Marjo Mlekwa
Member
- Jul 18, 2021
- 38
- 60
HIVI UNAJUA MAPENGO YA KINYWA CHA SANAA YANAWEZA KUZIBIKA KAMA TUKIAMUA?
'Licha ya jopo la madaktari kupambana Na changamoto za kinywa hiki, bado tatizo sugu la mapengo limeonekana kuwazidi nguvu, kinywa kinazidi kupata mapengo kila uchwao'
Leo nakukaribisha uone muundo halisi wa Kinywa hiki kilichoundwa na midomo ya mvuto, ulimi wa heshima na mate ya Umaarufu.
Kinaitwa kinywa cha Sanaa!!
Ndani ya kinywa hiki kuna ufizi ulioundwa Na sehemu kuu nne.
1: Kuburudisha
2: kuelimisha
3: kuhabarisha
4: kuhamasisha
Hiki ni kinywa cha heshima kilicho na kinachowatambulisha watu wengi wenye vipaji mbalimbali vya Sanaa.
Hiki ndio kinywa kinachopitisha chakula kwenye matumbo ya vijana wengi mtaani.
Mwaka fulani jopo la madaktari bingwa wa vinywa walikaa kutafakari namna gani yakupambana Na tatizo linalokumba kinywa hiki.
Tatizo la kutothaminiwa na kuheshimiwa licha ya kuwasaidia watu wengi kukidhi mahitaji yao ya njaa.
Maskini mpaka Leo sina uhakika kama madaktari walifanikiwa kutibu tatizo hilo.
Na ni siku nyingi zimepita tangu jopo hilo la madaktari wajadili suala hilo, Na hivi karibuni tatizo jingine linajitokeza kwenye kinywa cha Sanaa.
Tatizo la harufu mbaya ya dharau!
Ulimi wa heshima unaopatikana kinywani hauthaminiwi licha ya kuwa unatoa maneno matamu Na ya hamasa kwa jamii.
Mate ya Umaarufu Na midomo ya mvuto yamewazidi nguvu wenye kinywa na kusahau kabisa zile thamani za kazi nne ya ufizi wa kinywa hiki.
Hili nalo ni tatizo!
Likiwa bado halijaisha Leo hii kinywa kinakumbwa Na tatizo jingine la meno imara yanayounda kinywa kung'oka kila uchwao.
Jino lenye mvuto wa pekee kwenye kinywa Maarufu kama MFALME WA POP liling'oka mwaka 2009, mwezi wa 6 nakumbuka tarehe ilikuwa Ni 25.
Jopo la madaktari wa kinywa walidhani itakuwa ni kazi rahisi kuzibwa kwa pengo hilo kinywani.
lakini wapi!!
Mpaka Leo bado kinywa kina pengo la MFALME WA pop! MICHAEL JOSEPH JACKSON.
Inaelezwa kuwa tatizo hili la kupatikana kwa mapengo kinywani lilianza tangu kitambo.Watambuzi wa mambo watakumbuka miaka mingi iliyopita kinywa kulipoteza meno kadhaa kama vile jino la nguli wa mashairi Na Riwaya nchini uingereza WILIUM SHAKESPEARE, jino liling'oka nakuacha pengo mwaka 1616, mwezi wa 4 tarehe 23..
Unaweza kuona kuwa kumbe kinywa kilianza kupatwa Na shida hii ya mapengo yasiyozibika tangu Zama za kale sana.
Mwaka elfu 1 Mia 6 ni makarne kadhaa sasa yamepita!!
Lakini tatizo la mapengo bado halijapatiwa ufumbuzi,
Bado linakiandama kinywa!
Wanasema eti ukanda wa afrika mashariki kuliokotwa jino ambalo lilirandana Na lile la WILIUM SHAKESPARE, jino hilo liliitwa SHAABAN ROBERT.
Wataalamu walipoliweka kinywani kukabainika utofauti wa lugha utokao kwenye kinywa cha Sanaa.
SHAKESPARE jino lake lilileta ladha nzuri ya lugha ya kiingereza Na SHAABAN ROBERT alimudu vema kucheza Na Kiswahili.
Hivyo pengo la SHAKESPARE nchini uingereza bado limeendelea mpaka Leo.
Kinywa kiliendelea kukumbwa Na changamoto ya kung'oka meno.
Hata lile jino lililookotwa Afrika Mashariki nalo liling'oka.
Jino SHAABAN ROBERT Liling'oka tarehe 22 mwezi wa 6 mwaka 1962.
Pengo likabaki na sina hakika kama kuna jino limetosha kwenye pengo hili la BABA WA KISWAHILI.
Haikuishia hapo.
Kinywa cha sanaa kinazidi kung'oka meno yake!
Jino la wasanii wa HipHop kina Tupack, B.I.G Na wengine wengi tu.
Jino la kipaji cha pekee kutoka Tanzania lilioitwa ALBERT MANGWEIR nalo liling'oka mwaka 2012.
Pengo lake bado ni kubwa, lipo wazi mpaka leo.
Hakuna wakuliziba.
Tatizo bado limeendelea ambapo mwaka 2012 tena jino Jingine la kinywa likang'oka, jino hili liitwalo Hussein Ramadhaan au Maarufu kinywani kama SHARO MILLIONAIRE nakumbuka liliacha pengo usiku wa tarehe 26.
Bado kinywa kinaandamwa Na mapengo makubwa, licha ya vizazi vipya kuja Na teknolojia za kisasa za kutibu matatizo ya kinywa lakini bado tatizo la mapengo halijapata ufumbuzi kinywani.
Ona Pengo lile la STEVEN CHARLES KANUMBA bado Lina upana wake ambao kila jino linaloota halitoshi.
Ni dhahiri Kinywa sasa kimejaa mapengo ya meno imara!
Ingawa kila siku meno mapya yanaota lakini ni kweli kwamba Ladha ya kutafuna mifupa mitaamu Na migumu inazidi kupotea kinywani.
Kutahamaki!! kinywa kinapata pengo jingine.
Jino imara kwenye kinywa cha Sanaa linang'oka.
Jino hili Lina cheo Cha ufalme wa uchekeshaji Tanzania, AMRI ATHUMAN maarufu kama KING MAJUTO.
Kinywa kinapata pengo!!
Pengo hili ni muendelezo wa ubovu wa kinywa ambao unaendelea kuonekana kadiri siku zinavyokwenda.
Mapengo yanaongezeka licha ya meno mapya kuota lakini bado sehemu za mapengo tunaziona kwenye kinywa.
Masikini kinywa cha Sanaa!!
Ni yupi dokta sahihi wa kutibu matatizo yanayokiandama kinywa hiki.
NI KWELI HAYUPO DAKTARI HODARI?
Desturi ya Dunia ni watu kufa na wengine kuzaliwa, siamini kama vizazi vipya vinavyoongezeka kila siku iitwayo leo haina nguvu ya kuziba mapengo ya wakongwe waliochangamsha kinywa kwa ladha tofauti tofauti za vipaji vyao.
Kwa mataifa mengine yaliyoendelea angalau ukitazama uwiano wa vipaji vinavyokufa na vinavyoibuka walau utaona faraja ipo, maana kuna umakini katika kuwaandaa vijana tangu wangali wadogo sana.
Kwa nchi zetu zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara, hususani Tanzania bado tunadema dema katika kuwapika watoto tangu wakiwa wadogo, imeendelea ile kasumba ya kukumbatia mfumo wa elimu unaomlazimisha mtoto asomee kwa bidii vitu ambavyo hana muamko navyo kutokea ndani.
Ni ukweli kwamba tupo kwenye Dunia ambayo sanaa imekuwa msaada mkubwa kwa vijana kujiajiri na kuendesha maisha yao, haitakuwa kichekesho wala maajabu serikali zetu zikawekeza kwenye sanaa na ikibidi kuweka utaratibu utakampa chaguo mtoto afuate anachopenda tangu akiwa mdogo.
Ardhi imekinai miili ya wahandisi ambao walizaliwa waje kuwa madaktari na madaktari ambao walipewa zawadi ya kuigiza sinema.
Mbona wapo wasanii duniani wana pesa kuliko hata bajeti ya wizara kadhaa za serikali za nchi zetu kwa mwaka.
Nachelea kusema huenda kinywa ni desturi yake kung'oka meno kwahiyo hatupaswi kuchukulia ni tatizo lakini je! haya meno yanayoota yana nguvu ya kuvunja mifupa na kutupa ladha tamu walaji!?
Ushauri wangu kwa jopo la wataalamu wa kinywa cha Sanaa.
Nadhani badala ya kuhangaika kutafuta mbinu yakuzuia meno yasing'oke ni busara sasa kuhakikisha meno mapya yanasimamia misingi ya meno yanayong'oka, hapa pana wahusu wote wazazi kutambua ukuu wa watoto wao tangu wakiwa wadogo, watunga sera wawe makini katika upembuzi yakinifu wa njia sahihi za kuibua na kutunza vipaji vya watoto wetu.
Haya yakizingatiwa nina hakika italeta faraja na kutufuta machozi kwa kusahau meno yaliyong'oka.
Mwisho nasalia kwa kumuomba MUNGU abariki kinywa cha sanaa kiendelee kuwa kitambaa kinachofuta machozi ya vijana wengi kutoka kaya maskini, ambao bila ya vipaji vyao huenda familia zao hadi leo zingeendelea kuoga katika dimbwi la umaskini..

Upvote
10