Sanamu la Yesu halijachoka kupigwa na radi

Sanamu la Yesu halijachoka kupigwa na radi

Zile nyengine huwa zinapiga kikawaida.Hizi za hapa zinapiga kwa hasira kweli na huchagua muda watu wengi waone kama siku zile za kombe la dunia.Jee hupati ujumbe hapa

Ujumbe gani ulitaka wapate,mana hata huku kasulu radi zinapiga sana na zina ua kila mwaka ulitaka watu wa kasulu wapate ujumbe gani
 
Sanamu kubwa kuliko yote duniani ni lile la Yesu amani imshukie ambalo lipo juu ya mlima Corcovado pembezoni mwa jiji la Rio de janairo nchini Brazil.

Sanamu hilo limo ndani ya mbuga ya Tijuca na ni ubunifu wa kanisa katoliki la nchini humu.Lina ukubwa wa karibu futi 100 kwenda juu.Likiwa juu ya mlima huo karibu futi 2000 kutoka usawa wa bahari linalifanya sanamu hilo lionekane kirahisi na kila mkaazi na mtembezi wa jiji hilo kuu la Brazil.

Fikra za kujengwa sanamu hilo kubwa ili kila mtu alione zilianza mwaka 1850.Hata hivyo uamuzi rasmi wa kuanza ujenzi wake ulifikiwa mwaka 1921 na ujenzi wake kuanza mwaka uliofuatia,Mainjinia wa Brazil na Ufaransa walishirikiana mpaka ulipokamilika ujenzi wake.

Sanamu hilo lilimuonesha Yesu akiwa ameshika msalaba mkubwa mkono wake mmoja na dunia kwenye mkono wa pili.Pamoja na akili nyingi zilizotumika kufanikisha kazi hiyo lakiini iliishia kwa watu kulifanyia dhihaka kwamba Yesu ameshika mpira.

Baada ya utafiti mwengine kufanyika ya eneo jipya kujengwa karibu yake,sanamu nyengine yenye uzito wa tani 635 lilijengwa na kumalizika miaka 10 baadae hapo mwaka 1931 safari hii likimuonesha Yesu akiwa amekunjua mikono yake kama anayeamkiana au kukaribisha watu.

Mwaka 2007 juhudi kubwa zilifanyika ili kuliingiza sanamu hilo katika maajabu ya dunia. Mwanzoni watu waliweza kulifikia kwa kupanda vidaraja vyake vingi. Kwa sasa imekuwa rahisi kwa kutumia garimoshi na hata gari pamoja na ngazi za umeme,

Mwaka 2014 wakati wa kombe la dunia la mpira wa miguu lililofanyika nchini humo radi kubwa ililipiga sanamu hilo muda mfupi kabla kombe kuanza na kuharibu kichwa chake na mikono. Kwa haraka sana matengenezo yalifanyika na kulirudisha katika hali ya muonekano mzuri.

Tukio la mwaka huo lilikuwa ni kama mwanzo tu kwani mara kadhaa radi zmeliandama sanamu hilo kiasi kwamba kwa sasa limejengewa vifaa maalumu vya kuzuia radi. Pamoja na hivyo radi hazijakoma kulipiga sanamu hilo hasa maeneo ya kichwa.Tukio la karibuni ni lile la Februari 10 mwaka huu

67619375-11743733-image-a-7_1676262417790.jpg
Utakuwa ulifeli physics tu. Radi inafata the highest point. Sasa kwani hilo sanamu umeambiwa ndio Yesu? Mnafiq mkubwa wewe.
 
Ahsante kwa taarifa na inasikitisha sana...
 
Kula idi,acha makasiriko
Lugha in involve kila siku na biblia kila siku zinachapwa ili ziendana na mabadiliko ya lugha ili iwe rahisi kufikisha ujumbe kwa wasomaji. Sijui kwako hiyo verse inatengeneza hisia gani hata ukaamua kuileta hapa kama hoja.
Na zaidi hiyo verse imekuwepo karne nyingi kabla ya hata Yesu hajazaliwa ulivyo kichwa cheupe unahisi wakristo wamekopi kutoka kwenye kurani ambayo imetungwa juzi hapa tu.
May God have on you.
 
Kwa imani ya wakristo,yesu ni Mungu,
Kwa hiyo yesu ana amrisha radi ilipige sanamu lake?
 
Sanamu LA yesu[emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23] walimuona wapi mpk wakapata physical features zake???
 
Kula idi,acha makasiriko
Hii hapa verse.
New international version. :-What will you do on the day of your appointed festivals, on the feast days of the LORD?

Hii kwa New living translation.

New Living Translation
What then will you do on festival days? How will you observe the LORD’s festivals?.

Hii kwa berean:-

Berean Standard Bible
What will you do on the appointed day, on the day of the LORD’s feast
Ni wapi umeona kuna neno iddi?.

Kiswahili asili yake pwani so wachapa biblia katika lugha ya kiswahili wakaamua kubadili neno (festival) na kuweka neno (idd) ili kuweka urahisi kwa msomaji.
Hayo mengine ni ujinga wako.
 
Unataka kusema YESU anapigana na radi ?
Sio anapigana.Bali anapigwa kila siku mpaka anavunjika kichwa na vidole.Kwa heshima kubwa ya Yesu bora ateremshwe pale.Vyenginevyo waBrazili watamdharau sana.
 
Hii hapa verse.
New international version. :-What will you do on the day of your appointed festivals, on the feast days of the LORD?

Hii kwa New living translation.

New Living Translation
What then will you do on festival days? How will you observe the LORD’s festivals?.

Hii kwa berean:-

Berean Standard Bible
What will you do on the appointed day, on the day of the LORD’s feast
Ni wapi umeona kuna neno iddi?.

Kiswahili asili yake pwani so wachapa biblia katika lugha ya kiswahili wakaamua kubadili neno (festival) na kuweka neno (idd) ili kuweka urahisi kwa msomaji.
Hayo mengine ni ujinga wako.
Kwa Nini neno Pasaka walipate?

Neno idi Kwa Nini wakose?
 
Kwa Nini neno Pasaka walipate?

Neno idi Kwa Nini wakose?
Uwa mnafikiri kwa kutumia nini hasa?
Okay!! Mimi sina uwezo wa kushughulika na tatizo ulilonalo kichwani mwako. Dhumni langu ni kukuonyesha kuwa " fikiri yako ina makosa" na sina uwezo wa kukutoa kwenye ilo dimbwi la ujinga ulilomo.
SHAURI YAKO.
 
Jengo lolote refu lazima lipigwe radi. Sio supernatural effect na kwanza hili sanamu halina sura ya Yesu ni just nadharia.
🤷‍♂️🤷‍♂️ si kila jengo refu lazima lipigwe na radi pia
 
Back
Top Bottom