Roma hakuna utakatifu wowote,hilo sanduku litakuwa patakatifuInawezekana likawa Rome.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Roma hakuna utakatifu wowote,hilo sanduku litakuwa patakatifuInawezekana likawa Rome.
Hi hapa sio niliyoiona siku za nyuma lakini inafanana in details. Ile ni ndefu kidogo nafikiri niliiona kwenye documentaries za dstv, labda.Mimi pia nimeona documentary kama hiyo. Inasemekana liko Ethiopia kwenye kanisa moja dogo la kale. Pembeni yake Haile Sellasie alijenga kanisa lingine kubwa. Anayeingia kwenye chumba lilipo hilo sanduku ni mtu mmoja maalum. Akishachaguliwa mtu wa kuingia kwenye hicho chumba huwa haruhusiwi tena kutoka hekaluni kwenda uraiani mpaka anakufa, na pia haruhusiwi kuongelea details za hilo sanduku. Mtu mwingine atachaguliwa pale anapofariki huyo anayelitunza au anayelitunza akiwa hawezi tena kiafya. Watu wote waliokwisha fanya hiyo kazi hupata matatizo ya macho kutoona vizuri mara baada ya kuanza hiyo kazi.
Ngoja niitafute hiyo documentary niitazame tena, very interesting. I will share the link or upload it kwa jinsi nitakavyoipata.
Hapa kuna interesting story (ya 2021, sio zamani) kuhusu waethiopia wanavyopigana kulilinda hili sanduku SOMA HAPA
Ukweli ni upi?Si kweli
Kwa sehemu uko sahihi, lakini hoja yangu iko hapa kama wafilisiti waliweza kulichukua na likaweza kuwaua kwa maana kwamba bado lilikuwa na utukufu wa Mungu na kwamba amri ya kugushwa na wana wa lawi ilikuwa bado inafanya kazi ndio maana liliendelea kuwaua wafilisiti.mkuu ipo hivi israel waalipokuwa wanaasi MUNGU alikuwa anawaacha wanapigwa , na wapagani wanalibeba sanduku hawadhuriki
soma 1 SAMWELI KUANZIA SURA YA 2 LILIWAHI KUCHUKULIWA NA WAFILIST WAKALIPELEKA KWA mungu dagoni, baadae liliwaua wakiarirudisha
uzushi wa ROMAN HUOSanduku la agano ni kivuli tu juu ya Bikira Maria na nafikiri unajua Bikira Maria alipo.
Huu ni mfano wa sanduku la agano ambalo wana wa Israel waliambiwa watengeneze na Mussa wakiwa nyikani wakitoka Egypt (Misri) wakielekea promised land (Nchi ya ahadi). Sanduku hilo lilikuwa ni kama box la mbao lililotengenezwa na aina moja ya mbao inayoitwa (acacia wood) iliyofunikwa na dhahabu. Lilikuwa la urefu wa 1.15 metres, upana wa 0.7 metres na kimo cha 0.7 metres.
Ilikuwa inabebwa na mishikio miwili mirefu ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa mbao hiyo ya acasia ambazo pia zilikuwa zimefunikwa na dhahabu. Juu ya sanduku kuliwekwa makerubi wawili waliokuwa wamegeukiana mabawa yao yakiwa yamegusana. Uwepo wa Mungu haukuwepo ndani ya sanduku bali ulikuwa juu yake katikati ya hao makerubi.
Uwepo wa Mungu juu ya sanduku hilo ulikuwa kama nuru. Kuhani mkuu alipaswa kufunika macho asiione nuru hiyo ("hakuna mwanadamu anionaye na akaishi" Kutoka 33 : 20) kila alipokuwa akiingia lilipokuwa sanduku ambapo ni patakatifu pa patakatifu.
Hapa ndipo ambapo Mungu alipokuwa akiionana na Musa. Sanduku hili lilikuwa likibebwa na wana wa Walawi pekeyake hakuna mwingine aliyeruhusiwa kulishika, yeyote aliyedhubutu kulishika pasiporuhusiwa alikufa papohapo. Hao makerubi wawili wanawakilisha utukufu wa Mungu. Ndani ya sanduku hili kulikuwa na:
Sanduku hilo lilikuwa linakaa patakatifu pa patakatifu, chumba cha ndani kabisa katika hema la kukutania. Aliyekuwa anaruhusiwa kuingia mahala hapo lilipokuwa sanduku hilo ni kuhani mkuu na alikuwa anaruhusiwa kuingia mara moja kwa mwaka. Kabla ya Kuhani mkuu kuingia patakatifu pa patakatifu alikuwa ni lazima aingie na damu ya mwana kondoo kwa niaba ya dhambi zake yeye mwenyewe na dhambi za wana wa Israel.
- Mawe mawili yaliyokuwa yameandikwa amri kumi za Mungu
- Fimbo ya Aron iliyoota mauwa
- Chombo cha dhahabu kilichokuwa na manna waliyokula wana wa Israel nyikani
View attachment 1760924
Sanduku la agano lilikuwa ndani ya hekalu lililojengwa na Solomon mpaka hekalu hilo lilipokujwa kuvunjwa mikononi mwa utawala wa Babylon ukioongozwa na Nebuchadnezzar. Kilichotokea kwa sanduku hilo hakijulikani ingawa haiwezekani kuwa lilichukuliwa na majeshi ya Babylon kama vilivyochukuliwa vyombo vingine vya hekalu kwasababu katika list ya vitu walivyovichukua sanduku la agano halikutajwa.
Halitajwi kati ya vyombo vilivyopelekwa Babiloni hekalu lilipohabiriwa mwaka wa 607 K.K. wala halitajwi kati ya vyombo vilivyorudishwa Yerusalemu baadaye.—2 Wafalme 25:13-17; Ezra 1:7-11
Kulingana na baadhi ya vyanzo vya habari inasemekana kuwa mfalme Josiah, mmojawapo wa wafalme wa mwisho kutawala enzi za hekalu la kwanza, kutokana na unabii uliokuwa umetolewa alijua kuwa Jerusalem itavamiwa na Babylon, akalificha sanduku la agano.
Alipolificha sanduku imekuwa kitendawili. Chanzo kingine cha habari kinasema kuwa mfalme Solomon alionyeshwa kuwa Hekalu litakujwa kuvunjwa na majeshi ya Babylon, kwahiyo akaandaa pango karibu na bahari ya shamu (dead sea) ambapo Josiah akaja kulificha sanduku.
Na pia inasemekana nabii Yeremia (Jeremiah) alilificha sanduku chini ya Hekalu lililojengwa na Solomon.
HEKALU LA MBINGUNI
Halipo Rome wala kwa Waisrael tena. Nabii mkubwa Elia ndio alilificha chini ya ardhi na sio Israel na atakuja kuitoa wakati wa mwisho.Inawezekana likawa Rome.
Mostly chini ya ardhi ya Ethiopia au IraqSasa litakuwa lipo wapi?[emoji848][emoji848][emoji848].
Kupitia Malkia wa Sheba na kanisa kongwe la Orthodoxlilifikaje ethiopia? kuna connection gani kati ya utawala wa Babylon na wa-ethiopia ? yawezekana hawa wa-ethiopia ndiyo wakawa wana halisi wa Israel na wengi wao walikuwa utumwani Misri
Mawasli ni mengi....
Kuna Documentary niliangalia ya BBC/aljazera sina uhakika,wanasema lipo Ethiopia,kuna hekalu Fulani limewekwa huko ndani na huko anayeruhusiwa kuliona na kulilinda ni mtu mmoja tu na Mara nyingi hatoki nje.
Nje ya Hekalu hilo lina ulinzi mkali sana na hata mwandishi mwenyewe kwanza ilibidi apate ruhusa ya kufika huko na hata alipofika aliongea na mtu mmoja tu aliyekuwa nje ndio akamweleza hayo yite na wala hakuruhusiwa kusogea karibu na uzio wa Hekalu.