Samsung: Hii kampuni inachofanya ni sawa kweli?

Samsung: Hii kampuni inachofanya ni sawa kweli?

Niliposema msidanganyike na vitu vidogo vidogo nimemaanisha kuwa hao apple wanatoa toleo jipya likiwa na vitu vipya vya kipuuzi sana Then wanauza kwa mamilioni kwa sababu kuna wapuuzi lazima watanunua kisa n apple.
Makampuni yote yako hivyo sasa hivi, hakuna kitu kipya
Angalia matoleo ya Tecno, Infinix
 
Hiyo ni sawa kwa wapinzani wa jadi,Samsung walipokuja na Galaxy AI nikajua tu lazima na Apple wapite nyayo za Samsung.....apple wanakimbizwa.
 
Hiyo ni sawa kwa wapinzani wa jadi,Samsung walipokuja na Galaxy AI nikajua tu lazima na Apple wapite nyayo za Samsung.....apple wanakimbizwa.
Hiyo ni trend ya smartphone industry kwa sasa, sio kwamba kaiga kwa Samsung. Aliyeanza kuleta hivi vitu ni Google kupitia Google Pixel. Apple na Samsung wote wamekuwa inspired na Google
 
Apple naona kama wamewekeza kwenye jina kwa mafanikio makubwa. Hata wakifuta kila kitu wakaweka kioo cha kujitazama ukichana nywele inawezekana wakauza na usishangae ukakutana na mtu ana kipara kanunua hicho kioo. Binafsi ni mteja wa android.
🤣🤣🤣🤣🤣Mbavu sina
 
View: https://x.com/SamsungMobileUS/status/1800233900389617979?t=VDdvhRoSeZ0LKEnI_RgKcw&s=19
Kampuni ya Kikorea "Samsung" imeleta features nyingi zinazowezeshwa na Artificial intelligence kwenye Samsung Galaxy S24 series na collection ya AI features kwenye S24 series Samsung akaamua kuiita "Galaxy AI"

Apple nao kupitia iOS 18 wameshirikiana na OpenAI kuleta AI features mbalimbali kwenye iPhone 15 Pro na 15 Pro Max. Apple yeye anaiita "Apple Intelligence".
Lakini cha ajabu kampuni ya Samsung kupitia ukurasa wake wa Twitter wa Marekani naona anapost statement za ku criticize Apple.
Mfano kwenye hii tweet ameandika "Adding "Apple" doesn't make it new or groundbreaking. Welcome to AI 🍎."

View: https://x.com/SamsungMobileUS/status/1800233900389617979?t=bg3lV_UzzgGSNa9q8_P2eQ&s=19

iOS 18 sasahivi imewapa uwezo iPhone users kuhamisha apps na kuziweka popote pale kwenye home screen, I mean hiki si kitu kipya kwa Android users kwa sababu hiki kitu kipo kwa miaka 14 sasa.
Samsung kupitia ukurasa wake wa Twitter Marekani wamepost kauli ya kinafiki, Post inasema "Moving my icons wherever I want since 2010 ... isn't that cool?"
Ni kama Samsung wanawacheka Apple hivi, kwa kuchelewa kuleta hiyo feature.

View: https://x.com/SamsungMobileUS/status/1800217378216890411?s=19

Hivi kumkandia mshindani wako kupitia mitandao ya kijamii ni sahihi au mimi ndo sijaelewa 🙄🙄

Si afadhali Samsung wanaandika huko x kwa mafumbo....Hivi unamjua Steve Jobs wewe...alikuwaga akiwa na Event ya kutambulisha bidhaa mpya za Apple anaweka big screen kubwa na watu kama 10,000 hivi alafu simu zote ambazo zinashindana na Apple kwa wakati huo anazianika kwenye big screen na kuanza kuzikosoa wazi wazi moja baada ya nyingine..na kwa style yake hiyo alifanikiwa kupoteza simu nyingi sana zilizokuwa Kileleni kama Blackberry, Motorola, SonyErickson ...na Baba yao Nokia....

Kwenye kukosoa Vifaa na teknolojia za kampuni nyingine steve jobs alikuwa ndyo Kiranja...na ilimsaidia sana

View: https://youtu.be/MnrJzXM7a6o?si=70WXtmW3qGBe5QcK
 
Kama Steve Jobs alikuwa anafanya hivyo kweli, basi naye alikuwa anakosea. At least kwa mtazamo wangu
 
Back
Top Bottom