Sarafu ya Iran yashuka hadi chini kabisa huku kukiwa na mvutano kati yake na Marekani na Ulaya.
Sarafu ya Iran iliendelea kuporomoka siku ya Jumamosi, na kudorora zaidi dhidi ya dola ya Marekani huku kukiwa na sintofahamu kuhusu kukaribia kwa Donald Trump katika Ikulu ya White House na mivutano na nchi za Magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran.
Sarafu ya Iran maarufu kama (Rial), ilishuka hadi 756,000 kwa dola moja kwenye soko lisilo rasmi siku ya Jumamosi, ikilinganishwa na Rial 741,500 siku ya Ijumaa, kulingana na Bonbast.com, ambayo inaripoti viwango vya ubadilishanaji. Tovuti ya bazar360.com ilisema dola hiyo moja ilikuwa ikiuzwa kwa takriban Rial 755,000.