Sanduku la Agano liko wapi?

Sanduku la Agano liko wapi?

Huu ni mfano wa sanduku la agano ambalo wana wa Israel waliambiwa watengeneze na Mussa wakiwa nyikani wakitoka Egypt (Misri) wakielekea promised land (Nchi ya ahadi). Sanduku hilo lilikuwa ni kama box la mbao lililotengenezwa na aina moja ya mbao inayoitwa (acacia wood) iliyofunikwa na dhahabu. Lilikuwa la urefu wa 1.15 metres, upana wa 0.7 metres na kimo cha 0.7 metres.

Ilikuwa inabebwa na mishikio miwili mirefu ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa mbao hiyo ya acasia ambazo pia zilikuwa zimefunikwa na dhahabu. Juu ya sanduku kuliwekwa makerubi wawili waliokuwa wamegeukiana mabawa yao yakiwa yamegusana. Uwepo wa Mungu haukuwepo ndani ya sanduku bali ulikuwa juu yake katikati ya hao makerubi.

Uwepo wa Mungu juu ya sanduku hilo ulikuwa kama nuru. Kuhani mkuu alipaswa kufunika macho asiione nuru hiyo ("hakuna mwanadamu anionaye na akaishi" Kutoka 33 : 20) kila alipokuwa akiingia lilipokuwa sanduku ambapo ni patakatifu pa patakatifu.


Hapa ndipo ambapo Mungu alipokuwa akiionana na Musa. Sanduku hili lilikuwa likibebwa na wana wa Walawi pekeyake hakuna mwingine aliyeruhusiwa kulishika, yeyote aliyedhubutu kulishika pasiporuhusiwa alikufa papohapo. Hao makerubi wawili wanawakilisha utukufu wa Mungu. Ndani ya sanduku hili kulikuwa na:
  • Mawe mawili yaliyokuwa yameandikwa amri kumi za Mungu
  • Fimbo ya Aron iliyoota mauwa
  • Chombo cha dhahabu kilichokuwa na manna waliyokula wana wa Israel nyikani
Sanduku hilo lilikuwa linakaa patakatifu pa patakatifu, chumba cha ndani kabisa katika hema la kukutania. Aliyekuwa anaruhusiwa kuingia mahala hapo lilipokuwa sanduku hilo ni kuhani mkuu na alikuwa anaruhusiwa kuingia mara moja kwa mwaka. Kabla ya Kuhani mkuu kuingia patakatifu pa patakatifu alikuwa ni lazima aingie na damu ya mwana kondoo kwa niaba ya dhambi zake yeye mwenyewe na dhambi za wana wa Israel.

View attachment 1760924

Sanduku la agano lilikuwa ndani ya hekalu lililojengwa na Solomon mpaka hekalu hilo lilipokujwa kuvunjwa mikononi mwa utawala wa Babylon ukioongozwa na Nebuchadnezzar. Kilichotokea kwa sanduku hilo hakijulikani ingawa haiwezekani kuwa lilichukuliwa na majeshi ya Babylon kama vilivyochukuliwa vyombo vingine vya hekalu kwasababu katika list ya vitu walivyovichukua sanduku la agano halikutajwa.

Halitajwi kati ya vyombo vilivyopelekwa Babiloni hekalu lilipohabiriwa mwaka wa 607 K.K. wala halitajwi kati ya vyombo vilivyorudishwa Yerusalemu baadaye.—2 Wafalme 25:13-17; Ezra 1:7-11

Kulingana na baadhi ya vyanzo vya habari inasemekana kuwa mfalme Josiah, mmojawapo wa wafalme wa mwisho kutawala enzi za hekalu la kwanza, kutokana na unabii uliokuwa umetolewa alijua kuwa Jerusalem itavamiwa na Babylon, akalificha sanduku la agano.

Alipolificha sanduku imekuwa kitendawili. Chanzo kingine cha habari kinasema kuwa mfalme Solomon alionyeshwa kuwa Hekalu litakujwa kuvunjwa na majeshi ya Babylon, kwahiyo akaandaa pango karibu na bahari ya shamu (dead sea) ambapo Josiah akaja kulificha sanduku.

Na pia inasemekana nabii Yeremia (Jeremiah) alilificha sanduku chini ya Hekalu lililojengwa na Solomon.

HEKALU LA MBINGUNI


Liko ugweno kifula. Alileta mjerumani mmoja anaitwa fucs
 
lililokua Makka sio hili la agano ni lile la malaika jibril alilompatia Mtume.. na lilionekana mwaka 2015 wakati wa upanuzi wa msikiti ndipo viongozi wa kanisa la orthodox wakalifuata kwa escot ya meli za Mrusi mpaka kwenye Bara barafu la antactica.
Du,hilo la malaika jibril ungelianzishia uzi wake hapa tunazungumzia sandusky la agano
 
Wakati wa uhai wa Yesu, hekalu takatifu katika Yerusalemu lilikuwa ndilo nguzo muhimu katika maisha ya kidini ya Kiyahudi. Hekalu ilikuwa mahali ambapo dhabihu za wanyama zilikuwa zinafanyiwa na ibada kwa mujibu wa sheria ya Musa iliyofuatwa kwa uaminifu. Waebrania 9: 1-9 inatuambia kwamba katika hekalu pazia ilitenganisha pahali takatifu zaidi ya patakatifu – mahali ambapo uwepo wa mungu uishi ulimwenguni- kutoka kwa mahali pengine Hekaluni ambapo watu waliishi. Hii iliashiria kuwa binadamu alitenganishwa kutoka Mungu na dhambi (Isaya 59: 1-2). Ni kuhani mkuu tu aliyeruhusiwa kupita zaidi ya hii pazia mara moja kila mwaka (Kutoka 30:10, Waebrania 9: 7) aingie katika uwepo wa Mungu kwa ajili ya waisraeli wote na kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zao (Mambo ya Walawi 16).

Hekalu la Sulemani lilikuwa dhiraa 30 kuelekea juu (1 Wafalme 6: 2), lakini Herode alikuwa amezidisha urefu hadi dhiraa 40, kulingana na maandiko ya Josephus,mhisitoria Myahudi wa karne ya kwanza. Hakuna uhakika kwa kipimo halisi cha dhiraa moja, lakini ni salama kudhani kwamba pazia hili lilikuwa mahali fulani karibu futi 60 juu. Josephus pia anatuambia kwamba pazia hili lilikuwa na upana wa inchi nne na kwamba farasi hata wafungwe kwa kila upande hawangeweza kuirarua dhiraa hii . Kitabu cha Kutoka kinafundisha kwamba pazia hii pana iliundwa kwa mtindo kutoka samawati( buluu), zambarau, na nyekundu, na kitani kizuri cha kusokotwa.

Ukubwa na unene wa pazia unafanya matukio yanayotokea wakati wa kifo cha Yesu juu ya msalaba kuwa wa maana sana. "Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka."(Mathayo 27: 50-51a).

Hivyo, je,tunafanya nini kwa hili? Ni umuhimu gani dhiraa hii ilyopasuka inayo kwetu siku hizi? Zaidi ya yote, kuraruriwa kwa dhiraa wakati wa kifo cha Yesu kuliashiria kidrama kwamba kafara yake, kumwaga damu yake mwenyewe,kulikuwa upatanisho wa kutosha kwa ajili ya dhambi.Kuliashiria kwamba sasa njia ya kuingia Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa wazi kwa watu wote, kwa wakati wote, Wayahudi na Mataifa.

Wakati Yesu alikufa, dhiraa iliraruka, na Mungu akatoka mahali pale kwamba kamwe hangeishi tenai katika hekalu zilizojengwa na binadamu (Matendo 17:24). Mungu alikuwa amemalizana na hekalu hilo na mfumo wake wa kidini, na hekalu na Yerusalemu ziliachwa "zikiuzunika kwa ukiwa" (kuharibiwa na Warumi) katika mwaka 70 A.D., tu kama Yesu alitabiri katika Luka 13:35. Bora tu Hekalu lilisimama, liliashiria kuendelea kwa Agano la Kale. Waebrania 9: 8-9 inarejelea umri uliokuwa unapita mara tu agano jipya liliimarishwa (Waebrania 8:13

Suala la sanduku la agano kwa kweli kwamba limefichwa wapi ni tata,lakini kuna umuhimu na ulazima kwamba tusiwe nalo leo maana kwa kule kufa kwa Yesu msalabani na pazia lililokuwa linapatenganisha patakatifu na patakatifu pa patakatifu(ambapo kimsingi ndipo maskani ya sanduku la agano)kulifanya mwisho wa taratibu za kidini na kwa kuanzia hapo Mungu anakaa ndani yetu na si kwenye maskani maalum tu.

Sasa basi sanduku hilo lingekuwepo hata leo watu wangeshindwa kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli na yumkini wengine wangeabudu sanduku hilo.
 
Kupitia Malkia wa Sheba na kanisa kongwe la Orthodox
Jaman malkia wa sheba alienda Israeli wakati wa mfalme Suleiman na sanduku liliendelea kuwapo Israel miaka mingi mbele mpaka utawala wa mfalme Yosia mpaka Waisrael wanaenda utumwani Babeli.

Sasa malkia wa Sheba alirudi lini kulichukua?
 
Jaman malkia wa sheba alienda Israeli wakati wa mfalme Suleiman na sanduku liliendelea kuwapo Israel miaka mingi mbele mpaka utawala wa mfalme Yosia mpaka Waisrael wanaenda utumwani Babeli.Sasa malkia wa Sheba alirudi lini kulichukua??????
Hujanielewa, Malkia wa Sheba alikuwa ni Bibi yake Haile Sellasie na ni miongoni mwa wake za Mfalme Suleiman
 
Jaman malkia wa sheba alienda Israeli wakati wa mfalme Suleiman na sanduku liliendelea kuwapo Israel miaka mingi mbele mpaka utawala wa mfalme Yosia mpaka Waisrael wanaenda utumwani Babeli.Sasa malkia wa Sheba alirudi lini kulichukua??????
Waislam, Wakristo na Wayahudi wanaamini kuwa Malkia wa Sheba alichukua vitu vya thamani sana na kumpelekea Mfalme Suleiman kwa usafiri wa ngamia.

Lengo ni kupima HEKIMA yake na alimjaribu kwa mambo mengi tu kwasababu habari za Hekima ya Suleiman wakati huo ilivuma sehemu kubwa ya dunia.

Hatimaye Mfalme Suleiman alimtamani / alimpenda Malkia wa Sheba na kumuoa. Menelik ni Mwanae na Haille Sellasie ni Nyanya yake
View attachment 2046609
 
Haya Mambo yanapasua kichwa Sana inasemakana waliojenga hekalu la kuhifadhi Hilo sanduku walipewa karatasi zenye Mambo ya Siri na mfalme suleiman, wakatokea jamaa wakawavizia na wakawaua hao wajenzi wa hekalu na kuchukua hizo karatasi zenye Siri Sasa Hawa jamaa baada ya kuchukua karatasi za Siri ndio wakaanzisha kitu kinaitwa Freemason upo hapo
 
Hujanielewa, Malkia wa Sheba alikuwa ni Bibi yake Haile Sellasie na ni miongoni mwa wake za Mfalme Suleiman
Hata kama nikikubaliana na wewe bado haitaleta mantiki .Kwa sababu baada ya mfalme Sulemani wamepita wafalme wengi baada yake na sanduku lilikuwepo hapa namaanisha ili sanduku lichukuliwe na malkia wa sheba ilikuwa lazima kiwe limepotea nyakati za Suleiman au muda kidogo baadae .
 
lilifikaje ethiopia? kuna connection gani kati ya utawala wa Babylon na wa-ethiopia ? yawezekana hawa wa-ethiopia ndiyo wakawa wana halisi wa Israel na wengi wao walikuwa utumwani Misri

Mawasli ni mengi....
soma stori ya king solomoni na queen sheba wa ethiopia, kiufupi hawa walipata mtoto wa kiume aitwaye menelik.. solomon ndie aliemkabidhi menelik sanduku la agano na kuja nalo ethiopia
 
Kuna hekalu fulani la ma jews wa ethiopia ( watoto wa malkia wa sheba waliopatikana pale alipokwenda kuslalimia na kumpelekea zawadi king suleiman mzee wa totoz)
 
Wa
wala mimi sio mfatiliaji wa huyo jamaa, HOJA KWAMBA LIPO MAKKA NI UONGO MKUBWA.... makka lilifikaje kwa mfano...

Ukifatilia vzr utagundua LIMEPOTEA KIPINDI CHA yosia hadi kwa kina YEREMIA hapo....

kuhusu makka ni uzushi mkubwa usio na ushahidi au dalili zozote... kwanza jiulize lilifikaje makka,
Walaw wako wapi? Walipo ndipo sanduku lilipo
 
Hata kama nikikubaliana na wewe bado haitaleta mantiki .Kwa sababu baada ya mfalme Sulemani wamepita wafalme wengi baada yake na sanduku lilikuwepo hapa namaanisha ili sanduku lichukuliwe na malkia wa sheba ilikuwa lazima kiwe limepotea nyakati za Suleiman au muda kidogo baadae .
Hivi kuna mahala nimesema alichukua Malkia wa Sheba?

Mimi nilikuwa naelezea uhusiano wa Malkia wa Sheba na Mfalme Suleiman, na uhusiano wake na Haille Selassie

Kuhusu sanduku kuwa Ethiopia ni Rastafarians na wana dini wengine ndio wanaoamini hivyo.
 
Back
Top Bottom