Sanduku la Agano yawezekana limefichwa na makundi ya siri kama Priory of Sion?

Sanduku la Agano yawezekana limefichwa na makundi ya siri kama Priory of Sion?

Hao wa Ethiopia wahuni tu!!Hata wamasai wa Monduli wanaweza kuchonga wakasema lipo Kwao...
Kwaiyo Mungu hawezi kulilinda?
I
Nianze na Japani
Kuna wajapani wanaamini sanduku lilikuwa na wazee wao kwa sababu wana observe mila ya sanduku ya kutembea jangwani. Wengi wanaamini kuwa sanduku hili liliwafikia wajapan ila cha kushangaza ni utaratibu wao wa kulitanguliza sanduku mbele kama walivyokuwa wanafanya wana wa Israel. Je kweli lilifika Japan?

Amazon product ASIN 0595694276
“The Bible says that when David brought up the ark into Jerusalem, “David was clothed in a robe of fine linen” (1 Chronicles 15:27). The same was true for the priests and choirs. In the Japanese Bible, this verse is translated into “robe of white linen.” In ancient Israel, although the high priest wore a colorful robe, ordinary priests wore simple white linen. Priests wore white clothes at holy events. Japanese priests also wear white robes at holy events”.
Arimasa Kubo

https://www.youtube.com/watch?v=R8roCXKLhMA


https://www.abovetopsecret.com/forum/thread212055/pg1

shukraani kwa mchango mkuu
 
Nabii Yeremia alifahamu fika kuwa Yuda angeenda utunwani babeli,kutokana na uasi wao kwa Mungu ,hivyo nabii Yeremia alilificha sanduku Hilo kwenye pango mlimani ,ili lisije likachukuliwa na mataifa +(babeli).lakini pia haidhuru kitu kwa kuwa sanduku la agano lilihusu mfumo wa ibada za agano la kale,kwa hyo Mambo yote yaliyokuwepo yalikuwa Ni mfano wa Mambo halisi yaliyoko mbinguni ,kwa hyo kwa nyakati hizi hayapo Tena kwa kuwa hata Hilo agano la kale ilikuwa Ni Kati ya Mungu na Israel peke yake.
Aisee
 
Kumbe Mungu aliwashushia chakula waisrael directly toka mbinguni.
Kwa nini hawafanyii hii favor na wengine wanaokutwa na baa la njaa kama kule Turkana Kenya?
 
Kuna vitu vingine vipo ili vilete Jaribu kwako wewe mwanadamu
Sidhani pia kama mungu alishindwa kumlinda na mkewe na Hila za nyoka pale Eden.

Pia soma Isaya 14:14
Mkuu mimi siamini kwenye Mungu, samahani lakini.
 
Swadaktaa
Kilichomo au faida inayotokana na sanduku ndio msingi wenyewe
Sasa kuna watu linawafaidisha na kwa hakika hawawezi kukubali kulipteza,wajua wazungu wanajua sana kuiba tamaduni na kuziboresha kwa manufaa yao.
 
Mkuu mimi siamini kwenye Mungu, samahani lakini.
Sasa unaamini kwenye nini.

Kwa taarifa yako hakuna mtu asiyeamini. Kama huamini Mungu basi unamwamini shetani. Huwezi ukakosa upande. If you are not for God, you are for satan. (FACT)


JESUS IS LORD.
 
Sasa unaamini kwenye nini.

Kwa taarifa yako hakuna mtu asiyeamini. Kama huamini Mungu basi unamwamini shetani. Huwezi ukakosa upande. If you are not for God, you are for satan. (FACT)


JESUS IS LORD.
Usiseme hakuna mtu asiyeamini. Atheist hawaamini uwepo wa Mungu na shetani.

Sina upande na nikifa nikikutana na mmojawapo cha moto watakiona.
 
Waasalam

Anaandika,
DaVinci XV,

View attachment 2408231

Naam
Inajulikana na kuelezwa dhahiri katika Imaani na maandiko tofauti tofauti ya kwamba miongoni mwa vitu vikubwa na vitakatifu basi huwezi kuacha kulitaja sanduku la Agano , au Sanduku la Ushuhuda kama wengine wanavyoliita.

Utakatifu wa Sanduku hili inaelezwa kuwa Makuhani walilazimika kulibeba kwa kulishika katika sehemu maalumu (-Fimbo) ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kubebea sanduku na haikupaswa kuligusa sanduku lenyewe, na sababu ni kwamba utukufu wa Mungu na uwepo wake hauwezi kuguswa na mwanadamu.
Maana sanduku lenyewe lilikuwa ni utambulisho wa uwepo wa M/mungu duniani tazama andiko la (KUTOKA 25:22)

Nadhani wengi baina yetu si wageni wa hili na wanatambua mengi kuhusu sanduku hili takatifu, sitohitaji kuingia ndani zaidi kuelezea sanduku hili , bali nitamega kidogo na kujikita zaidi katika msingi wa maada.

VILIVYOMO NDANI YA SANDUKU

View attachment 2408232

Sanduku hili takatifu lilihifadhiwa vitu tofauti tofauti vitakatifu ikiwemo

1- Mawe mawili matakatifu ambayo yaliandikwa Amri kumi za Mungu katika zama za Musa

2- Fimbo ya Harouni ambayo ina muujiza wake pale ilipochipua Maua pale MwenyeziMungu alipowaonyesha waisraeli , Kuhani aliyemchagua ambaye ni Harouni (nadhani wengi wetu wanauelewa mkasa huu)

3- Na mtungi ambao ulikuwa na Chakula Manna ,
Manna ni chakula maalumu ambacho kiliweka muunganiko kati ya M/Mungu na wanaisraeli , Na katika Imani ya dini ya kiislamu inaeleza dhahiri wakati Waisrael walipoihama misri kuelekea Nchini kwao basi M/mungu Aliwarudhuku chakula kutoka katika Pepo yake ambacho ni Manna na Salwah.

View attachment 2408236

Na vyote hivyo katika vitu vilivyomo kwenye Sanduku vilikuwa na Utambulisho au maana zake , Ambazo ni Sheria, ukuhani( ukuu), na utoaji wa M/mungu.
Na kama wanatheolojia wengi walivyoeleza.,
Nadhani pia umeona utakatifu wa vitu vilivyohifadhiwa katika Sanduku la M/mungu.

UPORAJI NA BAADHI YA MAENEO DHAHANIA JUU YA LILIPOFICHWA SANDUKU LA AGANO

View attachment 2408238

Sanduku hili lilitengenezwa kwa mbao kama biblia inavyotanabahisha vyema , kisha ikafunikwa na dhahabu safi, na sanduku hili la Agano mda wote lilihifadhiwa katika hekalu

Na mara kadhaa historia imeonyesha tawala tofauti tofauti kulipora na kuondoka nalo
Mfano wafilisti walifanikiwa kuliteka na kulipeleka kwa Mungu wao lakini Athari zake lilipelekea kuzuka kwa ugonjwa wa Tauni katika jamii yao.

Sanduku hili limeonyeshwa simulizi nyingi zinazohusu kupotea kwake na kupatikana.

Lakini mara ya mwisho sanduku hilo kuonekana ni wakati wa uvamizi wa wababyloni chini ya mfalme Nebuchadnezzer kiasi cha miaka 500 (B.C)
hivi kabla hajazaliwa masihi Yesu mtoto wa maryam walipovamia Israel na kulivunja hekalu la Suleiman na huko ndio haswa kulihifadhiwa sanduku hili la Agano.


View attachment 2408237
Nebuchadnezzer

Na vivyo hivyo Hadithi nyingi zikielezea namna tofauti tofauti ambazo namna hizo hazina ithibati ya lilipofichwa sanduku hilo la Agano
Wengine husema sanduku lilifichwa Na
Mfalme Josiah baada ya kupokea Utabiri wa uvamizi wa wababyloni

Wasomi wengine hudai sanduku hili limehifadhiwa huko Makka chini ya Al-Kaaba, na haliwezi patika kwa maana waislam hawawezi kuruhusu sehemu hiyo takatifu kuchimbuliwa ili tu kutafuta Sanduku.

Na wasomi wengine wanataja sehemu tofauti tofauti ikiwepo ethiopia na Roma huko Italy.

Nadhani kwa kiasi tumejaribu kumega muktadha wa kihistoria juu ya Sanduku la Agano, ambao wengi wetu tunautambua.

View attachment 2408250

JE, INAWEZEKANA SANDUKU LA AGANO LIMEFICHWA NA JAMII ZA SIRI (Kama PRIORY OF SION)

Priory of sion au Prieure de sion (au makundi mengine ya siri kama Illuminant), ni nini??? Hiyo ni mada nyingine inayohitaji nyuzi yake


View attachment 2408240

Unakumbuka kuhusu Last supper ??, mlo wa mwisho wa Bwana Yesu na wanafunzi wake
Unaikumbuka vyema ile picha iliyochorwa na mchoraji na mwanasayansi hodari Leornardo Da Vinci aliezaliwa huko Vinci Italy???

Basi kama ujuavyo katika karamu yoyote , au hafla vitumikavyo ni vyombo.
Ushawahi kusikia kuhusu Holy grail kile kikombe alichotumia bwana yesu kunywea kinywaji katika mlo ule wa mwisho na wanafunzi wake.???
View attachment 2408249
Kikombe ambacho katika nyaraka tofauti tofauti zilizofichwa kimeelezwa kuwa na maajabu yaso kifani kwa yoyote aliyekitumia.

Kuna ambao , walitumia kunywa kinywaji kwa kutumia holy grail na kufanikwa kupona maradhi sugu na wasiumwe tena, kupata nguvu sisizo kifani, Kufa na kufufuka, kusafiri moja kutoka sehemu mmoja au nyingine ya umbali wa kilometa tele kwa mda mchache sana usio wa kawaida, kuwa na ufahamu mpana sana, mamlaka , na Amani ya moyo
Kuna waliotumia wakawa na ufahamu usio kifani na ujuzi wa kuvumbua mambo mengi ambayo kwa wengine si kawaida kama wanasayansi mashuhuri akiwemo Leornado Da Vinci mwenyewe ambaye baadhi ya maandiko yake ya siri yamefichua haya
Lakini ikumbukwe huyu Leornardo DaVinci ni member mkubwa sana Wa kundi la Priory of sion ambalo limehusishwa na kuwa na viongozi wengi wa kidini kama Mapapa na hata wanasayansi wakubwa na watu maarufu kama Sir Isaac Newtons , Boticelli ,na wengineo.
Na ndio kusema kwamba , wanasayansi wengi (sio wote) walikuwa katika makundi makubwa ya Siri, kutokana na uwezo uliopatikana kutoka kwao.

View attachment 2408248
Sir Isaac

Cha Ajabu zaidi usichokijua ni baadhi ya nyaraka hizo zinadai kwamba Kutokana na neema na maajabu ya holy grail kikombe hiki kimehifadhiwa kusikojulikana na mhusika mkuu ni hili kundi la priory of sion kama baadhi ya nyaraka za siri za mwamba Leornardo da Vinci zinavyodai, na si tu holy grail bali vitu vingi vitakatifu vimehifadhiwa na kufichwa kusikojulikana na makundi haya siri ili viendelee kuwanufaisha na kuwapa faida.

N.B Lakini nyaraka hizi hazina ushahidi wa kutosha kuzipa nguvu ili kiwe kitu cha kuaminika
Nani anajuaye????


(Tuachane na hapo Hii mada Holy grail panapo majaliawa tutaitafutia nyuzi yake)

Wakati mmoja nilipata kupitia documentary moja ambayo muandishi wake anadai yeye ni katika member wa makundi kati ya kundi mojawapo la siri na kubwa hapa duniani.

Moja kati ya vipengele vya documdntary hiyo vinaelezea.

Dunia yetu imeaminishwa ya kwamba sanduku takatifu la Agano limepotea na yakitajwa maeneo tofauti tofauti yakwamba huenda limehifadhiwa huko

Documentary inadai makundi haya makubwa (priory of sion, Illuminati ) , au jumuiya nyingine ya siri yoyote ya siri Huenda wana uhusiano na kupotea kwa sanduku la agano.

View attachment 2408244
Wasomi wale wanaijua Biblia vizuri sana, kuliko kawaida, ni miongoni mwa kitabu chao cha mwongozo.
Wanaelewa maneno ya siri na yenye faida juu ya kutawala .
Wameweza kuwafanya watu kuwa mpumbavu na wajinga juu ya maandiko na mafumbo tofauti tofauti ya dini.
Wana uelewa mkubwa sana juu ya Faida za ulimwengu wa kiroho unaopatikana kutokana na sanduku lile, na vitu vingine vitakatifu vilivyofichwa hivyo wakatengeneza nadharia nyingi sana kuaminisha ulimwengu juu ya sanduku ili kuwapoteza watu na wao kuendelea kufaidika na vilivyomo.

Sanduku halikufichwa huko Ethiopia kwa malikia wa Sheeba, wala halikufichwa kwa waarabu pale Makka wala halikufichwa kwa Wayahudi pale Israel, wala halipo kwa waitaliano pale Rome.

View attachment 2408245

Akili , Maarifa na Nguvu za utawala za makundi haya zinatokana na vitu kama hivyo vitakatifu ambavyo vimehifadhiwa na kutumika katika ulimwengu wa kiroho zaidi kama vilivyohifadhiwa vitu vingine
(Holy grail, Kinubi cha mfalme Daudi na hata hilo sanduku la Agano na vinginevyo)

Vitu kama hivyo (sanduku la Agano) vinawapa nguvu.
hawaogopi kifo, inawafanya wawe na nguvu Inawapa udhibiti wa akili na mwili wao na wanadamu wengine.
Inawapa mamlaka ya kutawala dunia na nguvu nyingine nyingi
Endapo vitu hivi vitarudi katika mkono sahihi basi hapo hapo ndipo nguvu itarud kama ilivyo kawaida

Na hapa ndipo kiu ya kumsubiri mwana wa Adamu (Issa au Yesu mtoto Wa marym) inapozidi kuwa kubwa ili aje kufichukua mengi msiyoyajua.

Naam nikipata wasaa nitaambatanisha jina la documentary ile

Kipindi fulani wakati najaribu kupata darasa kuhusu
Holy grail jinsi ilivyofichwa na kutumika kunufaisha watu ndipo nikajiuliza yawezekana hata sanduku la Agano ambalo sisi bado hatujui lilipo nalo limehifadhiwa na hawa mabwana wakubwa wa Dunia. Ili waendelee kunufaika na matunda ya faida zake

Wewe unadhani vipi!??

Shuqraani

DaVincii XV
Kwa sasa hivi hata wakilificha wanakojua halina tena kazi,
 
Sasa najiuliza iweje Mwanga na Giza vikae pamoja,Kama historia inasema hilo sanduku iliwahi kuibwa na wafilisti na likawaletea shida mpaka wakaamua kulirudisha Je leo huo utukufu uliopo kwenye sanduku umendoka sasa?

Kama haujaondoka basi sidhani kama kuna jamii yeyote ya siri inayofanya mambo ya Giza itafanikiwa kuvitumia vitu hivyo kinyume na kazi za Mungu.

Kuhusu liko wapi sanduku mpaka sasa ni kitendawili ila nilishaona documentary ya BBC wanadai lipo Ethiopia milimami huko kuna dhehebu Fulani lina hekalu na wana askari wao waumini wanavaa mavazi Fulani meupe na wana silaha na wako tayari kufa kulilinda, hawaruhusu mtu yeyote kuingia humo zaidi ya mtu mmoja tu ambaye ndiye hulinda hilo sanduku na akifa tayari kuna mwingine alishaandaliwa kufanya kazi hio,na huyo mtu huwa hatoki humo hekaluni.

Hata mwandishi aliyefika hapo hakuruhusiwa hata kuingia ndani ya uzio wa hekalu maana liko fenced,aliongea akiwa nje tu,lakini walikiri wanalo hilo sanduku la agano ila hawezi kuliona kutokana na masharti yao.
Kwa sasa sanduku ni kama Boksi tu halina kazi...Mungu hakai kwenye masanduku bali kwenye mioyo iliyopondeka

Unahitaji kumtafuta Mungu na siyo sanduku.

Sheria za Mungu haziandikwi tena kwenye Vibao vya nyama bali katika mioyo ya wanadamu

Ebrania 8:10
 
Kwa sasa sanduku ni kama Boksi tu halina kazi...Mungu hakai kwenye masanduku bali kwenye mioyo iliyopondeka

Unahitaji kumtafuta Mungu na siyo sanduku.

Sheria za Mungu haziandikwi tena kwenye Vibao vya nyama bali katika mioyo ya wanadamu

Ebrania 8:10
Aiseee
 
Kwa wale wasomaji wapya wa JF, hili Sanduku limeshajadiiwa kwa kina sana. Pitia hapa chini.

 
Wasomi wengi
Pasi na ithibati walidai hivi kwamba liliibwa na malikia wa sheeba na kuhifadhiwa huko Ethiopia, lakini hakuna ushahidi wa moja kwa moja kama ilivyo kwa maeneo mengine yanayosadikaka kuwepo.
Kama inasemwa hakuna Ushahidi kwamba Sanduku la Agano lilienda Ethiopia, Je! Kuna Ushahidi gani kwamba hizo Secret Societies ndo zimeficha hilo Sanduku la Agano?
 
Kama inasemwa hakuna Ushahidi kwamba Sanduku la Agano lilienda Ethiopia, Je! Kuna Ushahidi gani kwamba hizo Secret Societies ndo zimeficha hilo Sanduku la Agano?
Swali lako, jibu
Lipo kwenye nyuzi yote hapo mkuu,
Kama hukusoma ungesoma
, na kama ulisoma hebu jaribu kurudia kuisoma
 
Swali lako, jibu
Lipo kwenye nyuzi yote hapo mkuu,
Kama hukusoma ungesoma
, na kama ulisoma hebu jaribu kurudia kuisoma
Nimesoma ila sikuona Ushahidi zaidi ya kuona Mawazo ya Mtu na Vile ukielezea kuhusu Documentary moja ambayo imejaribu kuelezea kuhusiana na kile ulichokiwakirisha hapa.
 
Nimesoma ila sikuona Ushahidi zaidi ya kuona Mawazo ya Mtu na Vile ukielezea kuhusu Documentary moja ambayo imejaribu kuelezea kuhusiana na kile ulichokiwakirisha hapa.
Na ndiyo maana hata heading ipo katika mfumo wa kiulizo,
 
Yaani sanduku lile haliwezi chukuliwa hovyo hovyo tu bila Mungu kuchagua watu anaowataka na kwa sheria zake lkn km waki kiuka sheria anazo weka Mungu kulihusu basi ni kifo pia!

SASA eti leo azuke mnuka mikojo mmoja! asiyjua hata sheria za sanduku alishike shike tuuuu! weeee! kwanza hata weye kulitaja ivi sijui hizi nguvu umetoa wapi!!.......nina mashaka sana na uhai wako!

kulitaja sanduku si lele mama! ujue!! unatakiwa ule ushibe!! ufunge na kuomba je umefanya hayoooo!.......Wayahudi wali ishi nalo kwa Mazoea, natokeo yake likapotea mazimaaaa!

Mpaka leo wamepigika hao! sina hata hamu!! wayahudi wale ukiwaona walivo pigika nakwambia utalia machozi ya damu!...kisa walilitosa sanduku
 
Sanduku la agano Kuna conspiracy halikuwa Moja yanaweza kuwa yalikuwepo zaidi ya Moja.

1. Kuna kanisa Ethiopia la orthodox lindai sanduku liko Ethiopia na Kuna mtu Yuko appointed kama kuhani kulilinda Hilo sanduku. Ukweli huu ulidhiirika pale watu walipoandamana kulinda sanduku vuguvuhu ya vita juzi kati. Wakazi wa hapa Kuna wayahudi na wana unasaba nao

2. Pia kinasemekana sanduku hili Zimbabwe lilikuwepo pia. Kuna mzungu miaka ya 70 hivi alilikuta akalithibitisha. Japo baadae aliporudi hakulikuta. Ila wakazi wa hapa wana asili na unasaba na wana wa Israel

3. Sanduku hili pia linasadikika lipo limefichwa sehemu nyingi duniani. Mfano Japan, Italy, Israel huko nk

Sanduku hili hata Adolph Hitler alilitafuta sana. Wengi wanaoamini ni kama silaha. Wengi sana wanalitafuta ila in vain na Kuna watu wanaweza kuwa wanayalinda haya masanduku sio kweli kwamba hayapo hapa duniani. Hilo sanduku wakilitoa tu hivi litaleta maafa makubwa sana kwanza hairihusiwi kulitazama na macho lilikuwa linafunikwa. Very dangerous thing. .
What?? Very dangerous kwanini? Je uhatari huo ni upi?
 
Back
Top Bottom