Raha ya milele umpe Ee Bwana, apumzime kwa amani, Amina!
Binafsi nimeona mijadala mbalimbali ikimuhusisha Fr. Kitima na namna alivyowatambulisha watu kanisani na namna alivyomkaribisha Rais kuaga mwili wa Marehemu Pengo.
Sehemu kubwa ya mjadala watu wanasema kwamba Fr. Kitima kaonyesha dharau mbele ya Rais
Binafsi natofautiana sana na wanaosema hivyo kwasababu zifuatazo:-
1. Kwanza ikumbukwe Kanisa lilishapiga marufuku viongozi wa kisiasa na kiserikali kuongea kanisani. Hili liko wazi na liko kwenye maandishi yao. Kwanini jana Fr. Kitima alisema "...kama Rais ana neno anaweza kutoa..." Tuwaulize TEC kama lile tamko lao wameshalifuta? Vipi kama Rais angekubali mwaliko huo wa kuongea?
2. Watu waliodogoshwa jana wala sio Rais ila nadhani ni viongozi wa CHADEMA. Wakati anawatambulisha hakutaja jina la CHADEMA badala yake alitumia neno "vyama vingine". Fr. Kitima ameanza lini kuwa mwoga? Alihofia nini kuitaja CHADEMA kwa jina kama alivyoitaja CCM? Hofu yake ilikuwa ni nini?
3. Nakubaliana na wanaosema alionyesha chuki kwa Samia pale alipomtambua Jesca Magufuri na kuwaalika waumini kumshangilia kisha akahanikiza na kibwagizo kuwa "Marehemu alikuwa rafiki mkubwa wa familia yao". Kwa aliyotendewa na serikali haikufanya lolote la maana hata mimi lazima ningefanya action ya kumfanya aone simpendi waziwazi tena nadhani mimi ningefanya zaidi ya ile. Hata hivyo hii haiwezi kuwa sababu ya watu kusema "amemdharau Rais". Kiaje? Walitaka asitambulishe?
4. Rais kuondoka baada ya zoezi la kuaga mwili. Sijui kwanini watu wanatafsiri kwamba "aliamua kuondoka". Hii tafsiri sio sahihi kwasababu kilichompeleka kanisani ni kuaga mwili na tayari amepewa nafasi hiyo anabaki kusubiri nini? Huo ni utaratibu wa kawaida, angealikwa kuhutubia baada ya hotuba angebaki? Kwanini watu walitaka abaki baada ya kuaga wakati tayari shughuli iliyompeleka ameimaliza?
5. Fr. Kitima alikosea sana kutamka "kama ana neno anaweza kuongea". Nadhani hata maaskofu watakuwa walishituka kusikia vile. Sina hakika kama hilo alipanga kulisema au lilishajadiliwa kabla. Pengine neno hilo lilimtoka kwa bahati mbaya (au alijifanya kukosea kwasababu alijua kabisa hawezi kuongea chochote kama hajaandaliwa) kwasababu kimsingi jana kanisani palikuwa sio sehemu ya kutoa salamu za rambirambi. Siku ya kutoa salamu za rambirambi ni siku ya mazishi ambayo ni leo