Rais ajue kuna siku ni za upepo mkali hivyo nguo anazovaa lazima ziwe zimetiwa nanga au gololi marumaru nzito, nimeona kwa wale wanaofuatilia ziara zake haswa pale anapohitajika kukagua gwaride anaposimama ukivuma upepo inakuwa mswalie mtume. Hilo sio ninalotaka kulisema ila nahisi anahitaji nguo pana ili ajinafasi na awe free mbele za watu.
Nilichokusudia leo sasa hivi ni kuhusu pale inapoonekana anaenda mrama au kuna sintofahamu kati yake na anaoongozana nao, watu wakienda kulia yeye anaonekana anaenda kushoto na hapo ndio huzuka taharuki ya migangano kati ya Rais na walinzi na wale wahusika wa kumpeleka kukagua gwaride lao.
Na hili nimeliona karibu kila anapohitajika kukagua gwaride, inakuwa mtihani kwa Rais Samia, kuanzia ile siku pale Ikulu halikadhalika alipoenda Uganda kazi ikampata Museveni kumuelekeza mgeni wake.
Wahusika hawalioni hili na kumfahamisha Rais stepu za ukaguzi wa gwaride zaidi ampe nafasi ya kama mita moja na nusu yule anaeongoza kuliko kukaa karibu, mfahamisheni tu.
Maana mimi hubakia kufurahi na kucheka tu ikifika wakati Raisi anaenda kukagua, najua sasa mtihani,