipigia kura kule kwingine CCM ndio inaenda kuunda Serikali, tutashinda vikubwa sana Tanzania

Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, (CCM), Mh. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 15/10/2020 amewambia wakazi wa Chunya mkoani Mbeya kuwa wasipige kura kwa Chama Kingine kwa sababu hata wakipiga kwingine Chama Cha Mapinduzi kinaenda kuunda serikali.

Amesisitiza kuwa watashinda vikubwa sana Tanzania, na amefananisha kupigia kura kwa chama kingine kama kitendo cha kumwaga sukari Ziwa Viktoria na kutegemea maji yatakuwa matamu, ambacho ni sawa na kupoteza sukari yako.

Mh. Samia amesisitiza kuwa maendeleo watakayoyaleta sio kwa wana CCM peke yake na wale ambao hawatokipigia Chama Cha Mapinduzi basi kura yao itawasuta pale watakapokuwa wanaletewa maendeleo.
Mama Samia yuko sahihi kabisa. Upinzani ushakufa zamani, na hivyo vyama vya wajasiriamali binafsi wataishia kuiona ikulu kwenye TV tu. Kuwapa kura hawa saccos na wenzake, na kutazamia ushindi ni upunguani wa kiwango cha 5G.
 
Makamu wa Rais huna cha kupoteza, utalipwa mshahara 80% mpaka unakufa. Lakini ujue Watanzania hawatawarudisha na mwenzio. Ulikuwa mama wa kupigiwa mfano, umekaa karibu na jiwe umekuwa mgumu!
Kwa mtazamo wako na akili zako nyingi unaona kabisa Tundu anashinda?.
 
Kura yao itawasuta pale wanapoletewa Maendeleo, Kwani hayo maendeleo ni fadhila ama ni lazima serikali ifanye hivyo?
 
She has spoken a very good point,because it's hard for opposition to defeat CCM . People loves CCM alot and they gonna vote for it no matter what.
Unamdhalilisha sana mzee Lowassa kwa kiingereza hiki
 
Huyu mama sijui amekumbwa na tatizo gani alikuwa makini kwenye kauli zake na kuheshimika lakini sasa hivi anaongea kama kama mlevi kabisa
 
Mama Samia yuko sahihi kabisa. Upinzani ushakufa zamani, na hivyo vyama vya wajasiriamali binafsi wataishia kuiona ikulu kwenye TV tu. Kuwapa kura hawa saccos na wenzake, na kutazamia ushindi ni upunguani wa kiwango cha 5G.
Kufikiria na kuunga mkono maneno ya Mama Samia na Magufuli ni kuwadharau wananchi..na kuwataka wajeuke kwenye uasi .
Lakini naweza kumuelewa mama samia , yuko soo frustrated kwakua Magufuli kamuachia mzigo mzima wa kampeni kama vile yeye ndio anagombea urais ...
 
🤣🤣🤣 Kuna watu huwa mnajifanya kuwajua sana watu zaidi ya wanavyojifahamu wao wenyewe.Kwahiyo wewe nae ni wakutoa vitisho kama hivyo?

Sidhani kama unayo hiyo nguvu ya kufanya hivyo, na kama unayo hauna haja ya kusemea huku kwenye fake ID's na penye watu wachache.Nenda kayaseme hayo unayotaka kuyasema kwenye mitandao mikubwa. Amini kwamba wewe ni mtu ambae uko uchi Sana mbele ya serikali.

NB:Ngoja nikucheke kidogo 🤣🤣🤣🤣🤣.

Mitandao mikubwa ni ile iliyosheheni mijitu isiyojulikana?

Usitutishe na wala usitufokee!
 
Tuwapigie Chadema wanao hitaji kura zetu.

Mtapoteza kuwapigia ccm, maana watashinda mkipiga na watashinda msipopiga.
 
Tupige kura ya kimbunga kwanza halafu hayo mengine tutajua mbele ya safari.
 
Makamu wa Rais huna cha kupoteza, utalipwa mshahara 80% mpaka unakufa. Lakini ujue Watanzania hawatawarudisha na mwenzio. Ulikuwa mama wa kupigiwa mfano, umekaa karibu na jiwe umekuwa mgumu!

Hakuwa wa mfano tangu hapo awali
 
Back
Top Bottom