Sanamu ya Nyerere kutofanana; Je sanamu ya Christiano Ronaldo inafanana na mwenyewe

Sanamu ya Nyerere kutofanana; Je sanamu ya Christiano Ronaldo inafanana na mwenyewe

Bora wabebe lile lisanamu lililo Nyerere Square Dodoma lipelekwe huko Addis Ababa likabadilishwe.
 
Usijifanyie sanamu ya kichonga mfano wa kitu chochote kilichopo duniani ama mbinguni ama kuzimu chini ya bahari,usivisujudie wala kuvitumikia,kwa kuwa mimi Bwana Mungu wako ni Mungu mwenye wivu,nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu
 
Kwa maendeleo ya teknolojia na matumizi ya 3D printing, ilitakiwa sanamu zifanane zaidi na wahusika wakati huu kuliko zile za awali.
 
Muhimu tujifunze tukishaambiwa hii ni sanamu ya fulani na inafanana fanana nae basi tukubali maisha yaendelee, sometime tunajiumiza vichwa kwa vitu vidogo sana.

Sanamu ikishaitwa ya Nyerere, itabaki kuwa ya Nyerere tu, hawezi kujitokeza anyone akasema hiyo sanamu ni yangu sio ya Nyerere, sasa sijui huwa malumbano ya nini.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
😆 😆 😆 😆
 
Mtu kalipiwa nauli na posho ya kwenda huko halafu awagomee kweli kwamba sanamu siyo la baba yake? Mbona miaka kadhaa nyuma pale bustanini jijini Mwanza kuna lisanamu fulani hivi liliwekwa na kudaiwa ni la Nyerere na wananchi walipiga sana kelele kwamba halifanani nae na nadhani baadae likabadilishwa?
Basi na hii itabadilishwa tu
 
Haiwezekani SANAMU lifanane typical na kitu HALISIA binadamu anachonga mfanano iwe MBUZI, BATA, NJIWA , KASUKU ,NG'OMBE hata binadamu.

Hata ndugu wa kuzaliwa na binadamu tunarahisisha tu, hwa wamefanana lkn kiuhalisia tumerahisisha tu.
Nakubaliana na wewe ile ni sanamu ya Nyerere. Ila wangesema ni mwili wa Nyerere hapo ingekuwa ni issue ya ku contest
 
Haya madai kwamba sanamu hilo limetengenezwa na kampuni iitwayo Epitome Architects Limited ambayo mkurugenzi wake mkuu ni Nuru Nyerere-Inyangete ambaye ni mtoto wa hayati Joseph Nyerere ni ya kweli? Basi pasi na shaka ndiyo maana Madaraka Nyerere ili kulinda huo ulaji kwa familia yake kupitia tenda waliyopewa, analazimisha kwa nguvu zote kwamba sura ya sanamu ni ya baba yake huku asilimia kubwa ya watanzania tukiona kuwa sura ya sanamu siyo ya baba wa taifa.
 
Watanzania tuna haki sawa na huyo asemaye yule ni baba yake, kama anaamini ni baba yake tumuite basi baba Makongoro ama Andrew watanzania kwa pamoja twamuita baba wa taifa iweje sura yake ikosewe ye awe wa kutujibia kama ni hiyo asemayo angetujibia huo utofauti mama yetu mama Nyerere na si mtoto
 
Haya madai kwamba sanamu hilo limetengenezwa na kampuni iitwayo Epitome Architects Limited ambayo mkurugenzi wake mkuu ni Nuru Nyerere-Inyangete ambaye ni mtoto wa hayati Joseph Nyerere ni ya kweli? Basi pasi na shaka ndiyo maana Madaraka Nyerere ili kulinda huo ulaji kwa familia yake kupitia tenda waliyopewa, analazimisha kwa nguvu zote kwamba sura ya sanamu ni ya baba yake huku asilimia kubwa ya watanzania tukiona kuwa sura ya sanamu siyo ya baba wa taifa.
Mradi wa sanamu ya J K Nyerere ulitekelezwa na Kampuni ya SAMCRO ya nchini Afrika Kusini chini ya usimamizi wa SADC na Tanzania na uĺigharimu takriban Dola za Marekani 267,992.60 ambazo ni sawa na takriban Shilingi 615,000,000 ambazo zilitolewa na SADC na gharama za usimamizi kutolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Back
Top Bottom