Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Sanamu kubwa kuliko yote duniani ni lile la Yesu amani imshukie ambalo lipo juu ya mlima Corcovado pembezoni mwa jiji la Rio de janairo nchini Brazil.
Sanamu hilo limo ndani ya mbuga ya Tijuca na ni ubunifu wa kanisa katoliki la nchini humu.Lina ukubwa wa karibu futi 100 kwenda juu.Likiwa juu ya mlima huo karibu futi 2000 kutoka usawa wa bahari linalifanya sanamu hilo lionekane kirahisi na kila mkaazi na mtembezi wa jiji hilo kuu la Brazil.
Fikra za kujengwa sanamu hilo kubwa ili kila mtu alione zilianza mwaka 1850.Hata hivyo uamuzi rasmi wa kuanza ujenzi wake ulifikiwa mwaka 1921 na ujenzi wake kuanza mwaka uliofuatia,Mainjinia wa Brazil na Ufaransa walishirikiana mpaka ulipokamilika ujenzi wake.
Sanamu hilo lilimuonesha Yesu akiwa ameshika msalaba mkubwa mkono wake mmoja na dunia kwenye mkono wa pili.Pamoja na akili nyingi zilizotumika kufanikisha kazi hiyo lakiini iliishia kwa watu kulifanyia dhihaka kwamba Yesu ameshika mpira.
Baada ya utafiti mwengine kufanyika ya eneo jipya kujengwa karibu yake,sanamu nyengine yenye uzito wa tani 635 lilijengwa na kumalizika miaka 10 baadae hapo mwaka 1931 safari hii likimuonesha Yesu akiwa amekunjua mikono yake kama anayeamkiana au kukaribisha watu.
Mwaka 2007 juhudi kubwa zilifanyika ili kuliingiza sanamu hilo katika maajabu ya dunia. Mwanzoni watu waliweza kulifikia kwa kupanda vidaraja vyake vingi. Kwa sasa imekuwa rahisi kwa kutumia garimoshi na hata gari pamoja na ngazi za umeme,
Mwaka 2014 wakati wa kombe la dunia la mpira wa miguu lililofanyika nchini humo radi kubwa ililipiga sanamu hilo muda mfupi kabla kombe kuanza na kuharibu kichwa chake na mikono. Kwa haraka sana matengenezo yalifanyika na kulirudisha katika hali ya muonekano mzuri.
Tukio la mwaka huo lilikuwa ni kama mwanzo tu kwani mara kadhaa radi zmeliandama sanamu hilo kiasi kwamba kwa sasa limejengewa vifaa maalumu vya kuzuia radi. Pamoja na hivyo radi hazijakoma kulipiga sanamu hilo hasa maeneo ya kichwa.Tukio la karibuni ni lile la Februari 10 mwaka huu