Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 7,748
- 10,288
Uongozi wa Kampuni ya Sandaland Fashion Wear limited unatarajia kuzungumza na Waandishi wa Habari kesho September 22 2026 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam kuanzia saa tano kamili asubuhi.
Hata hivyo kupitia taarifa yake kwa Umma, Kampuni hiyo ambayo ndiyo yenye tenda ya jezi za Timu ya Taifa Stars, haijaeleza hasa ni nini inachokwenda kukisema mbele ya Waandishi wa habari hiyo kesho ikiwa ni siku tatu tangu ieleze kuwa inakusudia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kauli ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo aliyoitoa kuhusu jezi za Taifa Stars.
Mkutano huu na Waandishi unakwenda kufanyika ikiwa ni siku tatu tangu Wizara hiyo kufafanua rasmi kuwa Waziri Paul Makonda hatambui matangazo ya jezi za Timu ya Taifa kutokana na mchakato wa kuzibadilisha jezi hizo kutoshirikisha Wizara hiyo licha ya maelekezo aliyoyatoa Mwezi February 2026.