Sanduku la Agano yawezekana limefichwa na makundi ya siri kama Priory of Sion?

Jamiiforums ni kisima Cha maarifa na sio matusi. Kwa wale wenye kupenda mjadala huru na sio matusi karibuni. .

Kuna conspiracy nyingi sana mojawapo ni hiyo niliyosema kuwa ancient aliens threory Ina suggest hiki kifaa kilikuwa kama silaha. Na wanaoamini it is scientific made, ku connect na viumbe wa sayari nyingine ambao wanajulikana kama extraterrestrial πŸ‘Ύ

Hawa viumbe waliaminika kuwa ni miungu kumbe lakini walikuwa ni viumbe vya kawaida. Mbali na wana wa Israel haya masanduku yalikuwa pia yalipatukana kwenye asili za watu wengine. Dunia ya Leo sio dunia ya kuzungumza bila ushahidi kwamba watu wanaweza connect dots kitu flani kwa nini Kiko hivi na vile. .

Mijadala hii pia haijaanza Leo hata wenzetu wakenya hapo na duniani inaendelea siku nyingi. Mfano:

https://www.JamiiForums.com.com/ind...ts-caused-nasty-sores-to-its-handlers.181778/


Sijatulia coz Niko road ila nikitulia nitaonyesha asili ambazo mpaka Leo hii wanafanya Mila za sanduku za agano kwa kirefu. Ila kifupi
1. Ethiopia
2. Zimbabwe -
3. Japan - Hawa Hawana asili kabisa na wana wa Israel ila mpaka Leo hii wanafanya Ile walk ya jangwani sanduku likiwa mbele Yao

Kuna vitabu vingi vimeandikwa na huyu jamaa anaitwa Erick Von Danineck about ancient gods. Kwa wale wanapenda kumkosea ease vitabu vyake wapate kumkosoa. .

Nitaendelea. .
 
Nianze na Japani
Kuna wajapani wanaamini sanduku lilikuwa na wazee wao kwa sababu wana observe mila ya sanduku ya kutembea jangwani. Wengi wanaamini kuwa sanduku hili liliwafikia wajapan ila cha kushangaza ni utaratibu wao wa kulitanguliza sanduku mbele kama walivyokuwa wanafanya wana wa Israel. Je kweli lilifika Japan?

Amazon product ASIN 0595694276
β€œThe Bible says that when David brought up the ark into Jerusalem, β€œDavid was clothed in a robe of fine linen” (1 Chronicles 15:27). The same was true for the priests and choirs. In the Japanese Bible, this verse is translated into β€œrobe of white linen.” In ancient Israel, although the high priest wore a colorful robe, ordinary priests wore simple white linen. Priests wore white clothes at holy events. Japanese priests also wear white robes at holy events”.
Arimasa Kubo

https://www.youtube.com/watch?v=R8roCXKLhMA

https://www.abovetopsecret.com/forum/thread212055/pg1
 
SHIDA SIO SANDUKU NI NGUVU ZILIZOKO SANDUKUNI,NA JINSI YA KUZITUMIA.SANDUKU WAWEZA KUPEWA NA USIELEWE WALA KUFANYA CHOCHOTE.TATIZO NI ZILE NGUVU NA UFANISI WAKE.
 
Hakuna kitu ni watu wenye akili tu ya kucheza na akili za wajinga..Ukisoma upuuzi mwengine kama unawapa viumbe nguvu kuliko MUNGU...
 
Sanduku la agano zimbabwe:
Kuna ushahidi wa sanduku ile mbao ambao ilitengenezea sanduku nadhani imehifadhiwa makumbusho kuu zimbabwe. Watu hawa na mapadri walitoa vinasaba vyao vipimwe na wengi walionekana wana asili na wana wa Israel. Kuna mzungu aliwahi kulikuta kabisa sanduku hili na waliporudi hawakulikuta, Je limefichwa bado Zimbabwe? Hiyo mbao waliyoitoa kwenye sanduku na kuweka nyingine je ni ya sanduku?
https://www.ctsryan.com/ark-of-the-covenant-found-in-africa-the-stories-behind-the-story/
https://www.denverpost.com/2010/05/29/profs-theory-that-zimbabwe-artifact-is-replica-of-ark-of-covenant-stirs-fierce-response/
https://www.youtube.com/watch?v=sjFDLGr5TKw
https://www.haaretz.com/jewish/2010-05-30/ty-article/scholars-ark-of-the-covenant-claims-spark-african-storm/0000017f-db82-df62-a9ff-dfd7d97b0000
 
SHIDA SIO SANDUKU NI NGUVU ZILIZOKO SANDUKUNI,NA JINSI YA KUZITUMIA.SANDUKU WAWEZA KUPEWA NA USIELEWE WALA KUFANYA CHOCHOTE.TATIZO NI ZILE NGUVU NA UFANISI WAKE.
Hili sanduku lina nguvu kubwa sana:
1. liliangusha kuta za Jericho
2. Liliwavusha wana wa Israel bahari ya shamu
3. Linasemekana bila sanduku kuwepo mana isingeshuka
4. Kulitazama tu lazima ufe ilikuwa hairuhusiwi kulitazama
5. Halikuwa linafunuliwa hili sanduku, mda mwingi lilikuwa covered
6. Image of God appeared on top on this ark of covenant
7. Kulikuwa kunafuka moshi juu ya sanduku katikati ya wale malaika wawili
8. Watu wa jamii ya yuda tu ndio walikuwa wanaruhusiwa kulihifadhi hili sanduku
9. Lazima liwatangulie wao, halijawahi kuwa nyuma yao
10. Ndani yake kulikuwa na fimbo ya Mussa , mana na
11. Wakati sanduku likuwa jangwani mbele yao kuna mwanga ukawa unawatangulia mbele yao kuwaonyesha nyia
12. Liliibiwa hili sanduku ila watu walikufa kwa mionzi, (radiation)
13. Ilikuwa lazima uvae nguo maalumu kwa makuhani waliokuwa wanahufadhi hili sanduku
14. Kuna wana wa Israel walilifungua waone ndani ukatgokea mwanga mkali ndani ya sanduku na kuwaua
nk
 
Sanduku la agano lipo mbinguni, soma ufunuo 11:19

Kisha hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la Agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake.
Hilo sanduku lililotajwa mbinguni ni fumbo juu ya Bikira Maria sio lile sanduku la agano la kale. Sanduku la agano ni kivuli juu ya Bikira Maria! How ....

Baada ya andiko hilo uliloweka ufunuo 11:19 andiko linalofata ni ufunuo 12:1 ambalo linazungumza habari za "na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota 12."

Biblia imekuja kuwekwa chapter na verse baadae sana, kabla ya unaweza kuona Yohana anazungumzia ujumbe mmoja ambao ni Bikira Maria!

Agano la kale ilitabiriwa kuwa Bwana atajitwalia Bikira safi! Na alipoamuru kujengwa sanduku la agano alikuwa anafunua mpango wake wa ukombozi kwa mwanadamu. Kwamba atavaa mwili kupitia huyo Bikira safi na kutukomboa.

Kama mwanzisha mada alivyoandika, sanduku la agano ndani yake kulikuwa na fimbo ya haruni kuwakilisha Ukuhani, amri za Mungu kuwakilisha neno la Mungu, Mana ambayo ni mikate iliyoshuka toka mbinguni ambayo inamwakilisha mwili wake Kristo ambaye mwenyewe alisema yeye ndio chakula cha uzima.

Hivyo kwa ufupi yaliyokuwemo ndani ya sanduku la agano ni fumbo la Kristu mwenyewe na Bikira Maria ndiye sanduku la agano pale alipobeba mimba ya Yesu na fumbo la sanduku la agano likafumbuliwa.

Mfalme Daudi alipoletewa sanduku la agano alicheza mbele yake na lilikaa miezi 3 huko na kitu hicho hicho kilitokea pale sanduku la agano "Bikira Maria" baada ya kubeba mimba ya Yesu na kumtembelea Elizabeth aliyekuwa na mimba ya Yohana Mbatizaji, Yohana mbatizaji alicheza tumboni kwa mama yake! Bikira Maria alikaa huko miezi mitatu pia.

Inasemekana maeneo yaliyotokea hayo, Mfalme Daudi kucheza mbele ya Sanduku la Agano, na Yohana mbatizaji kucheza mbele ya Bikira Maria ni eneo lile lile!

Lakini pia Mfalme Daudi alicheza na kutumia maneno yale yale ambayo Elizabeth aliyatumia mbele ya Bikira Maria " imenitokeaje neno hili hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?" Daudi akiwa mbele ya sanduku la agano yeye alisema "Naye Daudi akamwogopa Bwana siku ile; akasema, Litanijiaje sanduku la Bwana?
2 Samweli 6:9

Hivyo ujumbe wa Mungu juu ya sanduku la agano ulishakamilika tusitegemee tena ujumbe mpya nje ya ukamilisho wa neno la Mungu kuvaa mwili kupitia Bikira Maria!

Sasa wenye alerge wakisikia habari za Bikira Maria anatajwa mniwie radhi! Kadiri unavyomfafanua Bikira Maria unazidi kumfafanua Kristo! Simulizi zima ni ukuu wa Mungu kupitia Yesu Kristo ndio maana tutaona mantiki ya sanduku la agano ni vile ilivyobeba na sio sanduku lenyewe!

Lakini huwezi kufafanua yaliyo ndani ya sanduku bila kulitaja sanduku lilotumika kuhifadhi hilo fumbo.
 
I am Roman Catholic na wakatoliki wengi wanaamini Bikira Maria ndio sanduku, it's a conspiracy
Na wapo walokole wengi pia nao wanaamini kuwa sanduku ni Yesu mwenyewe ndio kaja kumwaga damu ya agao lipya, pia ni conspiracy

Kifupi maana ya sanduku ni nini? Kazi yake ni nini? Ndani ya sanduku kulikuwa na amri kumi za Mungu, fimbo ya Mosses some claims Aaron, mana ambazo zilikuwa zinashuka juu wakiwa jangwani. .

Hivi vitu viliashiria nini? Kwa nini sanduku kiwe interpreted kama Yesu au Bikira Maria 😊
 
Nimepata mshangao mkubwa sana ambao pengine sitakuja kuusahau kufuatia ulichoandika hapa. Ngoja nikae kimya ili isionekane ninakashifu imani za watu lakini kwakweli katoliki bado sana kulielewa neno la Mungu.

Nawaombea tu neema ili macho yenu ya rohoni yafunguke mpate kumfahamu Yesu Kristo na kujua kwanini hasa alikuja duniani na nini kinatokea pale mtu anapomuamini yeye.
 
Umewaza kidhehebu, badala ya kuchallenge andiko langu umeishia kuhukumu Kanisa Katoliki kuwa halijui hata kusudio la ujio wa Kristo! Bora hata ungesema mimi binafsi sijui neno! Simply mna ignorance ya kiroho kubwa sana kama Mafarisayo!

Mnahisi mnajua neno nyie binafsi kuliko waliokusanya na kuviweka pamoja vitabu vya Biblia! Kwamba mnajua sana kuliko Kanisa lenye miaka ya 2000 likipokezana mafundisho kwa kuyatunza kwa mfumo usioweza kuvurugwa kibinadamu!

Nyie mna sehemu tu ya ukweli, ukweli mwingi utaukuta Kanisa Katoliki na ukweli wote anao Mungu pekee! Usilojua ni kiza! Pengine hili ulilosoma limekushtua kidogo! Siku ukijua kweli juu ya meza ya Bwana si utazimia? Kuwa mtafiti wa neno la Mungu kama waberoya acha mentality ya kuamini ulichosimuliwa tu! Anza kwanza ku challenge your source of facts ili uiamini.
 
shukran
 
Shukraan kwa mchango mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…