Sarah Simbaulanga: Mwanamke wa kwanza kuiba pesa ndefu katika historia ya benki zote nchini

Sarah Simbaulanga: Mwanamke wa kwanza kuiba pesa ndefu katika historia ya benki zote nchini

Nani anajua huyu mama yuko wapi sasa? nakumbuka tulishangaa sana miaka ile mwanamke kuiba pesa kama ile!!!

Namfahamu mama Sara Simabaulanga alipo. Kwa taarifa yenu alishatoka jela siku nyingi mno na alikuja kuolewa na mzee Toroha Mohamed Toroha na sasa ni mtu mzima ni kama chotara hivi. Kwa sasa wanaishi Kawe mzimuni.

Ukitaka data zaidi nitakuelekeza mpaka wanapoishi kwani nilikuwa mpangaji wa nyumba yao nao wakiishi hapo hapo na niliondoka hapo mwaka 2007.

Pia kumbuka Mohamed Toroha ndiye aliyemsaidia Sara kukimbilia Uingereza na baadaye naye alikamatwa na magari yake kuleta Tanzania kwani yeye alikuwa akiishi Kenya.
 
Those were the days, the days of our lives.
Gazeti la mfanyakazi ndio lilikuwa kama mwanahalisi ya sasa

Pia baadae lilikuwepo gazeti la Motomoto......Hili kwa kiasi kikubwa nadhani ndo lilikuwa kama Mwanahalisi la sasa
 
Hebu tujikumbushe kesi yenyewe ilivyokuwa....

THE CASE OF THE TRAVELLERS CHEQUES
The case of Sarah Simbaulanga, a National Bank of Commerce (NBC) employee who stole Shs 31.0 million in foreign exchange (mostly travellers cheques) astonished Tanzanians because of the sum of money involved in the theft, the apparent ease with which it was carried out and, the biggest surprise of all, the immediate admission of guilt after the lady had been arrested. The accused looked very calm in the dock. Yes she said it is true to the five counts she was facing. The Principal Resident Magistrate asked her twice if she really understood the charges against her. She confirmed her plea of guilty.

The evidence presented to a packed court in Dar es Salaam was, in abbreviated form, as follows:

Between October 19th and 29th 1987 Simbaulanga and an accomplice named Toroha (whose extradition from Kenya is being demanded by the Tanzanian authorities) stole from the NBC 1,100 travellers cheques worth US$ 390,000 and 200 travellers cheques worth £20,000. Simbaulanga and Toroha had been friends since the early seventies when she had been at Kisutu Secondary school in Dar es Salaam.

She and Toroha hired two rooms at the Skyway Hotel on the night of October 29-30. Simbaulanga had managed to obtain four passports for herself and her three children. They travelled on an Air Tanzania plane to Nairobi on October 31st. They then used some of the travellers cheques to buy five KLM tickets to London. On November 1st and 2nd they made twelve different transactions using $246,000, The Police are still trying to trace the remaining travellers cheques.


The accused then bought five tickets to Nairobi on November 5th, and in Nairobi they carried out further transactions with new travellers cheques they had bought in London. Toroha bought four mini-buses and a pick-up and registered them under the name of his wife Elizabeth.

Later three other suspected accomplices were arrested Simbaulangas NEC Controller, a KLM Sales Manager and a businessman.

On February 10th Simbaulanga was sentenced to 35 years imprisonment, seven years on each count, to run concurrently. But, on February 16th, the Prosecution appealed the case and asked the High Court to issue an order for the sentence to run consecutively. Subsequently, Simbaulanga was sentenced to 28 years in prison.

The case was one of many referred to later by SHIHATA under the heading Tanzanias thriving theft industry
in which it quoted a whole spate of thefts by servants of the NBC from branches all over the country. It estimated the total loss at over Shs 60.0 million.
 
bado una hamu naye huyu bi kiroboto, na jinsi alivyokuwa akizembea na uchafu dar, mweeeee! Nakumbuka alivyokuwa mzito kutolea maamuzi mambo madogo hadi kuingiliwa na Mrema kusafisha mji.
 
bado una hamu naye huyu bi kiroboto, na jinsi alivyokuwa akizembea na uchafu dar, mweeeee! Nakumbuka alivyokuwa mzito kutolea maamuzi mambo madogo hadi kuingiliwa na Mrema kusafisha mji.

Acha kudandia train kwa mbele Ndokyo. Huyu mama ni mfanyakazi wa zamani wa bank ya NBC aliyekomba milioni kadhaa miaka hiyo na kukamatwa. We unamzungumzia nani? au unamaanisha Chipungahelo?
 
Mwenye taarifa atujuze yule fisadi sara simbaulanga yuko wapi?

Huyu mama siku hizi kawa mlokole kampokea Bwana na katubu madhambi yake.
Haya mambo ya kuitana FISADA hata kama mtu kaungama makosa tutaishia kumalizana kwa style ya 'JINO KWA JINO'
 
yupo magomeni fundikira anauza supu ya mapupu na miguu ya kuku vishingo..
 
Huyu mama uko alipo atakuwa anatema mate chini kwa jinsi nchi inavyomung'unywa!!
 
Yalikuwa mapenzi ya hatari.

Aliiba pesa benki kwa kushirikiana na serengeti boyz wake.

Hata ndugu zake hawakutaka kujihusisha na mtu MWIZI!
 
Yalikuwa mapenzi ya hatari.

Aliiba pesa benki kwa kushirikiana na serengeti boyz wake.

Hata ndugu zake hawakutaka kujihusisha na mtu MWIZI!
Siku hizi ukiiba ndugu zako wanakupigia makofi hata ukikamatwa na kushitakiwa watakuwa wanakuja na kujaa mahakamani kukusapoti. Na usipoiba na kushikilia misimamo yako basi utaonekana bonge la juha!!
 
Ninachokumbuka ni kuwa huyu Mama alikuwapua dola za marekani nyingi sana akataka kutoroka nazo nje ya nchi ila kabla hajafanikiwa dili likafumuka wakawa wanafukuzwa mpaka walipo kamatwa na hela mkononi. Nakumbuka kuna wakati yaliwahi toka mashati ya ujiuji (Kitambaa kama cha magauni ya CHARANGA kwa wanaoyakumbuka) yenye picha za dola za marekani tukawa tunayaita SIMBAULANGA.

Kweli kabisa mwanakijiji huyu mama aliwahi, maana enzi zile wizi ulikuwa haulindwi wala kusukiwa mikakati IKULU kama ilivyo sasa ambapo angechukua kiualaini na kuzikuta nje zinamsubiri badala ya kukimbia na bulungutu.

Kweli kabisa nadhani yule mama hakuwa na mpango na zile fedha. Kama kumbukumbu yangu ni sahihi ilikuwa ni kama Traveller's cheques (zinatumika bado siku hizi?) zenye thamani kubwa kama USD laki tatu hivi. Lakini alishirikiana na mumewe(?)

Toroha Mohammed Toroha (munamkumbuka?) ambaye niliwahi kusikia alinunua magari mengi kwa kipindi kifupi.

Walikamatwa wote na maskini alikula miaka 28 jela. Ila yule Toroha alifariki au aliishia wapi?
 
nilikua mdogo kipindi hicho alakini nilikua nafuatilia sana,vipi hebu tupe habari kidogo yupo wapi now.ndie mtanzania mwanamke wa kwanza kuiba kiasi kikubwa cha hela benki kuu,alikammatwa nairobi akijiandaa kwenda majuu.
 
MM Umenikumbusha mbali saana! Enzi ya gazeti la uhuru na katuni zake za Chakubanga, Chupaki N.k. Ingekiuwa leo yule mama angeachiwa tuu, vijisenti vile! Kama mtu anakuwa na Bil 3 na hamna kesi!
 
Back
Top Bottom