Sanchword abadili dini sasa kuitwa Surraiya Evarist Rimoy

Sanchword abadili dini sasa kuitwa Surraiya Evarist Rimoy

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
1587981208001.png

Mrembo maarufu mtandaoni Sanchword amebadili dini na kuwa muislam rasmi na kuitwa Surraiya Evarist Rimoy. Sanchi binti wa kichaga mwenye shepu matata amekuwa akifunga ramadhani wakati bado hajaingia kwenye uislam.

sanchiworld said:
ALHAMDULLILAH moyo wangu una amani kupita nitakavyoweza kuelezea na ALLAH shahidi 😭 It’s official my spirit is where it truly belongs...

Najivunia kufanya shahada yangu jana.. 24/04 Call me SURRAIYA EVARIST RIMOY.

Nimekua nikifunga Ramadan tatu mfululizo just because i love Islam but this one is very special, this is my first Ramadan as a Muslimah 🙏🏽🙏🏽 Alhamdullilah kwa hili na mengine mazuri yajayo INSHA’ALLAH.

Nawatakieni waislamu wote mfungo mwema wa mwezi mtukufu.
Wabillahi Taufiq Walhidayah, Wassalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh. 🤲🏽❤

Alhamdulillah lathee bi ni’matihi tatimmus saalihaat 🤲🏽 Kwa hakika ALLAH humuongoa amtakaye na kwa Muda atakaoupenda nakwa hakika amenichagua mimi 😭 Nawashukuru Sanaa kwa jumbe zenu nzuri mno walah sikutegemea 😭 JAZAK ALLAH KHAIR kwa wote mlionipongeza nakunitakia kheri 🙏🏽 Allah awalipie na apokee funga zenu Insha’Allah awaepushe na shari zote na hili gonjwa baya la Corona nyie pamoja na familia zenu. 🤲🏽 Nimepokea kwa dhati ushauri na maoni yenu hata mlionitumia DM nawashukuru sana nyingi nimeona na bado naendelea kusoma.

Hii ni hatua kubwa sana kwangu na inawezekana kila kitu kisiwe sawa kwa asilimia mia lakini taratibu InshaAllah. I will do my best my Brothers and Sisters na ndio malengo na dhamira yangu kufuata kila kitu kama dini yangu inavyonitaka naamini Allah aliyenichagua ataniongoza kwenye hili.

My beautiful Jilbab from: @stara_and_beauty

Na sote tuseme: Subhan’Allah, walHamdulilah, wa La illaha ilAllahu, waAllahu Akbar, wa la Hawla wa la quwwata illa billah.
1587981021110.png
1587981053772.png


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom