Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Makonda na genge lake wanatengeneza njia ya kuiba pesa za huo mradi wa jezi.View attachment 3673376View attachment 3673377
Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited imesema inakusudia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kauli ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda aliyoitoa hivi karibuni kuhusu jezi mpya za Taifa Stars.
Katika taarifa iliyotolewa leo Septemba 18, 2026, Kampuni hiyo imesema imesikitishwa na kauli iliyotolewa na Waziri Makonda Septemba 16, 2026 kupitia ukurasa wake wa Instagram iliyosomeka “
Hii sio jezi ya Taifa Stars, Taifa Stars kwa ubora wake hatuwezi kuwa na jezi za kiwango chini hivi, acheni kutumia picha za Naibu wangu huku Ofisi yangu haina taarifa”Kufuatia kauli hiyo, taarifa ya Sandaland leo imeeleza kuwa Kampuni hiyo ina mkataba halali na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa kutengeneza na kusambaza jezi za Timu za Taifa, ikieleza kuwa jezi hizo zimewahi kutumika katika mashindano mbalimbali ya timu za Taifa za Wanaume na Wanawake.
“Kauli hiyo iliyozua taharuki na sintofahamu mpaka sasa imekwishasababisha madhara makubwa sana ya kihadhi na kiuchumi”
Aliyemteua alitumia vigezo gani kumpa hiyo nafasi?Paul Makonda hajawahi kuwa na akili
Hakika Mkuu hili ndo na mie nimeliona pia.Hakuna maelewano kati ya waziri,naibu wake na TFF.
wote makambare.
Makonda atavinyoosha vyama vya michezo! Madudu ya hivi vyama ndiyo mkwamo wa michezo hapa nchini!Hili sakata si bure uenda kuna upigaji huko na kuna mtu anatafutwa hapa kama si karia basi Mwana FA
Inaonekana TFF inawasiliana sana na naibu waziri kuliko waziri
Bora iwe mwendo wa mahakama!Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited imetangaza nia ya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, kufuatia kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii iliyoponda ubora na uhalali wa jezi mpya za timu ya taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars).
Sakata hili limeibuka kufuatia taarifa iliyotolewa leo, Septemba 18, 2026, na kampuni hiyo nchini Tanzania, ikijibu ujumbe wa Waziri Makonda uliowekwa Septemba 16, 2026 kwenye ukurasa wake wa Instagram unaosema:
"Hii sio jezi ya Taifa Stars, Taifa Stars kwa ubora wake hatuwezi kuwa na jezi za kiwango chini hivi, acheni kutumia picha za Naibu wangu huku Ofisi yangu haina taarifa."
Sandaland imeeleza kuwa imechukua hatua hiyo kwa sababu kauli ya Waziri imesababisha sintofahamu na kuiletea kampuni madhara makubwa, ikifafanua kupitia taarifa yao kuwa:
"Kauli hiyo iliyozua taharuki na sintofahamu mpaka sasa imekwishasababisha madhara makubwa sana ya kihadhi na kiuchumi."
Wamesisitiza kuwa wana mkataba halali na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa kutengeneza na kusambaza jezi hizo ambazo tayari zimeshatumika katika mashindano mbalimbali ya timu za taifa za wanaume na wanawake.
View attachment 3673373View attachment 3673369
Pia soma: Sandaland Kuiburuza Mahakamani Wizara ya Michezo Kuhusu Jezi za Taifa Stars