Samsung A-series za 2019 naona kama zishaanza kuwa yeboyebo

reyzzap

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Posts
6,813
Reaction score
21,807
Nimekuwa mtumiaji wa Samsung A-series tangu za 2015,
hizi ni mid-range Samsung smartphone, na wamekuwa wakizibadilisha muonekano mwaka kwa mwaka (binafsi toleo la A-series la 2016 ndio bora kwangu mpaka sasa).

Samsung A-series na M-series za mwaka huu, ukiondoa A60, A80 na M40 yaani zote physical appearance ni almost zinafanana. Aliyeshika A10 ya 250,000 na aliyeshika A70 ya 850,000 kimuonekano hasa wa juu hamna tofauti, zote wanatumia water drop Notch display (angalia kale ka camera kalivyokaa pale juu).

Official wali discontinue J series (hutosikia J series tena zaidi ya J8 na ya mwisho kabisa kutolewa ni J4core ya 2018) ambazo zilikuwa low end na hazikuwa na soko kubwa nje ya Africa while A series (mid-range) zikauza sana.

Kuona hvyo mwaka huu ikabd waue J-series na wa extend A-series zitoke kwenye mid-range mpaka lower end ili waziuze kwa wingi maana watu walishakariri A-series ni bora, ndio labda ni bora ila wakajisahau ya kuwa uki introduce simu nyingi na ukaziuza kwa bei chee watu wanajenga mentality ile ile ya kuwa ni ovyo japo sio lazima iwe kweli, japo pia kuna ukweli.

Angalia A-series za 2016 zilivyokuwa nzuri kuanzia kwenye muonekano na perfomance. Kimuonekano hazikuwa tofauti na S6 au S7, na no wonder A9 pro-2016 iliuzwa sawa na S7 edge na mpaka leo A9 pro 2016 ina miaka zaidi ya mitatu lakini ni almost 400k na ushee, bei ambayo unapata A30 au A40 ya mwaka huu.

Kwahiyo zile zilikuwa chache, zikawa bora na zikauzika na kupendwa, na walioshindwa kununua zile wakanunua J-series. Samsung wanatoa models kulingana na hali za kiuchumi za wateja. S & Note series walilenga watu wenye kipato cha juu. A (alpha) & C-series watu wenye kipato cha kati na J (joy/junior) series watu wenye kipato cha chini.

Sababu walisha merge J-series ikaingia ndani ya A-series (kwaio hapa wamechanganya mid-range na low-end) kumbuka wamethitisha kimya kimya C-series maana hatuzioni sokoni , sasa waka wakaintroduce M-series feb ili ichukue nafasi ya C-series katika mid-range na pia iuzike kimataifa zaid maana tayari A-series zishaanza kuonekana si chochote japo wanadai M-series n mbadala wa J-series.

Ukiangalia na hili wanaelekea ku fail, M-series ni chache sana mtaani kulinganisha na A-series japo ni bora zaidi ya A-series na hata bei zipo juu. Kumbuka walikuwa na E (Elegant) series wakafai ndio wakaja na C-series.

Wakaja na Core/grand wakafail wakahamia kwenye J-series. Sasa J-series wameua na bila shaka hata C-series maana hazipo tena sokoni kuanzia 2017. A-series ndio hizo saa hizi ukiingia mtandaoni mfano A10 watumiaji wanaziuza kama njugu na hazina hata mwaka.

Sifa waliyobaki nayo ni Note na S-series. Hapa heshima bado ipo. Edge display ndio zinawapa point za utofautish kwenye muonekanoo. Siku wakijichanganya waka introduce edge display kwenye hizi series zao nyingine itakuwa wameamua wenyewe kuua soko la flagship zao wenyewe.

Kwa hiyi ukiangalia sio kama ni A-series zote ni sawa, kuna zilizosimama kama A80, na A90 na hata bei yake haishikiki, ila kitendo cha kuchanga simu za bei chee na bei ya juu kwenye toleo moja ndio inaonekana tatzo labda.

iPhone hili wameepuka kwa kutokubali kujaza matoleo mengi ya simu.

Mimi ni mpenzi wa Samsung na Nokia na sijawahi waza toka nje ya hapo, Nokia ndio karudi ila naona bado kama tulivyomzoea. Huyu Samsung japo ndio hivyo ila still flagship zake bado zinawasumbua sana ma giants wengine.

Sitaki kuzungumzia Tecno ambazo unatoka Kariakoo kununua Tecno Spark 3, unapanda daladala washatoa Spark 3 pro, hujalipa nauli washatoa Spark 3 Max, unafika nyumbani Spark 3 plus ishatoka, unafungua Box tayari Spark 3 Max pro, unaweka laini Spark 3 Grand asubuhi unaamka Spark 4 ishatangazwa. Hawa jamaa hawa wahurumii wateja wao.

Simu imetoka asubuhi inafika jioni tayari ni old model. Sasa hivi ukipita pale Aggrey na Likoma chini utakuta kumejaa mabox ya Tecno Spark,Tecno Spark, Tecno Spark.

Masahihisho na ukosoaji hayapingwi.

===



 
Halafu toka watengeneza simu waanze kutoa simu za notch display na water drop display imekuwa shida kutofautisha simu bila kutoa kava au kuangalia nyuma.

Longtime ilikuwa ukishika simu fasta mtu anajua umeshika nini unauza na sura kidogo.

Pongezi kwa Google Pixel naona toleo lao la Pixel 4 wameachana na notch hizo na water drop na pia S10.
 
1. A10 haina super amoled display.ina kioo cheupe kabisa.
2. Water drop ya A30 kuendelea ni semi circle, tofauti na A10 na A20 ambazo ni V shape.
3. A20 kuendelea zina camera mbili nyuma na nyingine tatu kabisa.

Hizo ni tofauti za haraka haraka ambazo mtu anaweza ziona. Labda ambazo zimeshazagaa mtaani ni A10 na A20 nazo huwezi kujilinganisha nazo na Infinix zenu.

Kimsingi hapa naona mdau wa Tecno akijaribu kujiweka sawa na watu wa super amoled.
 
Mkuu simu zinakwenda kwa matoleo na wasaidizi wake kila mwaka.

Samsung S10/Plus, Note 10 Plus ni water drop cameras na edge displays, matoleo andamizi camera zinakaa sehemu tofauti, A80 camera ina eject kwa juu.

Kwa hiyo usitegee kuchanganyana kwa vyovyote vile.
 
Samsung hata afanyeje kwa upande wangu series ya S yenye muonekano poa, Edge tamu ni S6 Edge, S6 Edge Plus, na S7. Juzi nimeshika S10 Plus, nimeichezea yaani sioni tofauti na J6 Plus yangu.

Ingekuwa maamuzi yangu hizi high end angetofautisha hizi za kawaida upande wa user interface. Simu software, namna una navigate kwa mfano android 9 ni sawa sawa mwenye simu ya laki 2 na ya mil 2. So boring.
 
Unachekesha!! Huwezi fananisha design ya S6 edge na S10+
 
Nilikuwa na kiherehere cha kununua A30 zilivyotoka tu hela ndefu. Ila laiti ningejua zingekuja kutoka nyingi hivi na kwa bei rahisi mara 10 ningenunua Tecno nitulie tu. Kiufupi inapoelekea kwa style hii Samsung wataipoteza brand yao kizembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…