Johnny Sins
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 2,537
- 3,873
[emoji23][emoji23]chaiLipo Ethiopia na linalindwa kinoma mwaka huu January walikufa watu zaidi ya mia nane wakijaribu kulilinda.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23]chaiLipo Ethiopia na linalindwa kinoma mwaka huu January walikufa watu zaidi ya mia nane wakijaribu kulilinda.
Liko ugweno kifula. Alileta mjerumani mmoja anaitwa fucsHuu ni mfano wa sanduku la agano ambalo wana wa Israel waliambiwa watengeneze na Mussa wakiwa nyikani wakitoka Egypt (Misri) wakielekea promised land (Nchi ya ahadi). Sanduku hilo lilikuwa ni kama box la mbao lililotengenezwa na aina moja ya mbao inayoitwa (acacia wood) iliyofunikwa na dhahabu. Lilikuwa la urefu wa 1.15 metres, upana wa 0.7 metres na kimo cha 0.7 metres.
Ilikuwa inabebwa na mishikio miwili mirefu ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa mbao hiyo ya acasia ambazo pia zilikuwa zimefunikwa na dhahabu. Juu ya sanduku kuliwekwa makerubi wawili waliokuwa wamegeukiana mabawa yao yakiwa yamegusana. Uwepo wa Mungu haukuwepo ndani ya sanduku bali ulikuwa juu yake katikati ya hao makerubi.
Uwepo wa Mungu juu ya sanduku hilo ulikuwa kama nuru. Kuhani mkuu alipaswa kufunika macho asiione nuru hiyo ("hakuna mwanadamu anionaye na akaishi" Kutoka 33 : 20) kila alipokuwa akiingia lilipokuwa sanduku ambapo ni patakatifu pa patakatifu.
Hapa ndipo ambapo Mungu alipokuwa akiionana na Musa. Sanduku hili lilikuwa likibebwa na wana wa Walawi pekeyake hakuna mwingine aliyeruhusiwa kulishika, yeyote aliyedhubutu kulishika pasiporuhusiwa alikufa papohapo. Hao makerubi wawili wanawakilisha utukufu wa Mungu. Ndani ya sanduku hili kulikuwa na:
Sanduku hilo lilikuwa linakaa patakatifu pa patakatifu, chumba cha ndani kabisa katika hema la kukutania. Aliyekuwa anaruhusiwa kuingia mahala hapo lilipokuwa sanduku hilo ni kuhani mkuu na alikuwa anaruhusiwa kuingia mara moja kwa mwaka. Kabla ya Kuhani mkuu kuingia patakatifu pa patakatifu alikuwa ni lazima aingie na damu ya mwana kondoo kwa niaba ya dhambi zake yeye mwenyewe na dhambi za wana wa Israel.
- Mawe mawili yaliyokuwa yameandikwa amri kumi za Mungu
- Fimbo ya Aron iliyoota mauwa
- Chombo cha dhahabu kilichokuwa na manna waliyokula wana wa Israel nyikani
View attachment 1760924
Sanduku la agano lilikuwa ndani ya hekalu lililojengwa na Solomon mpaka hekalu hilo lilipokujwa kuvunjwa mikononi mwa utawala wa Babylon ukioongozwa na Nebuchadnezzar. Kilichotokea kwa sanduku hilo hakijulikani ingawa haiwezekani kuwa lilichukuliwa na majeshi ya Babylon kama vilivyochukuliwa vyombo vingine vya hekalu kwasababu katika list ya vitu walivyovichukua sanduku la agano halikutajwa.
Halitajwi kati ya vyombo vilivyopelekwa Babiloni hekalu lilipohabiriwa mwaka wa 607 K.K. wala halitajwi kati ya vyombo vilivyorudishwa Yerusalemu baadaye.—2 Wafalme 25:13-17; Ezra 1:7-11
Kulingana na baadhi ya vyanzo vya habari inasemekana kuwa mfalme Josiah, mmojawapo wa wafalme wa mwisho kutawala enzi za hekalu la kwanza, kutokana na unabii uliokuwa umetolewa alijua kuwa Jerusalem itavamiwa na Babylon, akalificha sanduku la agano.
Alipolificha sanduku imekuwa kitendawili. Chanzo kingine cha habari kinasema kuwa mfalme Solomon alionyeshwa kuwa Hekalu litakujwa kuvunjwa na majeshi ya Babylon, kwahiyo akaandaa pango karibu na bahari ya shamu (dead sea) ambapo Josiah akaja kulificha sanduku.
Na pia inasemekana nabii Yeremia (Jeremiah) alilificha sanduku chini ya Hekalu lililojengwa na Solomon.
HEKALU LA MBINGUNI
Sio wote wakigusa wanakufa,Wana wa Lawi walikuwa na ruhusa kuligusa.Nafikiri hao Walawi ndo walilihamishaSasa lilibebwaje ikiwa kuligusa tuu UNAKUFA.
Khaaa! Jamaniliko chato kata ya ibungagilagwanana
Du,hilo la malaika jibril ungelianzishia uzi wake hapa tunazungumzia sandusky la aganolililokua Makka sio hili la agano ni lile la malaika jibril alilompatia Mtume.. na lilionekana mwaka 2015 wakati wa upanuzi wa msikiti ndipo viongozi wa kanisa la orthodox wakalifuata kwa escot ya meli za Mrusi mpaka kwenye Bara barafu la antactica.
Wakati wa uhai wa Yesu, hekalu takatifu katika Yerusalemu lilikuwa ndilo nguzo muhimu katika maisha ya kidini ya Kiyahudi. Hekalu ilikuwa mahali ambapo dhabihu za wanyama zilikuwa zinafanyiwa na ibada kwa mujibu wa sheria ya Musa iliyofuatwa kwa uaminifu. Waebrania 9: 1-9 inatuambia kwamba katika hekalu pazia ilitenganisha pahali takatifu zaidi ya patakatifu – mahali ambapo uwepo wa mungu uishi ulimwenguni- kutoka kwa mahali pengine Hekaluni ambapo watu waliishi. Hii iliashiria kuwa binadamu alitenganishwa kutoka Mungu na dhambi (Isaya 59: 1-2). Ni kuhani mkuu tu aliyeruhusiwa kupita zaidi ya hii pazia mara moja kila mwaka (Kutoka 30:10, Waebrania 9: 7) aingie katika uwepo wa Mungu kwa ajili ya waisraeli wote na kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zao (Mambo ya Walawi 16).
Hekalu la Sulemani lilikuwa dhiraa 30 kuelekea juu (1 Wafalme 6: 2), lakini Herode alikuwa amezidisha urefu hadi dhiraa 40, kulingana na maandiko ya Josephus,mhisitoria Myahudi wa karne ya kwanza. Hakuna uhakika kwa kipimo halisi cha dhiraa moja, lakini ni salama kudhani kwamba pazia hili lilikuwa mahali fulani karibu futi 60 juu. Josephus pia anatuambia kwamba pazia hili lilikuwa na upana wa inchi nne na kwamba farasi hata wafungwe kwa kila upande hawangeweza kuirarua dhiraa hii . Kitabu cha Kutoka kinafundisha kwamba pazia hii pana iliundwa kwa mtindo kutoka samawati( buluu), zambarau, na nyekundu, na kitani kizuri cha kusokotwa.
Ukubwa na unene wa pazia unafanya matukio yanayotokea wakati wa kifo cha Yesu juu ya msalaba kuwa wa maana sana. "Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka."(Mathayo 27: 50-51a).
Hivyo, je,tunafanya nini kwa hili? Ni umuhimu gani dhiraa hii ilyopasuka inayo kwetu siku hizi? Zaidi ya yote, kuraruriwa kwa dhiraa wakati wa kifo cha Yesu kuliashiria kidrama kwamba kafara yake, kumwaga damu yake mwenyewe,kulikuwa upatanisho wa kutosha kwa ajili ya dhambi.Kuliashiria kwamba sasa njia ya kuingia Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa wazi kwa watu wote, kwa wakati wote, Wayahudi na Mataifa.
Wakati Yesu alikufa, dhiraa iliraruka, na Mungu akatoka mahali pale kwamba kamwe hangeishi tenai katika hekalu zilizojengwa na binadamu (Matendo 17:24). Mungu alikuwa amemalizana na hekalu hilo na mfumo wake wa kidini, na hekalu na Yerusalemu ziliachwa "zikiuzunika kwa ukiwa" (kuharibiwa na Warumi) katika mwaka 70 A.D., tu kama Yesu alitabiri katika Luka 13:35. Bora tu Hekalu lilisimama, liliashiria kuendelea kwa Agano la Kale. Waebrania 9: 8-9 inarejelea umri uliokuwa unapita mara tu agano jipya liliimarishwa (Waebrania 8:13
Jaman malkia wa sheba alienda Israeli wakati wa mfalme Suleiman na sanduku liliendelea kuwapo Israel miaka mingi mbele mpaka utawala wa mfalme Yosia mpaka Waisrael wanaenda utumwani Babeli.Kupitia Malkia wa Sheba na kanisa kongwe la Orthodox
Hujanielewa, Malkia wa Sheba alikuwa ni Bibi yake Haile Sellasie na ni miongoni mwa wake za Mfalme SuleimanJaman malkia wa sheba alienda Israeli wakati wa mfalme Suleiman na sanduku liliendelea kuwapo Israel miaka mingi mbele mpaka utawala wa mfalme Yosia mpaka Waisrael wanaenda utumwani Babeli.Sasa malkia wa Sheba alirudi lini kulichukua??????
Waislam, Wakristo na Wayahudi wanaamini kuwa Malkia wa Sheba alichukua vitu vya thamani sana na kumpelekea Mfalme Suleiman kwa usafiri wa ngamia.Jaman malkia wa sheba alienda Israeli wakati wa mfalme Suleiman na sanduku liliendelea kuwapo Israel miaka mingi mbele mpaka utawala wa mfalme Yosia mpaka Waisrael wanaenda utumwani Babeli.Sasa malkia wa Sheba alirudi lini kulichukua??????
Mkuu weka wazi nafikiri Sote tungependa kufahamuMtoa post uko vizuri unaandika ulichojifunza na kukielewa ukikupendeza nitakuomba tu share hoja Fulani inbox kuhusu sanduku hili Sina jawabu la uhakika
ni lanini sasa au hao wenye sanduku wanasemaje???
Hata kama nikikubaliana na wewe bado haitaleta mantiki .Kwa sababu baada ya mfalme Sulemani wamepita wafalme wengi baada yake na sanduku lilikuwepo hapa namaanisha ili sanduku lichukuliwe na malkia wa sheba ilikuwa lazima kiwe limepotea nyakati za Suleiman au muda kidogo baadae .Hujanielewa, Malkia wa Sheba alikuwa ni Bibi yake Haile Sellasie na ni miongoni mwa wake za Mfalme Suleiman
ukwel ambao weng hawatataka kuukubalLipo Ethiopia mpaka leo hii hapa
soma stori ya king solomoni na queen sheba wa ethiopia, kiufupi hawa walipata mtoto wa kiume aitwaye menelik.. solomon ndie aliemkabidhi menelik sanduku la agano na kuja nalo ethiopialilifikaje ethiopia? kuna connection gani kati ya utawala wa Babylon na wa-ethiopia ? yawezekana hawa wa-ethiopia ndiyo wakawa wana halisi wa Israel na wengi wao walikuwa utumwani Misri
Mawasli ni mengi....
Walaw wako wapi? Walipo ndipo sanduku lilipowala mimi sio mfatiliaji wa huyo jamaa, HOJA KWAMBA LIPO MAKKA NI UONGO MKUBWA.... makka lilifikaje kwa mfano...
Ukifatilia vzr utagundua LIMEPOTEA KIPINDI CHA yosia hadi kwa kina YEREMIA hapo....
kuhusu makka ni uzushi mkubwa usio na ushahidi au dalili zozote... kwanza jiulize lilifikaje makka,
Hivi kuna mahala nimesema alichukua Malkia wa Sheba?Hata kama nikikubaliana na wewe bado haitaleta mantiki .Kwa sababu baada ya mfalme Sulemani wamepita wafalme wengi baada yake na sanduku lilikuwepo hapa namaanisha ili sanduku lichukuliwe na malkia wa sheba ilikuwa lazima kiwe limepotea nyakati za Suleiman au muda kidogo baadae .