Samia ,Traore chungeni ndimi zenu na waheshimu Mabeberu

Uhusiano wa Venezuela na USA tofauti kabisa na Tanzania na USA, huko Mmarekani anafuata mafuta, Tanzania yamegundulika madini sio mafuta.

Who are you waliambiwa wale mashoga wa EU hakuambiwa Mmarekani.
Jichanganye tu Kama ugali maharage wa jela! Eti EU! Yaani kwa elimu yako huujui uhusiano wa NATO ya EU na marekani? Na vile mlijitia vimbelembele kuililia Palestina mtajua tu maana ya usiwe rafiki wa adui yangu!
Umeifuatilia SA kilichomkuta baada ya kuandaa G20 ya mchongo? Kuna makubwa yatamkuta muda mfupi ujao na atajuta kuipigania Palestina na kuishtaki Israel ICC.
Badala ya kutafuta lobbyist wa kimataifa awapatanishe na mliowananga who are you mnajificha kwenye makambi ya jeshi. Dunia imevaa bukta kwa Sasa inatrot!
 
umeandika point za nguvu, shida ya maFISIMU hayana uelewa sidhani kama amekuelewa!
watu wanachaguliwa hadi mgombea uraisi na JK kwani yana akili basi?
 
Who Are You?

Waliambiwa hakina Trump!
 
Tumewazoea nyinyi mashabiki wa yote mabaya kwa upande wa TZ. EU wanazo ndoto za kijinga kupitia kwa machawa wao CHADEMA, wanachokitaka hakitakuja kutokea.

Ujumbe ulifikishwa ukafika. Akisema hayati JPM miaka ile kwenu poa tu akisema maneno yale yale SSH ishakuwa nongwa tayari.

Ulimwengu wa kidiplomasia huwa hauendi kama mnavyodhania.
 
JWTz wapo imara sana ndugu, houni matofali yanavyovunjwa pale taifa siku ya siku kuu ya uhuhu?, so marekani watachapwa vibaya mno... si jeshi letu ni la sita kwa ubora duniani? Chini ya CDF mwenyewe,
 
Nilidhani unatania US kumdaka Maduro. Bila kuingia JF ningechelewa sana kuipata habari hii. Al-jazeera wapo live kukamatwa kwa maskini jeuri Maduro. Russia aibu tupu, mchina anachungulia dirishani...
 
Daa! Hapo kwenye "kulaani vikali akiwa nyumbani kwake anakula mishikaki ya chatu" pamenivunja mbavu.. πŸ˜ƒπŸ˜„πŸ˜„πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜…πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…